Tafuta

2026.02.03 Tuzo ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis. 2026.02.03 Tuzo ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis. 

Tuzo ya"Mtakatifu Francis na Mtakatifu Acutis,"kwa ajili ya uchumi unaohudumia udugu

Toleo la sita la tuzo lilonaheshimu mipango yenye tija na wajasiriamali vijana katika pembezoni mwa duni liliwasilishwa tarehe 3 Februari 2026 katika Jumba la Pio,Roma.Kuna uwezekano wa kujiunga na shindano hadi Februari 28 na sherehe ya tuzo imepangwa kufanyika tarehe 16 Mei 2026 katika Madhabahu ya Kuvua nguo huko Assisi.Kardinali You,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri alisema kuwa"Mpango huu ni chanzo cha msukumo kwa utakatifu."

Na Daniele Piccini  na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa upande mmoja, kukuza mipango ya kiuchumi na mipango  iliyopendekezwa na Jumuiya zinazoishi pembezoni mwa dunia; kwa upande mwingine, kutoa mfano wa mfumo wenye tija, unaotegemea ushirikiano, kama mbadala wa ule unaotawala, unaowanyonya watu na rasilimali za Uumbaji. Hayo ndiyo Malengo mawili ya  "Tuzo ya Kimataifa ya Francis wa Assisi na Carlo Acutis kwa Uchumi wa Udugu," iliyofadhiliwa na Chama cha Mfuko wa Madhabahu ya Kuvua ya Jimbo Katoliki la Assisi - Nocera Umbra - Gualdo Tadino. Toleo la sita la Tuzo - lililoelezwa kama "maalum" na wahamasishaji wake kwa sababu 2026 linaambatana na maadhimisho mawili ya maadhimisho ya miaka mia nane ya kifo cha Mtakatifu Francis na maadhimisho ya ishirini ya Kifo cha  Mtakatifu Carlo Acutis, lililowasilishwa asubuhi ya Jumanne, tarehe 3 Februari 2026, katika Ukumbi wa Marconi kwenye Jumba la  Pio , Makao Makuu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Un momento della conferenza stampa di presentazione nella Sala Marconi di Palazzo PIo.

Chachu ya Udugu

"Leo tunahitaji kutazama ulimwengu kupitia macho ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis," alisema Kardinali Lazzaro You Heung-sik, Mwenyekiti wa  Baraza la Wakleri, wakati wa uwasilishaji. Hata hivyo mnamo 2023, alitoa Tuzo kwa kijiji huko Chad, Afrika, kwa mpango wa kutengeneza mkate ulioitwa "Bethlehemu, Nyumba ya Mkate."  "Katika wakati wetu," Kardinali aliendelea, "tunaona migongano na majeraha mengi, na dhana ya kiuchumi inayotumia rasilimali za dunia vibaya. Ndani ya unga huu, tunataka kuwa chachu ndogo ya udugu na chanzo cha msukumo wa utakatifu," alihitimisha, "kuonyesha mfumo mpya wa kiuchumi kwa nyakati hizi."

Ishara halisi ya uchumi mpya

Askofu Domenico Sorrentino, Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la  Assisi – Nocera Umbra – Gualdo Tadino, ambaye mnamo 2021 aliandika kitabu kiitwacho "Francis wa Assisi na Uchumi wa Udugu," alielezea wazo lililo nyuma ya Tuzo hilo. "Ilinijia mnamo 2013, Papa Francisko alipokuja Assisi kutembelea Mahali Patakatifu pa kujivua nguo. Papa alikuwa na huzuni sana kwa sababu kulikuwa na vifo vingi vya  wahamiaji. Kwa hivyo nilifikiria kutoa ishara halisi ya uchumi mpya, nikiuita kwa jina la Mtakatifu Francis wa Assisi na Mtakatifu Carlo Acutis, kwa sababu wote wawili," alihitimisha Askofu, "walijiweka katika nafasi ya maskini. Mbinu mbili tofauti, lakini zimeunganishwa na upendo wa udugu."

Kuelezea maana ya Tukio hilo

Ushirikiano dhidi ya sheria za soko

Padre Giulio Albanese, mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kijamii na Ofisi ya Ushirikiano wa Kimisionari miongoni mwa Makanisa ya Vicariate ya Roma, akiangalia hali ya sasa ya kimataifa, alizindua upya "wazo la ushirikiano," hasa "katika ulimwengu unaotawaliwa na falme zinazoweka sheria zao, ambapo kukata tamaa kunatawala katika pembezoni mwa kuwepo na ambapo ushirikiano wa pande nyingi uko katika mgogoro." Hili ndilo lengo la mpango huu, ambao, mjumbe wa tume ya tathmini alihitimisha, "unatoa msukumo na mfumo mbadala." Utambuzi huu unaheshimu miradi katika pembe za mbali zaidi za dunia na, kama Martina Giacomel, afisa wa Baraza la Kipapa la Kukuza Maendeleo Jumuishi ya Binadamu, Utafiti na Tafakari, alivyoelezea, unategemea kigezo cha "hasa ​​kuhimiza mpango wa vijana walio chini ya miaka 35."

Tuzo ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis
Tuzo ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis

Mipango inayokuwa fursa za kazi

"Tuzo hii si kuhusu ustawi, bali ni kuhusu kuzalisha fursa," alielezea Monsignor Anthony Figueiredo, mratibu wa tuzo hiyo. "Mnamo 2022," aliendelea, "ilienda kwenye mradi wa matofali ya mkaa uliotengenezwa kwa maua ya yungiyungi ya maji yaliyokaushwa na maganda ya nazi, uliopendekezwa na jamii huko Manila, Ufilipino, ambayo sasa inafanya kazi kutokana na wazo hili. Mnamo 2025, Tuzo hiyo ilienda India na kuunga mkono mpango wa simu ya dharura kwa vipofu na viziwi." Miradi inayokua kupitia ushiriki. "Miaka minne iliyopita, tulipokea maombi 30 kutoka nchi 15. Mwaka 2025 , tulipokea mipango  60 kutoka nchi 50, mingi kutoka Afrika na Asia. Mpango huu ni wa kinabii na wenye maono," alihitimisha mratibu wa tuzo hiyo ya kimataifa, "ili kufikia maeneo maskini zaidi na yaliyosahaulika zaidi."

Uno dei premi in palio, il "manto di Francesco".

Moja ya zawadi itakayotelewa pamoja na tuzo la mshindi(Joho)

Sherehe ya tuzo itafanyika Assisi mnamo Mei 16.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mipango ni tarehe 28 Februari  2026. Maombi yatatathminiwa na jopo la wataalamu sita. Sherehe ya tuzo itafanyika tarehe 16 Mei 2026 huko Assisi, siku ya siku kuu ya Madhabahu ya Kujivua. Mpango ulioshinda utapokea zawadi ya Euro 50,000 na "joo la Francis," lililoundwa na mbuni Brunello Cucinelli, ambalo linaadhimisha ishara ya Askofu wa Assisi wa wakati huo, Guido, ambaye alifunika Poverello alipovua nguo zake mbele ya baba yake, Pietro Bernardone. Alama ya Mtakatifu Francis na Mtakatifu Carlo Acutis pia itatolewa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

04 Februari 2026, 10:46