Caritas Ulaya,inataka uongozi wa serikali mahalia uwe kiini cha hatua za kibinadamu
Na Linda Bordoni - Vatican.
Ripoti mpya ya Caritas Ulaya inasisitiza umuhimu wa kurudisha usawa kimadaraka ndani ya mfumo wa kibinadamu, ikitoa wito kwa wahusika wa ndani kuhama kutoka kwenye ukingo wa kufanya maamuzi hadi kwenye nafasi za uongozi wa kweli. Ripoti hii iliyozinduliwa Jumatatu tarehe 2 machi 2026, ilikuwa na kichwa cha habari: “Kukuza uongozi mahalia katika hatua za kibinadamu: Kuchochea maendeleo, changamoto na fursa.” Ripoti hii ni mwendelezo wa ile ya mwaka 2023 iliyoonyesha pengo kati ya ahadi za Kimataifa na uhalisia uliopo kwenye jamii kupitia taasisi za kibinadamu.
Akizungumza na Vatican News, Abriel Schieffelers, Ofisa wa Utetezi wa Kibinadamu wa Caritas Ulaya, alibainisha kuwa, pamoja na jitihada za miaka kadhaa kuimarisha uwakilishi wa kijamii, maendeleo bado hayapo bayana.“Bado tunashuhudia utegemezi katika misaada kwenye miradi midogo na ya muda mfupi, inayotegemea pesa za mradi ambapo mashirika ya ndani wanaonekana kama watendaji badala ya viongozi,” alibainisha.“Bado kuna tabia ya kutounda programu pamoja na kutoweka mashirika ya ndani katika nafasi za kufanya maamuzi.”
“Uhalisia wa Maisha” kwa Uongozi wa mtaa
Katika uzinduzi rasmi wa ripoti hii, mapema siku hiyo, rais wa Caritas Ulaya, Monsinyo Michael Landau, alisisitiza kuwa, “uongozi mahalia ni msingi katika utume wa Kanisa.” Kwetu sisi, uongozi mahalia siyo suala la kuangaziwa, ni uhalisia wa maisha ambapo unajikita katika utu wa ndani ambao unapaswa kuwa kiini na kipaumbele, alisema. Pia alikiri kuwa, katikati ya mfumo mpana ya kibinadamu kanuni hii “mara nyingi, haitambuliwi kikamilifu, na wala haipewi rasilimali za kutosha na haiaminiwi kikamilifu.
Kwa mujibu wa Monsinyo Landau alibanisha kuwa Ripoti hii imekuja katika “wakati ulio mgumu kipekee” kwa watendaji wa kibinadamu. Kuna upungufu mkubwa wa dhati ambao ni pamoja na kupungua kwa ufadhili kutoka kwa USAID na kufuatiwa na wafadhili kadhaa wa Ulaya, hii imekuwa na madhara makubwa. "Uchambuzi huu unabainisha kuwa wahusika wa ndani na kitaifa mara nyingi wanabeba mzigo mkubwa zaidi. Wakati ufadhili unapopungua, ubia upo kwenye hatari zinanzoshushwa chini, na mashirika ya ndaniyanatarajiwa kutoa zaidi kwa rasilimali chache na ushawishi mdogo. Hili siyo tu jambo la dhuluma bali pia haliwezi kudumu.”
Kustahimili kupungua kwa ufadhili
Katika mahojiano hayo, Schieffelers alibainisha kuwa mashirika ya ndani “yanabeba mzigo mkubwa wa kupungua kwa ufadhili wa kibinadamu,” uliyoanza takribani mwaka mmoja uliopita. “Hii inaacha mashirika ya ndani katika mazingira hatarishi sana kadiri rasilimali zinavyozidi kupungua,” hapa, akiashiria kuongezeka kwa ushindani mkubwa kwa wahusika wa kitaifa hasa katika uwezo wa kujiendeleza kwa shirika. Ushirikiano wa hatari na mgawanyo sawa wa gharama za juu hubaki kuwa mapungufu muhimu. “Linapokuja suasa la kugawana gharama za ziada, kugawana hatari, hizo ni baadhi ya vipengele muhimu ambavyo bado havipo katika suala la uongozi mahalia,”alibainisha.
Hospitali ya watoto Caritas, huko Bethlehem
Zaidi ya Ufanisi na gharama: Haki na kujitawala
Ingawa unajibishaji mara nyingi hupangwa kulingana na ufanisi wa gharama, Caritas inasisitiza suala hili ni la msingi zaidi. Wakati mwingine uongozi mahalia unatazamwa katika mrengo wa gharama na ufanisi,” Schieffelers, alisisitiza. “ Lakini kile tunachotaka kusisitiza na kukuza kama Caritas ni jambo msingi zaidi. Lengo letu limejikita katika haki na kujitawala, katika uamuzi wa kibinafsi na umiliki wa ndani.” Alisema kuwa, kuhakikisha kwamba wale walioathirika na migogoro wanashirikishwa katika maamuzi ambayo yanaunda maisha yao si tu mageuzi ya kiufundi, bali ni suala la kanuni. Mtiririko wa rasilimali fedha unapaswa kufuata mabadiliko ya uongozi, ingawa hili linaweza kuwa na gharama nafuu, hili siyo lengo mahususi.
Njia mbili za kuwajibika na mabadiliko ya kimuundo
Miongoni wa mabadiliko madhubuti yaliyopendekezwa kwenye ripoti hii ni kuanzishwa kwa njia mbili za mifumo ya uwajibikaji. “Tulitaka kuonesha umuhimu wa washirika kuwa katika uongoza wa tathmini ya uwezo na mijadala kuhusu kufafanua upya jukumu la mashirika ya kimataifa.” Mashirika ya ndani yaliripoti mara kwa mara kuwa mamlaka ya kufanya maamuzi yanasalia kutokuwa sawa, mara nyingi yakielezea ushirikiano kama wa ngazi za juu. “Ili kubadilisha kipengele hicho, nguvu ni jambo la msingi sana na huenda zaidi ya mabidiliko ya ufadhili,” aliongeza. Kwa kuwa na maono ya siku za usoni, Caritas inataka kulinda mafanikio ya hivi karibuni na kutatua vizuizi vya kimfumo vinavyozuia maendeleo. Miradi ya maendeleo pamoja na mifumo yenye ubunifu ipo tayari, kinachotakiwa ni kuongeza wingi wake, hilo litakuwa jambo muhimu sana.
Maombi ya Papa na mwelekeo wa migogoro ya Kisiasa
Akizungumzia matokeo ya maombi ya mara kwa mara ya Papa ya kutosahau migogoro na vita vilivyopuuzwa, Abriel Schieffelers, alisema kuwa jambo hili lina uzito mkubwa. “Tunatambua kuwamara nyingi ni uamuzi wa kisiasa wakati migogoro sio tu imesahaulika lakini kupuuzwa,” alisema. Misaada ya kibinadamu peke yake haitoshi katika majanga ya muda mrefu, ushiriki wa kidiplomasia na juhudi za kujenga amani pia zinahitajika. Katika muktadha huu alikazia umuhimu wa ushiriki wa mashirika ya ndani, hasa viongozi wa dini, katika kuimarisha mshikamano katika ngazi ya jamii. Monsinyo Landau ,alikumbusha na kurejea mtazamo huu wakati wa uzinduzi,akisisitiza kwamba mtazamo wa Caritas umejikita katika mshikamano na ufadhili, kanuni zinazotaka maamuzi kuchukuliwa kwa haraka kwa wale walioathirika.
Mradi wa Maendeleo wa Caritas huko Cape Verde
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here