Tafuta

2026.03.23 Watawa wa Karmeli huko Phnom PenhCambodia. 2026.03.23 Watawa wa Karmeli huko Phnom PenhCambodia.  (Catholic Church in Cambodia)

Monasteri ya Karmeli ya Wakorea yafungwa nchini Cambodia baada ya miaka 21 kwa kukosa miito

Baada ya zaidi ya miongo miwili ya uwepo wa watawa wa ndani katika monasteri ya Wakarmeli iliyoanzishwa na masista wa Korea huko Phnom Penh ilifungwa rasmi mnamo Machi 19,huku viongozi wa Kanisa wakitaja kutokuwepo kwa miito mipya miongoni mwa wanawake vijana wa Cambodia.

Na Chainarong Montienvichienchai- LiCAS News.

Monasteri ya Wakarmeli ya Watawa wa ndani  huko Phnom Penh, iliyoanzishwa mwak 2004 na masista kutoka Monasteri ya Wakarmeli wa Seoul, ikiwa na sifa ya kuwa jumuiya ya kwanza ya Watawa wa ndani  kutoka Korea Kusini kufanya kazi ya umisionari nchini Cambodia, imefungwa. Baada ya miaka mingi ya huduma, masista waliobaki sasa wanarudi katika nchi yao. Tukio la kufunga iliadhimishwa na Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Olivier Schmitthaeusler, Askofu Mkuu wa Phnom Penh, akisaidiana na Askofu Pierre Hangly Suon, Mratibu wa Askofu Mkuu wa Phnom Penh, na mapadre wengi.

Waamini karibu 100 walishiriki kutoa shukrani za ushuhuda wao

Karibu waamini 100 wa jumuiya ya Wakatoliki wa eneo hilo walikusanyika kutoa shukrani kwa ushuhuda wa kimya kimya, lakini wa kina wa watawa hao kwa miaka mingi. Katika mahubiri yake, Askofu Schmitthaeusler alionesha masikitiko makubwa kuhusu kufungwa kwa Kanisa hilo, akitambua utajiri wa kiroho ambao uwepo wa Wakarmeli ulioletwa katika Kanisa la eneo hilo. Wakati huo huo, aliwahimiza waamini kubaki na matumaini na umoja katika sala, akisisitiza thamani ya kudumu ya maisha watafakuri wa Ndani  hata wakati hawapo kimwili. Masista Wakarmeli, wa Shirika la Watawa wa Wakarmeli wa Ndani (OCD), walifika Cambodia kwa mara ya kwanza mwaka  2004. Hapo awali waliishi katika nyumba huko Phnom Penh kabla ya kuhamia mwaka 2010 katika nyumba ya Watawa iliyojengwa kwa madhumuni maalum katika Wilaya ya Ang Snuol, Mkoa wa Kandal, nje kidogo ya mji mkuu. Katika kilele chake, jumuiya hiyo ilikuwa na watawa saba wa Kikorea, ambao wengi wao walijifunza Kikhmer na Kiingereza kidogo ili kuungana vyema na Kanisa la eneo hilo. Wakiwa waaminifu kwa karama yao, watawa hao waliishi maisha ya kujificha yaliyojitolea kwa sala, ukimya, toba, na kazi za mikono.

Monasteri ilioonekan kuwa mahali pa amani

Monasteri yao ilionekana sana kama mahali pa amani na kimbilio la kiroho katikati ya maendeleo ya haraka na mabadiliko ya kijamii yanayotokea Cambodia. Wageni mara nyingi walielezea hisia kubwa ya utulivu walipoingia kwenye uwanja huo, ambapo mdundo wa sala uliunda maisha ya kila siku na wasiwasi wa kidunia ulionekana kutoweka zaidi ya kuta za monasteri. Licha ya ushiriki wao mdogo wa nje, uwepo wa watawa hao ulikuwa na utume wa ulimwengu wote. Kwa kuzingatia utamaduni wa Wakarmeli, "kazi" yao kuu ilikuwa maombi, kwa ajili ya Kanisa, kwa ajili ya jamii, na kwa ajili ya ulimwengu uliojaa mateso na mgawanyiko. Sadaka zao zilizofichwa zilitolewa kama aina ya mshikamano wa kiroho na ubinadamu.

Kufungwa kwa Monasteri ya Cambodia ya wakarmeli kwa ukosefu wa miito
Kufungwa kwa Monasteri ya Cambodia ya wakarmeli kwa ukosefu wa miito   (Catholic Church in Cambodia)

Kufungwa kwa Monasteri kuaakisi wasiwasi mpana wa kikanda

Kufungwa huko kwa Monasteri pia kunaakisi wasiwasi mpana wa kikanda. Katika nchi jirani ya Thailand, viongozi wa Kanisa wanashuhudia mitindo kama hiyo. "Hali kama hiyo nchini Thailand," alisema Niphon Saengpradab, rais wa zamani wa Baraza la Serra nchini Thailand, ambalo ni shirika lililojitolea kukuza miito ya upadre  na utawa. "Uhaba wa miito unahusishwa na ulegevu, kupungua kwa imani ya kifamilia, na katekesi duni," alisema akizungumza na Shirika la Habari Katoliki Asia (LiCAS News.) Bwana Niphon, ambaye aliongoza semina kwa wanachama wa Serra katika eneo la mashariki mwa nchi mnamo Machi 20-21, alisisitiza kwamba kushughulikia kupungua huko kunahitaji mbinu ya kuchukua hatua zaidi. "Lazima kuwe na juhudi mpya na za makusudi za kukuza utamaduni wa miito ndani ya Kanisa," alisema. "Lazima tubadilike kutoka msimamo wa kutojali hadi uhamasishaji hai, unaoambatana na sala."

Nguvuza sala na ushuhuda wao utaendelea hata baada ya kuondoka kwao

Akitafakari asili ya uutume huo , Mama mkuu wa monasteri, Sr. Mary, OCD, aliwahi kuelezea msingi wa Cambodia kama hatua ya kihistoria kwa Kanisa la Korea. Monasteri hii iliyoanzishwa mwaka 1940 ikiwa na mizizi inayohusiana na Ufaransa, jumuiya ya Seoul Wakarmelo ilikuwa imekua kwa kasi kwa miongo kadhaa, hatimaye ikianzisha monasteri nyingi Korea Kusini yote. Utume sasa wa Cambodia  ulikuwa hatua ya kihistoria, na utume wao wa kwanza wa Kikarmeli kutoka nje ya Korea.  Ingawa kufungwa kwa monasteri hiyo kunaashiria mwisho wa uwepo wake huko Cambodia, wengi katika Kanisa la eneo hilo wanawakumbuka watawa wa Wakarmeli kama ushuhuda wenye utulivu ambao uwepo wao na nguvu za sala zao zitazidi kuendelea hata baada ya kuondoka kwao.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

24 Machi 2026, 17:34