COMECE na UISG:Maombi kwa ajili ya kunyamazisha milio ya risasi
Vatican News
Wasiwasi mkubwa kuhusu "kudhoofika zaidi kwa utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria" na kuendelea "kutojali sheria za kimataifa" kulioneshwa na Rais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya,(COMECE)Askofu Mariano Crociata. Katika taarifa, alielezea mawazo yake kwa wale wanaopitia "kuongezeka kwa vurugu hivi karibuni nchini Iran na kote Mashariki ya Kati." Askofu Crociata pia alielezea kama "ana wasiwasi sana" kuhusu ukweli kwamba vurugu zinapewa kipaumbele kuliko diplomasia na kwamba "mantiki ya kulipiza kisasi" inaweza kuchochea "mzunguko wa vurugu, kuhatarisha utulivu wa kikanda na kimataifa, na uwezekano wa kusababisha janga kubwa."
Wito kwa Umoja wa Ulaya
Rais wa COMECE, akizungumzia wito wa Papa Leo XIV wa kukomesha "mzunguko wa vurugu," alitoa wito kwa Umoja wa Ulaya "kubaki na umoja" na kutimiza "wito wake kama mpango wa amani," kufanya kazi ili "kupunguza msukosuko miongoni mwa pande zote zinazohusika, kufufua juhudi za kidiplomasia, na kudumisha sheria za kimataifa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na katika eneo la kutoeneza silaha za nyuklia." Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) pia unahimizwa kuhakikisha usalama wa raia wake. Mwaliko ni kuomba "kwamba silaha zitanyamazishwa Mashariki ya Kati yote," na kwamba watu wa Iran na wale wote katika eneo hilo waweze kuanza "njia kuelekea mustakabali wa amani unaoangaziwa na heshima kwa utu wa binadamu na haki za msingi za binadamu."
UISG:Maombi Mbashara, Machi 6
Mwaliko wa kusali pia umetoka kwa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa mashirika ya Kitawa (UISG), ambao, "katika kukabiliana na kuongezeka kwa vurugu na vita" vinavyoathiri sehemu mbalimbali za dunia, unahitaji hatua "kwa amani isiyo na silaha na ya kupokonya siala."
Kwa njia ya kufunga, kutenda matendo mema na wakati wa sala kimataifa, uliopangwa kufanyika Ijumaa, tarehe 6 Machi 2026 , saa 9:30 alasili masaa ya, Roma, maombi hayo yatarushwa mbashara kwa wote. "Kama wanawake waliowekwa wakfu, watawa, waliopo katika mazingira dhaifu zaidi ya jamii na karibu na wale wanaoteseka, hatuwezi kukaa kimya tukiwa na springi ya uharibifu ambayo inadhoofisha utu wa binadamu na kuweka hatarini mustakabali wa vizazi vipya”, alielezea Sista Roxanne Schares, Katibu Mtendaji wa UISG.
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here