Wanawake Kanisani: 'Tuna jukumu maalum la kuchukua'
Na Kielce Gussie – Vatican.
Wanawake kutoka kote ulimwenguni walikusanyika jijini Roma mnamo tarehe 9 Machi 2026 katika kushiriki mpango wa pamoja wa Balozi za Uingereza na Australia wanaowakilisha nchi zao mjini Vatican kuhusu mada: "Wanawake wa imani: Viongozi wa wanafunzi wa kesho." Siku moja baada ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8 wanawake kumi na watano wa mataifa kumi na tatu tofauti walianza kozi ya mchana mzima iliyozingatia maslahi yao ya pamoja ya jinsi imani, maadili, na ushiriki wa umma unavyoweza kusaidia kuleta mabadiliko chanya katika Kanisa na katika jamii kwa ujumla. Wanawake hawa walitoka katika vyuo vikuu na mashirika mbalimbali yaliyoko Roma. Kwa muda wote wa siku nzima kikundi kilijadili jinsi uongozi na mitazamo ya wanawake iliyojengwa katika imani inavyochangia katika kushughulikia masuala kama vile ujenzi wa amani, kupunguza umaskini, elimu, na mabadiliko ya tabianchi.
Sio kuwa wa A au B pekee,tunahitaji sana sehemu za marejeo
Kwanza kabisa, wanawake walisikia sauti kutoka kwa Balozi wa Canada, anayewakilisha nchi yake Vatican Bi Joyce Napier; Balozi wa Uswiss anayewakilisha nchi yake Vatican, Bi Manuela Leimgruber; Balozi wa Australia anayewakilisha nchi yake Vatican, Bi Keith Pitt; na Balozi wa Uingereza, anayewakilisha nchi yake Vatican. Wakitafakari kuhusu hotuba ya Balozi Napier, baadhi ya washiriki walielezea uzuri wa kuona mwanamke akiweka usawa katika familia, kazi, na maisha ya kiroho. Hili lilimgusa sana Daniela Niño Giraldo kutoka Colombia, ambaye ni mwanamke aliyeolewa hivi karibuni, anayefanya kazi, ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza. Mkutano huo ulimkumbusha kwamba wanawake hawapaswi "kuogopa kitakachotokea" baada ya kujifungua, Giraldo alielezea. Kuona mfano wa Balozi wa Canada, Mwanamke kulimpa moyo asiogope kusawazisha kazi na umama. Halazimiki kukata tamaa katika misheni yake Kanisani. "Tunahitaji sana sehemu za marejeleo kwa sababu wakati mwingine tunafikiri tunahitaji kuchagua kati ya A au B. Kuona mifano hii kunatupa njia ya kufuata."
Wanawake wana jukumu muhimu
"Ingawa tunasherehekea mafanikio ya wanawake, tunapaswa pia kukumbuka wanawake ambao sauti zao zimezimwa na mazingira yao ya unyanyasaji," Mary Wangithi Mugo kutoka Kenya alisisitiza mwishoni mwa tukio hilo akizungumza kwa lugha ya Kiingereza. Kwa balozi huyu wa vijana wa Talitha Kum na mwanzilishi wa Mfuko wa Sema Nami - shirika lililojitolea kupambana na biashara haramu ya binadamu - tukio hili lilikuwa wito wa kuchukua hatua "kufanya kitu dhidi ya usafishaji haramu wa wanawake.”
Talitha Kum imejitolea kupambana dhidi ya biashara haramu ya binadamu (M. Mastrandrea / Talitha Kum)
Akifanya kazi moja kwa moja na manusura wa biashara haramu ya binadamu, Mugo alisisitiza jinsi wanawake wanavyocheza jukumu muhimu na maalum. Watu wengi hugeukia Kanisa kwa msaada baada ya uzoefu wao, na mara nyingi hupata mapdre. Licha ya kujua unyonyaji ni nini, Mugo alisema, mapadre hawawezi kuelewa uzoefu wa mwanamke. "Hapo ndipo wanawake huingilia kwa sababu tunaelewana. Ingawa sielewi hasa kile ambacho mtu alichopitia kama manusura, kwa mtazamo wangu kama mwanamke, ninaweza kuwaelewa asilimia 90%", alisema. Jukumu la wanawake katika jamii na Kanisa ni tofauti na la wanaume. Sio sawa na ukuhani au kasisi wa kidini. Lakini lengo la tukio hili lilikuwa kusisitiza kwamba wanawake wana jukumu katika Kanisa Katoliki, katika ngazi za mitaa na za ulimwengu wote. "Kama Mkatoliki aliyebatizwa, kama mwanamke, tuna jukumu [mahususi] la kuchukua, haswa linapokuja suala la masuala ya wanawake na masuala ya watoto," Mugo alisisitiza. Kwa wasichana na wanawake wanaotoka katika malezi magumu, kuwaona wanawake katika majukumu ya uongozi katika Kanisa hutoa matumaini. "Haitakuwa njia ya waridi," alielezea, "lakini kuna matumaini kwetu sisi viongozi wajao."
Mazungumzo kwa lugha ya kiswahili ya Sr Mugo: Ninaitwa Mary Wangithi Mugo. Mimi ni mwanafunzi katika shule ya kikuu cha Gregoriana, Roma, na pia mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali kiitwacho Sema Nami Kule Kenya. Leo ilikuwa siku kuu ya kusherehekea wanawake kote ulimwenguni, na kwa kweli kuwaona wanawake viongozi hasa mabolozi wanawake kutoka nchi tofauti, kunaonyesha nguvu ya mshikamano, siku ya wanawake inatukumbusha kwamba kuwawezesha wanawake kunahitaji ushirikiano katika tamaduni, taasisi na pia imani. Kama mtu ambaye anafanya kazi na wanawake wahamiaji na manusura wa biashara haramu ya binadamu kunanikumbusha kwamba wanawake wengi sana bado wanahitaji kusikilizwa. Matukio kama haya yanatukumbusha kwamba, mabadiliko hutokea wakati uongozi, huruma na vitendo vinapokutana Wanawake wanaposaidiana, mabadiliko ya kweli hasa yanawezekana."
Zaidi ya hayo, tukio hilo liliwaonesha wanawake walei katika nafasi za uongozi ndani ya Kanisa, jambo ambalo lilimtia moyo sana Giraldo. Alisisitiza uzuri wa kuona uhusiano wa Kanisa na kikosi cha kidiplomasia. Hii ilimpa tumaini kwa sababu, kama alivyoelezea, "wakati mwingine nadhani niko hapa (Roma) nikisoma kama mwanamke mlei, na sijui nitawezaje kuunganisha vipande hivi vyote. Lakini najua siwezi kuacha." Kuwaona mabalozi wanawake, waandishi wa habari, na wawasilianaji, wanawake walei wakishiriki kikamilifu katika kazi ya Kanisa, kulikuwa chanzo chenye nguvu cha msukumo na matumaini kwa Giraldo.
Mtandao mpya wa usaidizi
Giraldo na Mugo wote wawili walisisitiza jinsi tukio hili lilivyowapatia mtandao wa usaidizi kwa kuwaunganisha na wanawake wanaokabiliwa na changamoto nyingi zinazofanana. Ni mfumo unaoweza kusaidia kuwajenga wanawake. Mugo alibainisha kuwa hii inawakilisha "hatua moja mbele katika kupambana na biashara haramu ya binadamu na unyonyaji wa wanawake.""Sisi, kama wanawake, tunahitaji kufanya kazi pamoja na kuwa na nafasi ambapo tunaungana na kuzungumza na kusaidiana," Giraldo alisisitiza. Hii, alisema, husaidia wanawake kukua pamoja na kujifunza kutoka kwa mitazamo tofauti. Kuunda mtandao huu ni muhimu kwa sababu huwasaidia wanawake "kuelewa kwamba hatuko peke yetu katika mchakato huu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here