Tafuta

Sr Abby Avelino,Mratibu wa Kimataifa wa Talitha Kum, Mtandao wa Kimataifa wa Watawa dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu. Sr Abby Avelino,Mratibu wa Kimataifa wa Talitha Kum, Mtandao wa Kimataifa wa Watawa dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu. 

Talitha Kum dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu:Amani huanza na utu

Mama Kanisa akiadhimisha Siku ya Maombi Ulimwenguni na Tafakari dhidi ya Biashara Haramu ya Haramu ya Binadamu Februari 8,Sr Abby Avelino,Mratibu wa Kimataifa wa Talitha Kum,Mtandao wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa Ulimwenguni,alielezea changamoto na vipaumbele vya sasa katika mapambano dhidi ya Biashara haramu ya binadamu.

Na Francesca Merlo – Vatican.

Biashara haramu ya binadamu inabaki kuwa mojawapo ya aina za janga zilizoenea sana nyakati hizi duniani. Inaathiri mamilioni ya watu katika mabara yote, na hufanywa kimya kimya, ikiwezeshwa zaidi na teknolojia mpya, njia za uhamiaji na ukosefu wa usawa wa kimataifa. Kila mwaka, katika Siku ya Maombi Duniani na Tafakari dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu inatafuta kufichua uhalifu huu uliofichwa.

Juma la Kazi

Kuanzia tarehe 4 hadi 8 Februari 2026, Roma iliandaa mfululizo wa mikutano, sala na mipango ya umma inayoadhimisha Siku hii ya 12 Duniani ilyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko. Ikichochewa na mtandao mpana wa mashirika mengi yaliyojitolea kushughulikia biashara  haramu ya binadamu, ikiwa ni pamoja na Talitha Kum, Juma hilo lilizingatia uelewa, kinga na hatua Madhubuti kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Amani huanza na utu.”

Kuwa pamoja na walionusurika

Miongoni mwa wale walioshiriki kila siku katika kazi hii ni Sr Abby Avelino, Sista wa Maryknoll na Mratibu wa Kimataifa wa Talitha Kum, mtandao wa kimataifa wa Masista Wakatoliki wanaofanya kazi dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Akizungumza  na Vatican News, alitafakari jinsi biashara haramu ya binadamu inavyobadilika, kwa nini kinga inazidi kuwa ya haraka, na jinsi heshima inavyopaswa kubaki katikati ya majibu ya uhamiaji na unyonyaji. Sr Abby alizaliwa Ufilipino na kulelewa Marekani baada ya familia yake kuhama. "Mimi ni Mfilipino kwa moyo," alisema, "lakini maisha yangu yameumbwa kwa kuishi kati ya tamaduni nyingi."

Kazi yake ya umisionari nchini Japan iliashiria mwanzo wa kuhusika kwake katika juhudi za kupambana na biashara haramu ya binadamu, hasa kupitia wahamiaji na wakimbizi, na watoto wasiosindikizwa na kuwa nao karibu, wengi wao wakiwa wanawake na watoto." Kupitia kusikiliza uzoefu wao," alielezea, "nilianza kuona jinsi uhamiaji na biashara haramu ya binadamu vina ukaribu." Uzoefu huo uliongoza Talitha Kum, Mtandao ambao sasa upo katika zaidi ya nchi mia moja. Ingawa ufahamu wa biashara haramu ya binadamu umeongezeka, alibainisha kuwa tatizo lenyewe linaendelea kukua. "Watu wengi leo hii wanatambua biashara haramu ya binadamu kama ukiukaji wa utu wa binadamu," alisema. "Lakini visa vingi bado vimefichwa, na idadi tunayoiona haioneshi uhalisia kamili."

Wadanganywa kwa  ulaghai

Alielezea kuwa mbinu za ulaghai zimebadilika sana. "Sio tu maskini au wasio na elimu ya kutosha ndio walengwa," Sr Abby alisema. "Leo hii, wafanya biashara haramu wanazidi kuwalenga vijana waliosoma vizuri na wanaozungumza lugha kadhaa." Mbinu nyingi kupitia fursa za kazi mara nyingi hufanyika mtandaoni, kupitia ofa zinazoonekana kuwa halali na za kitaalamu. "Waathirika wengi wanaamini wanaomba kazi halisi," alielezea. "Wanaoneshwa mikataba, visa na mahitaji yaliyo wazi." Kutokana na uzoefu wa Talitha Kum, wanabainisha kuwa ajira za uongozi zinatoka katika sehemu za Afrika na Asia, ikiwa ni pamoja na Ufilipino. Baadhi ya waathiriwa husafirishwa katika shughuli za ulaghai kwa njia ya mtando wa kulazimisha, mara nyingi katika maeneo ya mpakani kati ya Myanmar, Cambodia na Thailand. "Wanaambiwa watafanya kazi nchini Thailand," alisema, "lakini huishia kunaswa katika mikumbo mibaya. Mara tu wanapofika huko, hawawezi kuondoka." Waathiriwa hulazimishwa kufanya kazi ili kulipa gharama ya uajiri wao na usafiri. "Wanafunzwa, wanapewa majukumu na kushinikizwa kutoa matokeo. Huu ni uhalifu uliopangwa, na ni aina ya utumwa mamboleo.”

Kinga

Uokoaji unabaki kuwa mgumu, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro. "Ufikiaji wa baadhi ya maeneo ni mdogo sana," Sr Abby alielezea. "Mara nyingi, msaada unawezekana tu mara tu mtu anapofika mpakani." Talitha Kum unafanya kazi na washirika waliopo kwenye mipaka hiyo, tayari kuwasaidia wale wanaofanikiwa kutoroka. Kwa sababu hiyo, kinga ni muhimu kwa kazi ya mtandao. "Tunataka kusitisha biashara haramu ya binadamu kabla haijatokea," Sr Abby alisema. Elimu na uelewa ni muhimu, hasa kuhusu uhamiaji wa salama. "Uhamiaji ni haki ya binadamu, lakini watu lazima wajue haki zao na kuelewa hatari zinazohusika."

Alikumbuka kisa ambapo padre anayemjua alimwomba athibitishe ofa ya kazi kwa mwanafamilia anayejiandaa kuhama. "Kupitia mtandao wetu, tuligundua kuwa kampuni haikuwepo. Ukaguzi huo rahisi ulizuia hali inayoweza kuwa hatari." Kulingana na Sr Abby, waathiriwa wengi hawatambui kwamba wanasafirishwa. "Mara nyingi, wafanyabiashara haramu ni watu wanaowaamini," alielezea. "Baadhi ya walionusurika wametuambia hawakuwahi kufikiria kwamba jamaa wa karibu  au mtu anayewajua angewatumia vibaya." Wakati mwingine waathiriwa hulazimishwa kuwaajiri wengine kama sharti la kuishi kwao wenyewe.

Kiwewe cha kudumu

Athari kwa walionusurika ni ya muda mrefu. "Biashara haramu  ya binadamu husababisha kiwewe kikubwa. Huathiri hisia ya utu na usalama wa mtu." Kupona kunahitaji muda, kumsindikiza  muathiriwa na baadaye upatikanaji wa kazi thabiti. "Bila uchumi mzuri, watu hubaki katika mazingira magumu." Licha ya haya, baadhi ya waathiriwa huchagua kuzungumza hadharani kuhusu wanachopitia. "Wanataka kuwazuia wengine kupitia mateso kama hayo," Sr Abby alielezea. "Ushuhuda wao ni muhimu, hasa kwa vijana." Alikumbuka kukutana na waathirika ambao mwanzoni hawakujitambulisha kama waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu," alisisitiza.

Watu wengi husema, 'Sikujua hii ilikuwa biashara haramu ya binadamu, Sr alieleza tena kwamba "Baadaye tu, wanapoanza kuelewa haki zao na kile kilichochukuliwa kutoka kwao, ndipo wanapogundua kilichotokea." Ukosefu huu wa ufahamu, hufanya kuzuia biashara hii haramu kuwa kitu cha dharura. Kwa sababu hiyo, kitengo cha Talitha Kum kinasisitiza sana elimu katika kila ngazi. "Masista wetu hufanya kazi katika Shule, Parokia na Jamii," Sr Abby alisema. "Tunaanza hata na watoto, kwa sababu ufahamu lazima uanze mapema." Alibainisha kwamba, vijana wote wako hatarini sana na pia ni mawakala wa mabadiliko. "Vijana wanapoelewa kinachoendelea, wanasaidia kulindana."

Suala la kibinadamu, si la kisiasa

Alitafakari mijadala ya sasa ya kimataifa kuhusu uhamiaji na sheria kali za uhamiaji, Sr Abby alisisitiza umuhimu wa kumweka mwanadamu mbele. "Uhamiaji mara nyingi huchukuliwa kama suala la kisiasa tu," alisema. "Lakini kimsingi ni suala la kibinadamu." Alirejea uzoefu wa uhamiaji wa familia yake na hofu inayohisiwa na wahamiaji wengi leo hii. "Sera zinazotegemea kutengwa au adhabu huongeza udhaifu," alibainisha. "Hazishughulikii sababu za uhamiaji au biashara haramu."

Amani huanza na heshima

Kwa  upande wa Sr Abby, ujumbe wa Siku hii kwa mwaka huu uko wazi ambao unaongozwa na mada ya  "Amani huanza na heshima," alisema. "Ikiwa heshima hailindwi, amani haiwezi kudumishwa." Biashara haramu ya binadamu, haiwezi kutenganishwa na masuala mapana ya kimataifa. Umaskini, majanga yanayohusiana na hali ya hewa, migogoro na uhamiaji wa kulazimishwa vyote huongeza udhaifu, alisisitiza. "Watu hawaachi nyumba zao kirahisi. Wanapolazimika kuhama, wafanyabiashara haramu huwa tayari kutumia fursa hiyo." Kwa hivyo, kazi ya Talitha Kum inaenea zaidi ya uokoaji na uhamasishaji hadi utetezi na ushirikiano katika ngazi ya kimataifa. Mtandao huu unafanya kazi ndani ya nchi, alielezea, lakini unabaki umeunganishwa kimataifa, ukishiriki taarifa na kujibu maswali kuvuka mipaka. "Hili si jambo ambalo kundi moja linaweza kufanya peke yake," Sr Abby aliongeza. "Linahitaji uwajibikaji na mshikamano wa pamoja - miongoni mwa taasisi, serikali, jamii na watu binafsi."

TALITHA KUM

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here.

 

09 Februari 2026, 11:01