Tafuta

Kardinali Zuppi, wakati wa Misa huko Assisi. Kardinali Zuppi, wakati wa Misa huko Assisi.  (ANSA)

Ukraine,Kard.Zuppi huko Assisi:Amani inayowekwa katika silaha pekee ni ya uwongo

Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) aliongoza Ibada ya Misa tarehe 11 Machi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis wa Assisi pamoja na kufanya maombi ya amani nchini Ukraine na ulimwenguni kote.Tukio liliandaliwa na Ubalozi wa Ukraine jijini Vatican,wakati wa maonesho ya masalia ya Mtakatifu Maskini na maadhimisho ya miaka minne ya uvamizi wa Urusi.Kardinali alilaani kitendo chochote cha vita kinacholenga kuharibu miji mizima bila kubagua:Ni uhalifu dhidi ya Mungu na ubinadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maadhimisho ya Misa Takatifu ilifanyika alasiri tarehe 11 Machi 2026  katika Kanisa la juu ya Basilika ya Mtakatifu Francis ili kuomba zawadi ya amani nchini Ukraine. Mpango huo uliandaliwa na Ubalozi wa Ukraine unaowakilisha  Vatican,  kama sehemu ya kuheshimu mabaki ya Mtakatifu Francis, na  kukumbuka miaka minne baada ya kuanza kwa vita nchini humo.  Misa hiyo iliongozwa na Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa Baraza la  Maaskofu wa Italia, pamoja na ushiriki wa takriban mahujaji 70 kutoka jumuiya ya Kiukraine nchini Italia.

Wakati wa misa huko  Assisi
Wakati wa misa huko Assisi   (ANSA)

"Kupitia sala hii ya kwaya," alitangaza Ndug Marco Moroni, OFMConv, Mkuu wa Comvent Takatifu, akiwakaribisha waliokuwepo mwanzoni mwa maadhimisho ya misa hiyo, "wakiwa wameimarishwa na uwepo wa mapadre wengi wa Kiukraine na watu wengi kutoka nchi hiyo iliyojeruhiwa, tunaweka ubinadamu wote mikononi mwa Bwana. Kupitia maombezi ya Mtakatifu Francis, tunamkabidhi Mungu hali ngumu tunayopitia duniani kote, tukiomba amani si kwa Ukraine tu, bali kwa kila mahali palipo na mifarakano.

Misa ya Kardinali Zuppi
Misa ya Kardinali Zuppi   (ANSA)

Na  kwa upande wa  mahubiri, "Katika siku hizi za ajabu," Kardinali Zuppi alisema, "tumepata nyakati za ushiriki mkubwa, ambapo wanaume na wanawake wengi wamekutana na roho ya Ndugu Francis, wakimkuta ndani yake chanzo kisichoisha cha nuru na matumaini katika wakati mgumu kama huu kwa ulimwengu wetu. Mtakatifu Francis anatushika mkono na kutusaidia kutazama ukweli kwa macho halisi ya Kikristo, akitualika kuwa ndugu wanaowafikia ndugu wengine, kama vile tulivyoitwa kuishi kila siku." "Kwa kusaidiwa na ndugu yetu Mtakatifu Francis," Kardinali aliendelea wakati wa mahubiri yake, "tusiogope kutambua kwamba sisi sote ni ndugu. Hatupaswi kamwe kusahau kwamba kila vita ni mauaji ya kindugu.

Mtakatifu Francis anaendelea kuzungumza nasi

Hapa tunajifunza njia ya huruma na furaha: Mtakatifu Francis anaendelea kuzungumza, si kwa sababu anatoa suluhisho za kiufundi, bali kwa sababu maisha yake yanaelekeza kwenye chanzo halisi cha amani. Kwa sisi sote, tunaomba msaada katika kujenga meza ya mazungumzo ambayo inashawishi, salama, na inahakikisha usanifu wa amani pamoja na haki na wajibu.”

Balozi wa Ukraine  alitoa salamu

Balozi Andrii Yurash alishiriki katika misa hiyo, na katika hotuba ya mwisho wa mkutano wote walisalimiana. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa Askofu Grigori Komar wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine, na Mabalozi wa Kiti Kitakatifu cha Ghana, Guatemala, Honduras, Italia, Slovenia, na Uruguay, pamoja na wawakilishi wa Paraguay, Haiti, na Ubelgiji. "Wakati wa sala hii," Balozi wa Ukraine alisema, "tunaelewa kwa undani ukubwa wa wakati tunaoishi. Kuwa na fursa ya kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya mioyo yetu, ikiambatana na msaada wa kiroho wa Mtakatifu Francis, ni zawadi ya thamani isiyopimika. Katika mahali hapa, tunapokea ushuhuda wake usioyumba wa maelewano na upendo wa kimungu kwa wanadamu wote. Mikutano hii inatufundisha kwamba amani ya haki na ya kweli si lengo lisilowezekana. Kwa baraka ya Mtakatifu Francis, ishara ya milele ya upendo kati ya watu, nia zetu zinaweza kuwa ukweli. “Leo tunashiriki matamanio mazuri lakini rahisi: kuomba na kuota amani pia kunatuita kufanya kazi kwa bidii ili kuifanikisha." Mwishoni mwa sherehe, ujumbe wa Kiukraine uliwapatia  Kardinali Zuppi na Ndugu  Marco Moroni(OFMConv michoro miwili ya msanii Petrice Svitlana Dudenko.

Kulikuwepo pia mapadre wa Ukraine
Kulikuwepo pia mapadre wa Ukraine   (ANSA)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here

12 Machi 2026, 15:55