Padre Patton:Sala na kufunga ni silaha pekee ambazo Wakristo wanapaswa kutumia!
Francesca Sabatinelli na Sr. Christine Masivo, CPS - Vatican.
Padre Francesco Patton(OFM), aliyekuwa Msimamizi wa Nchi Takatifu alilalamika kuwa:"Tumeshikwa na aina ya wazimu wa vita, wazo kwamba kila kitu kinaweza kutatuliwa kwa nguvu na silaha. Wazo la waathiriwa wa raia ni la kila wakati na lipo kwa undani." Akizungumza kutoka Mlima Nebo huko Yordan, macho yake yaligeuka ng'ambo ya Bahari ya Chumvi inayotenganisha Ufalme wa Hashemite na Israeli na Palestina, mawazo yake yakiwa yameelekezwa Mashariki ya Kati ikiwaka moto.
"Kila siku ninawafikiria watawa wenzangu wanaoishi Lebanon, Beirut na kwingineko, Kusini na Kaskazini, ambao wanajaribiwa kupita kiasi," Padre Patton alielezea. "Chumba cha watawa huko Tyre kimegeuzwa kuwa kambi ya wakimbizi, na wale walio Beirut wanajaribu sana kuwasaidia raia, ambao hawawezi kuendelea, sasa kuna watu milioni moja waliohamishwa kati ya jumla ya watu milioni sita."
Ni nini kinachofuata baada ya vita?
Msimamizi wa zamani wa Nchi Takatifu alikumbuka kwamba tangu mwanzo wa vita huko Gaza ilikuwa wazi hasa kwa watu kama yeye wenye uzoefu wa miaka mingi katika eneo hilo, kwamba isipokuwa mzozo huo umalizike “kwa njia isiyo ya vurugu, ungeenea.”Lakini alionya kwamba, ni hatari ni kwamba, hakuna anayejua kitakachotokea mwishoni mwa vita. Kufuatia "vita vyote vya hivi karibuni vya Mashariki ya Kati, aina mpya za ugaidi zimeibuka na vikundi vipya vimeibuka, kama vile Al-Qaeda, ISIS, Hezbollah, na Hamas, kila kimoja kikiwa kimezaliwa kutokana na migogoro ambayo haikutatuliwa kisiasa, yote ni matokeo ya majaribio ya suluhisho za kijeshi kwa migogoro ambayo yangepaswa kushughulikiwa tofauti."
Mkasa wa Palestina
Padre Patton aligeukia Gaza, akirudia matamshi yaliyotolewa siku chache zilizopita na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, kwamba lisisitiza Ukanda umeharibiwa, kwamba watu wanaishi karibu na mfereji wa maji taka ulio wazi, na zaidi wanakabiliwa na njaa kali, "matatizo ya dawa, usalama, ya maisha yanayoishi kwa kuheshimu haki za msingi na utu wa binadamu. Zaidi ya hayo, kuna kinachoitwa Bodi ya Amani, ambayo haijaanza hata kufanya kazi na inaonekana kama mzimu kuliko ukweli wa uendeshaji."
Wakati huo huo, katika Ukingo wa Magharibi, upanuzi wa makazi ya Israeli unaendelea, huku makumi ya maelfu ya watu wakikimbia makazi yao. "Uvamizi unaendelea, na hivyo ndivyo vitendo vya vurugu," Padre Patton aliongeza, akikumbuka kwamba "familia iliyoua siku chache zilizopita katika eneo la Nablus, na nimtoto mmoja wa miakaa tisa aliyenusurika.” Pia kuna "mipango ya kisheria inayoendelea ambayo inazuia Ukingo wa Magharibi kutokana na zilizopo na Wapalestina kuwa na ardhi yao wenyewe na ulinzi wa haki za msingi, kama vile kusajili maeneo ya Palestina katika sajili ya ardhi ya Israeli au kukataa kuruhusu walimu wenye shahada kutoka vyuo vikuu vya Palestina kufundisha katika shule za Israeli."
Haya yote ni "aina za shinikizo la moja kwa moja au lisilo la moja kwa moja linalolenga kuwafukuza Wapalestina kutoka nchi ambayo wameishi kwa milenia." Mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaosababishwa na vita pia unasikika sana huko Jordan kutokana na watu kutotemebelea mji huo kwa hija. Mwishoni mwa Februari, tulikuwa tukiona ahueni fulani katika idadi ya wageni na mahujaji, na ghafla tumerudi karibu sifuri," Custos wa zamani alisisitiza. Hii inaathiri hasa sio tu Wakristu wanaofanya kazi katika maeneo matakatifu na sasa wameachwa bila kazi au njia za kusaidia familia zao.
Silaha pekee kwa Wakristo ni sala
Ili vurugu hizi zikome, Padre Patton anaamini Jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua kwa uamuzi zaidi na kwamba lazima kuwe na "mabadiliko katika sera ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati." Kwa mtazamo wa Kanisa, alisema, pia kuna matumaini ya "kwa kusali pamoja, kunaoelekezwa kwa Wakristo na waamini wa dini zote, kama Papa Yohane Paulo II alivyofanya wakati wa vita vya Iraq na kama Papa Franciscko alivyofanya mwaka 2013, kukusanyika pamoja kwa wote kwa ajili ya kufunga na kuombea amani." "Ni zana ambayo inaweza kuonekana kama ya kipuuzi ikilinganishwa na silaha, lakini ni njia ya kuongeza uelewa ambayo inaweza kuwaunganisha waamini wa dini tofauti," sambamba na kile ambacho Papa Leo XIV anakielezea kama "amani isiyo na silaha na kupokonya silaha ya unyenyekevu na inayodumu." Kwa waamini, Padre Patton alihitimisha na kusema kwamba, "Sala na kufunga ndio 'silaha' pekee tunazoruhusiwa kuchukua."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.