Tafuta

Sr Inês Paulo Albino,Katibu Mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu. Sr Inês Paulo Albino,Katibu Mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu. 

Italia:Wito wa kufikiria upya ulimwengu kupitia macho ya watoto

Katika maisha uwepo wa watoto unapaswa kuhamasisha kujitolea upya kwa kimataifa kwa utu wao, ndoto zao, na ustawi wao. Sr. Inês Paulo Albino alihimiza jamii kuwekeza kwa watoto huku wakiunda kikamilifu mustakabali wenye matumaini wa pamoja na kuwasaidia kukua vema.

Na. Sr. Christine Masivo, CPS - Vatican

Sr. Inês Paulos Albino, akizungumza katika mkutano huko Trani, Italia wenye mada: "Haki za watoto ziko karibu na moyo wangu," alisisitiza kwamba watoto lazima wawe kitovu cha vipaumbele vya kijamii. Kulingana na Shirika la Kipapa la habari za Kimisionari Fides, Sr. Inês Paulos, Katibu Mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu (POSI), ambalo watakatifu wake Wasimamizi ni pamoja na Mtakatifu Yosefu, mume wa Bikira Maria, alisisitiza hitaji la mabadiliko katika mtazamo unaomtambua kila mtoto kama mwenye matumaini na ndoto.

Kufikiria kuwapyaisha watoto katika ulimwengu wa uovu

Sr. Inês alibainisha kuwa kila mtoto anawakilisha mustakabali wa kipekee unaostahili kulelewa na kusisitiza kwamba ubinadamu halisi unaonyeshwa katika juhudi za kusaidia ndoto zao kutimia. Ujumbe wake uliguswa sana wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu ya kituo cha kijamii cha "Serafina Cinque" kinachoendeshwa na Masisita Waabuduo wa Damu Azizi. Kutokana na maisha Sr. Inês ya kimisionari amekabiliana na hali halisi tofauti ambazo watoto wanakabiliana nazo kutoka Afrika, Asia, na Amerika na hata huko Ulaya na Amerika Kaskazini, ameshuhudia watoto wakitunzwa vyema na pia kupuuzwa.

Katika nchi na maeneo mengi yanayoendelea, watoto wanapambana katika umaskini, ukosefu wa elimu, na njaa. Wakati huo huo, katika jamii zenye uwezo, aliona mgogoro wa kutengwa kihisia, ukosefu wa mwongozo, na kutoridhika kunakoongezeka miongoni mwa watoto ambao, licha ya wingi wa mali, mara nyingi huhisi upweke. Alielezea kunyimwa haki za watoto kama "janga baya" kwa binadamu, na kupuuzwa, iwe wa kimwili au kihisia, kudhoofisha jamii ya baadaye duniani kote, ambayo ipo kwa sasa kwa watoto.

Kulinda na kuwawezesha watoto katika maisha kama utume

Tukio hilo liliakisi kazi ya Shirika la Waabuduo wa Damu ya Kristo wanaosimamia Kituo cha Jiji la Daamu Azizi ya Kristo. Misheni yao inalenga kulinda maisha, hasa watoto ambao hawajazaliwa, huku ikisaidia familia zinazokabiliwa na hali ngumu, ikiwa ni pamoja na utasa na mimba zisizopangwa. Uangalifu maalum unatolewa kwa wanawake walio katika mazingira magumu na wasiojiweza. Sr. Inês Albino alielezea dhamira ya POSI, ambayo inasaidia takriban miradi 3,000 kila mwaka, huku mpango wake ukilenga kuwapa watoto duniani kote fursa za ukuaji kamili, malezi ya imani, na elimu ya umisionari.

Kupitia juhudi hizi, shirika halitafuti tu kukidhi mahitaji ya haraka ya watoto bali pia kuweka matumaini na kusudi la siku zijazo. Kwa kutoa mfano wa Mtakatifu Joseph, ambaye sherehe  yake huadhimishwa kila ifikapo tarehe 19 Machi ya kila mwaka  Sr. Inês Albino alihimiza jumuiya kukumbatia utunzaji na uwajibikaji na kuwalinda watoto. Ujumbe wake bado unaendelea kusimamia na  kama ukumbusho wenye nguvu kwamba kujenga ulimwengu bora kwa kuanzia kuwasikiliza, kuwaunga mkono, na kutembea pamoja na wadogo kati yetu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

24 Machi 2026, 16:08