Tafuta

“Mitandao ya Kijamii na Uendelezaji wa Ufundi:Ushuhuda na Jamii katika Ulimwengu wa Kidijitali." “Mitandao ya Kijamii na Uendelezaji wa Ufundi:Ushuhuda na Jamii katika Ulimwengu wa Kidijitali."  (REUTERS/Hollie Adams)

UISG na USG:Webinar yaakisi mitandao ya kijamii kama nafasi ya utume wa wito

Kukabiliana na mazingira ya kidijitali,Mkutano kwa njia ya Mtandoa wa hivi karibuni wa Kimataifa ulichunguza jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuwa nafasi halisi ya ushuhuda,ushirikishi na kufanya maamuzi ya kijamii.

Na Padre  Mark Robin Destura, RCJ.

Kuwepo mtandaoni leo hii si jambo la hiari tena; ni mahali pa kukutana. Kuwepo kwenye mitandao ya kijamii kunamaanisha kuishi katika nafasi ambapo vijana hutafuta, kuuliza maswali, na kutumaini. Ni hapo ndipo wanapojenga mahusiano, kuelezea mashaka yao, na kugundua upeo mpya. Ni katika uwepo huu ambapo Mkutano kwa njia ya mitandao(webinar) wa Kimataifa ulioongozwa kwa mada ya “Mitandao ya Kijamii na Uendelezaji wa Ufundi: Ushahidi na Jamii katika Ulimwengu wa Kidijitali" uliandaliwa na Vyombo vya habari Kimataifa wa Ushirikiano na Umoja wa Kimataifa wa Wakuu Mashirika ya Kitawa ya Kike (UISG) na Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa ya Kiume (USG). Mkutano huo ulifanyika hivi karibuni tarehe 27 Februari 2026 kwa kuwaleta pamoja washiriki 548 kutoka sehemu tofauti za dunia.  Mkutano huo ulifanyika hasa kwa ajili ya waalimu na wawasilianaji wanaohusika katika uendelezaji wa miito. Msimamizi wa semina ya mtandaoni alikuwa Sr. Thérèse Raad, SDC, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa UISG.

“Mtandao kwa mtandaoni ni halisi”

Mchango kwenye Mitandao ya Kijamii ulitolewa na Raffaele Buscemi, Mtaalamu mwandishi wa habari Mhusika wa  Mawasiliano katika Shirika la  Opus Dei tangu 2017, na mjumbe wa kitivo katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu. Kwa Buscemi katika hotuba yake, alianza na misingi mitatu muhimu kuwa: “Mtandao wa mtandaoni ni halisi. Uzuri ni halisi. Kinachofanya kitu kuwa halisi si chombo, bali mtu na nia iliyo nyuma yake.” Akipinga wazo kwamba mikutano ya kidijitali si halisi kama ile ya ana kwa ana, alisisitiza kwamba “uhalisia hauthibitishwi na chombo cha mawasiliano bali uhalisia wa mtu.”

Alizitaka Jumuiya za  kidini kufafanua nia zao kabla ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii: “Kabla ya kufungua akaunti kwenye Instagram, TikTok, Facebook, au kwingineko, lazima tujiulize: Ninataka kufanya nini mtandaoni? ninataka kufikia nini? Nataka kumfikia nani?” Na katika hili alionya dhidi ya malengo ya jumla kama vile "kumfikia kila mtu" au "kuinjilisha tu," huku akisisitiza hitaji la kufafanua hadhira na lengo halisi. Buscemi pia alisisitiza mwingiliano kama muhimu kwa mitandao ya kijamii: "Mitandao ya kijamii si televisheni." Ikiwa mtu atachapisha maudhui bila kujibu au kushirikisha, alisema, ana hatari ya "kuwepo televisheni kwenye mtandao," ni kukosa uwezo wa mazungumzo wa majukwaa ya kidijitali. Kuhusu miito, aliweka tofauti wazi: "Siamini kuna miito 'iliyozaliwa kidijitali'. Wito hutoka kwa Mungu. Mitandao ya kijamii inaweza kuwa mawasiliano ya kwanza, tangazo la kwanza. Lakini wito huo hukomaa katika jumuiya."

Mitandao ya kijamii kama mahali pa utume

Sr. Amélie Jarrousse, mtawa wa Shirika la  Moyo Mtakatifu wa Yesu, alisimulia vile kitengo cha mawasiliano katika Shirika lake hufanya kazi (Ubelgiji-Ufaransa-Uholanzi). Walikuwa na muda wa tafakari wa muda mrefu kabla hawajajitosa kwenye mitandao ya kijamii, alisema: "Tangu mwanzo tulijiuliza: Tunataka nini, na ni nini tusingependa kuishi nini kwenye mitandao hii?" Alieleza kwamba hawakutaka "kuanguka katika upotoshaji," wala kutoa taswira iliyo bora au bandia ya shirika lao. Kwao, mitandao ya kijamii si kujitangaza: "Tulisisitiza jambo moja: kuwa kwenye mitandao ya kijamii si kuhusu kujiuza; ni mahali pa utume." Alibainisha kuwa vijana tayari wanaishi maisha yao ya utambuzi mtandaoni, na Jumuiya  za kidini zinaitwa kuwasindikiza huko kwa uhalisia.

"Uwazi" katika bara la kidijitali

Fray David Jesús Velásquez Cardona, Mshauri wa Shirika la Wafranciskoano la Ndugu Wadogo  OFM, na Mhamasishaji wa miito  Kitaifa, nchini Colombia, alielezea mitandao ya kijamii kama fursa ya kupanua udugu wa Wafransiskani katika nyanja ya kidijitali. Alieleza kuwa: "Tunataka uwepo wetu mtandaoni utambulike kama uwepo wa udugu."Alielezea majukwaa ya kidijitali kama "aina ya 'kaburi la wazi', nafasi ambapo furaha ya Injili inaweza kuwafikia watu wanaotafuta maana, faraja, na udugu." Na zaidi alisema kwamba mawasiliano yao yamejikita katika maisha ya kila siku: "Hatuko mtandaoni ili 'tuonekane,' bali tuhudumie." Kupitia Instagram, Facebook, YouTube, na WhatsApp, wanakuza mawasiliano ya awali ambayo baadaye yanaweza kusababisha safari za kibinafsi na za kitaaluma.

Utambuzi wa jamii na busara ya kidijitali

Sr. Marta Arici na Sr. Anita Sberna wa Shirika la Wafanyakazi wa Nyumba Takatifu ya Nazareth(Suore Operaie della Santa Casa di Nazareth) walishirikisha  mbinu yao ya Shirika. Walielezea hamu yao: "kuwa karibu na watu, na kujishirikisha kile wanachoishi, na kushiriki kile kilicho hai ndani yetu na hatimaye kushiriki Injili." Walichagua kufanya kazi kupitia kurasa za kijamii badala ya kuzingatia mawasiliano kwa mtu mmoja: "Hatutaki kuwa 'TV kwenye mtandao,' wala kujenga historia inayozunguka mtu mmoja." Maudhui yote yanatambuliwa pamoja kabla ya kuchapishwa ili kudumisha mshikamano na kuepuka hatari zisizo za lazima. Pia walitambua mipaka na hatari za mitandao ya kijamii: matumizi ya muda, kufichua kupita kiasi, na kishawishi cha kutafuta kuridhika kupitia vipendwa na kuonekana.

Ushahidi halisi katika ulimwengu wa kidijitali

Katika kipindi chote cha Mkutano huo kwa njia ya mtandao(Wbinar),mtindo wa kawaida uliibuka kwamba: “mitandao ya kijamii lazima iwe nafasi ya uhalisia, uaminifu, na jamii. Kama Buscemi alivyoithibitisha: "Kuwapo mtandaoni ni kuwa mkweli. Kuwa mwaminifu. Kuwa na mazungumzo. Kuwa na nia." Katika wakati wa miito inayopungua, Kanisa linapewa changamoto,  sio tu kuchukua nafasi za kidijitali, bali kuziishi kama sehemu za utume ambapo Injili inaweza kupatikana, maswali yakikaribishwa, na utambuzi ukiambatana kwa upole.

 

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

04 Machi 2026, 11:53