Tafuta

2025.09.24 Suore Missionarie del Preziosissimo Sangue

Ghana:Mwili mmoja wa Kristo pamoja na Viziwi

Ofisi ya viziwi na Huduma ya Viziwi ya Mtakatifu Martin ilianzishwa huko Accra nchini Ghana kwa ajili ya ujumuishaji na ushirika kama mwili mmoja wa Kristo ili kuepuka kutengana kwa ajili ya utume wenye maana kwa Kanisa.

Na Sr. Christine Masivo, CPS - Vatican.

Utume wenye maana wa ujumuishaji huko Madina, jiji Accra nchini Ghana, kwa ajili ya viziwi na Wakatoliki wenye matatizo ya kusikia  ambapo ni mpango rahisi wa kichungaji unaoendelea kukua. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, linabainishwa kwamba  Mpango huo kwa kuongozwa na Padre René Yao wa Jumuiya ya Shirika la Wamisionari wa Afrika, (SMA) “huduma ya viziwi ya Mtakatifu Martin inasaidia kuhakikisha kwamba Injili inawafikia kila mtu, hasa wale ambao hawapewi kipaumbele katika jamii.” Alizindua rasmi huduma ya kichungaji ya viziwi huko Masina,  Accra mnamo Novemba 2020 na imekuwa huduma yenye nguvu inayohudumia kundi linalokua la viziwi na waamini wenye matatizo ya kusikia.

"Mwanzoni sikuwa na ofisi,nilikaa chini ya mti karibu na Kanisa" 

"Mwanzoni,  alisema - sikuwa na ofisi. Nilikaa chini ya mti karibu na Kanisa. Baadaye, waamini wa Kanisa waliniambia kwamba nisingeweza kufanya kazi chini ya mti na wakanisaidia kujenga  Ofiisi ndogo," alisema Padre René. Kulingana na Shirika la Kipapa la Habari la Kimisionari Fides, Padre Yao alielezea kwamba michango midogo na ukarimu wa waamini wa Kanisa hilo humsaidia kuendeleza shughuli za Huduma ya Viziwi wa Mtakatifu Martin aliyoianzisha. Ujumuishaji  ndiyo kiini cha juhudi za kichungaji, ambazo huchanganya usindikizaji wa kiroho na ushiriki wa kijamii na mpango wa kielimu.

Viziwi na vipofu wapate kuona
Viziwi na vipofu wapate kuona

Jumuiya ya Parokia jumuishi kwa kutumia Lugha ya Ishara

Huduma ya Padre Yao, inawaunganisha waamini viziwi wa Kanisa, kikamilifu katika maisha ya Kanisa katika shughuli zote. Kozi za lugha ya ishara pia hutolewa kwa waamini wa Parokia ili kukuza mawasiliano na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa huduma. Jitihada hizi husaidia kuunda mazingira ambapo waamini wa Kanisa viziwi na wanaosikia wanaweza kuingiliana kwa uhuru wakijenga jamii iliyojengwa katika uelewano na heshima ya pande zote.

Maono ya kichungaji yanasisitiza umoja badala ya utengano

"Sitaki kutenganisha umati kwa viziwi," alielezea. "Tayari wametengwa vya kutosha. Tukiadhimisha misa kwa ajili yao tu, tunawatenganisha zaidi na jumuiya ya wasikilizaji. Lazima tuombe pamoja kama mwili mmoja wa Kristo." Kupitia ahadi hii, huduma ya Viziwi ya Mtakatifu  Martin inaendelea kushuhudia Kanisa ambapo kila mtu bila kujali uwezo wake ana nafasi mezani pa Bwana.”

Kila mmoja ajumuishwe
Kila mmoja ajumuishwe

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Machi 2026, 16:50