Tafuta

Sr Lourdes akitembelea mwanamke mwenye ugonjwa wa saratani. Sr Lourdes akitembelea mwanamke mwenye ugonjwa wa saratani.  #SistersProject

Ufilipino: Masista Wamisionari watoa chakula, faraja na upendo

Masista Wamisionari wa Sakramenti Takatifu,wameshirikisha furaha ya Ekaristi Takatifu kwa familia maskini zilizo pembezoni mwa Baseco,huko eneo la bandari ya Manila, wakipanda matumaini katika maisha yao kwani wengi wao wanaoishi kwenye umaskini uliokithiri.

Na Sr. María del Pino Rodríguez de Rivera Olives, MSS.

Maisha ya masista wa Ekaristi Takatifu pamoja na walei wanaoishi karama hii na kazi za kimisionari imejikita katika ekaristi takatifu, ibada kwa Bikira Maria na Utume. Ekaristi Takatifu ni moyo na kiini cha yote wanayofanya na kupitia, hiyo inayojidhihirisha kwa njia ya kuabudu, na katika maisha yao kwa njia ya ukarimu na furaha katika kujitoa. Masista hufanya utume wa kila siku huko Baseco, huku wakijitahidi kuinua maisha ya watu wanaoishi katika hali duni na zisizo salama. Utapiamlo kwa watoto wadogo, afya duni, ukosefu wa elimu na makazi yasiyotosha, wakati mwingine yasiyo ya kibinadamu na  ni sehemu ya uhalisia mgumu ambao watu wanalazimika kuishi ndani yake.

Mpango wa “Jiko la Supu” na Malezi

Moja ya utume wa masista hawa katika eneo hilo ni  “mpango wa kuwalisha watu,” wakilenga kuwalisha na kuwaelimisha watoto kuanzia umri wa miaka mitatu hadi kumi. Mpango huu hufundisha watoto sala na namna ya kumwabudu Yesu wa Ekaristi.  Masista ni mashuhuda wa jinsi ambavyo Yesu wa Ekaristi amekuwa injini na chachu ya maisha ya watoto pamoja na familia zao. Historia nyingi ziosizosimuliwa hubaki moyoni mwa Yesu, ambako yeye huwatia nguvu na kuwahimiza kwa uwepo wake.

Sr. Lourdes teaches children to write

Sr. Lourdes akifundisha watoto kuandika

Ekaristi inayofanywa hai katika mambo yaliyo rahisi

Moja ya nyakati muhimu tunazopitia katika utume wetu ni adhimisho la Ekaristi Takatifu kila Dominika,” alisema Sr. Liliam María Taborda Viana. Furaha ilioje, aliongeza, “ukiwaona watoto wakivaa nguo zao zilizo bora zaidi kwa ajili ya adhimisho la Misa Tanakatifu, huku wakipiga kelele wakati wa maandalizi kabla ya Misa, Tara, magmisa tayo (“tunajiandaa kwa Misa,” kwa lugha yao ya Tagalog).” Furaha ya Bwana inajaza mioyo yao hata katikati ya umaskini. Wakati wa kutoa sadaka, kila familia inajiunga kwa maandamano ya kutoa vipaji matunda ya kazi zao (siku mbili za usiku za kumenya vitunguu saumu na kubeba kreti katika soko la mtaani). “ Nakiri kuwa kila mara wananifanya nalia. Wanaishi katika umaskini lakini wanamtolea Mungu kidogo walichonacho kama mama mjane katika injili,” alisema Sr. Liliam.

Rubi, Sr. Luz and Lucy prepare a meal for the "Feeding Program"

Rubi, Sr. Luz na Lucy wakiandaa chakula “Mpango wa Kuwalisha watu”

Kuongoza na Kusikiliza

Masista Wamisionari hushiriki maisha ya jumuiya ya kila siku kwa kutembelea familia, kuwasikiliza na kuwapa upendo. Huwasaidia wale waliopoteza mali zao zote kutokana na dhoruba ya kimbunga, ambavyo ni vya mara kwa mara nchini humo. Kitendo kidogo kama kuwagusa, tabasamu na kuwashika mkono ni mwanga unaoleta matumaini katikati ya changamoto na mateso. “Maskini ni marafiki zangu,” alipenda kusema mwanzilishi wa Shirika la Masista Wamisionari wa Ekaristi Takatifu, Mtumishi wa Mungu Maria Emilia Riquelme. Lucy, mmoja wa watu wa kujitolea katika Kikanisa kidogo cha Kuabudia Ekaristi Takatifu, kilichoanzishwa na masista Wamissionari, waliofika Baseco miaka 15 iliyopita. Mwanzoni, alishiriki utume huu kwa kutazama tu. Alitumia muda mwingi kukaa nyumbani kwake. Akiwa anafikiria kwa kina na kusongwa na huzuni, akimenya vitunguu kuanzia saa 3.00 asubuhi  hadi  saa 10.00 jioni, ili aweze kuuza, na kutumia kipato kidogo kwa kulisha familia.

Wakati fulani, aling’amua kuwa upendo wa Mungu ni mkuu kuliko mateso na changamoto anazopitia, na sasa ni mwanautume mmisionari mmoja wa familia ya Missami (huu ni ushirika wa masista na walei wanaoshirikishana  maisha na karama moja ). Anafanya utume kwa kushirikiana na akina mama wengine katika jamii.” “Tunajisikia kuwa tumetumwa na Yesu wa Ekaristi,” alisema mwanamke huyo. Wanasaidia kupika kwa ajili ya kuwalisha wahitaji, na kufundisha watoto, kuongoza adhimisho la Dominika na kuwaandaa watoto kabla ya kupokea sakramenti.

Sr. Liliam with one of the children from the community of Baseco

Sr. Liliam akiwa na mtoto mmojawapo kutoka kwenye jumuiya ya Baseco

Kumtumaini Mungu Mpaji

Masista waliopo kwenye utume huu hugusa mahitaji ya walio wengi: kujisikia wanadhaminiwa kama binadamau, kuheshimiwa na kuwa washiriki wa imani, mila na tamaduni, ambazo mara nyingi hazidhaminiwi kwa sababu ya ubaguzi. Kwa ushuhuda wao, masista hujitoa maisha yao, kuwahudumia wahitaji, wakitumkumbusha maneno ya Papa Leo XIV kwenye Waraka wake wa Kitume wa  Dilexit te yaani "Nimekupenda," unabainisha kuwa “ tukutana na wale walio katika maisha ya chini na wasio na nguvu, hii  ni njia muhimu ya kukutana na Mungu katika historia. Kupitia maskini, Mungu anaendelea kuzungumza na sisi.”

MASISTA UFILIPPINO

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

04 Machi 2026, 10:17