Oceania/Vanuatu:Wamewasili huko Vanuatu wamisionari 3 wa Kisalesiani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko akikutana na vijana katika Uwanja wa Sir John Guise huko Port Moresby, nchini Papua New Guinea, tarehe 9 Septemba 2024, wakati wa Ziara yake ya Kitume nchini humo, katika hotuba yake alionesha furaha ya kukutana nao wakiwa na ari na furaha kwa kile wanachofanya na kufikiria. Papa alisema: “Mfikiri kuna hali moja tu maishani ambayo tunaweza kuwatazama wengine ni njia ya kuwasaidia kuinuka. Ikiwa mmoja wenu ameanguka, ameshuka kidogo katika maisha ya maadili, ninyi ni lazima umwinue.” Hii ndiyo njia ya Kanisa na njia ya Wamisionari. Ni katika muktadha huo wa njia ya Wamisionari ambapo. Tumeguswa sana kuona jinsi Don Bosco anavyotusaidia kweli kutimiza ndoto yake huko Oceania," alisema Padre Alfred Maravilla, Mkurugenzi wa Utume wa kwanza ya Wasalesian wa Don Bosco, iliyofunguliwa huko Port Vila, Vanuatu, mnamo tarehe 13 Desemba 2025.
Kutumwa kwa Wamisionari 3 wa kwanza huko Vanuatu
Wakala wa Habari za Kisalesiani, ambao ulifuatilia historia yake, ulitangaza hatua hii mpya kwa Shirika la Kipapa la habari za Kimsionari Fides. Kwa kutumwa kwa wamisionari wake watatu wa kwanza kwenda Vanuatu mnamo Desemba 8, 2025katika siku kuu ya Mkingiwa Dhambi ya Asili, alisema Philip Rinaldi" Makamu wa Jimbo la Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon (PGS), kuwa iliashiria uzinduzi rasmi wa uwepo wa Wasalesian katika nchi ya 137 ya Shirika hilo. Mnamo tarehe 18 Desemba 2025, timu mpya ya wamisionari, iliyojumuisha Padre Alfred Maravilla, Salesian kutoka Ufilipino, Padre Moïse Paluku, Salesian kutoka Congo, na Ndugu Paulus "Noce" Bataona, kutoka Indonesia, walitua katika makazi yao ya muda, wakilenga kuelewa muktadha wa kichungaji na utamaduni wa wenyeji, na baada ya muda, kuandaa mpango wa Wasalesian unaoweza kukabiliana na hali ya vijana katika nchi hii. Wakiwa wapya, waanzilishi wa Wasalesia walikuwa wamepanga kusherehekea sikukuu ya Don Bosco, Januari 31 iliyopita, kwa njia rahisi, peke yao na mapadre na watawa.
Kujifunza kuhusu Don Bosco
Hata hivyo, bila kutarajia, kama wamisionari wanavyosema katika maelezo yao, waamini wa parokia wenyewe waliwakaribia Wasalesia, wakiomba kujifunza zaidi kuhusu Don Bosco. Wakikubali mwaliko wa waamini wa Parokia, Misa ya novena iliadhimishwa katika kanisa kuu, na alasiri, wamishonari, pamoja na viongozi wa parokia, walitembelea Jumuiya tisa, wakileta picha na masalio ya Don Bosco. "Jinsi watu wanavyoheshimu masalio kwa kujitolea na maombi ilikuwa jambo lililotugusa sote." Jumuiya za wenyeji zilijitokeza kwa wingi kukaribisha 'ziara ya hiyo ya Wana wa Don Bosco,' na “wengi walitujia kwa ajili ya Kuungama baada ya miaka mitano au hata kumi!” alishuhudia mmoja wa waanzilishi wa kimisionari. Wakati wa Sherehe ya Don Bosco, Kanisa dogo la kijiji lilikuwa limejaa waamini kwa ajili ya Misa iliyoongozwa na Chansela wa Jimbo la Port Vila.
Siku ya kuwasili kwa wamisionari wapya inakuwa siku ya Don Bosco
"Tuliguswa sana na jinsi watu walivyoandaa karibu kila kitu: sherehe, chakula cha mchana cha kiutamaduni cha Vanuatu, programu, na vifaa," alisema Padre Paluku. Wao wenyewe walisema hadharani: kuanzia sasa, hiyo ni 'Siku yetu ya Don Bosco'! Katika kumbukumbu ya miaka 45 ya kuwasili kwa Wasalesia wa kwanza huko Papua New Guinea na kumbukumbu ya miaka 150 ya Msafara wa Kwanza wa Wamisionari wa Salesian, ufunguzi huko Vanuatu unawakilisha hatua muhimu ya kihistoria na ishara ya kasi mpya ya kitume. Vanuatu, ambacho ni kisiwa cha Melanesia kusini magharibi mwa Pasifiki, kinaundwa na visiwa vikuu 13 na kinakaliwa na takriban watu 341,500.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here