Congo,DR,Radio Don Bosco:sauti ya amani katika nchi ya vita
Na Federico Piana – Vatican.
Sauti ya amani na matumaini, ukombozi kwa maskini na waliokandamizwa(uzoefu wa Radio Don Bosco katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo). Lakini Je ni nani anasikiliza Radio Don Bosco? Ni maskini, watu wanaoteseka. Hawana kompyuta, simu ya mkono au televisheni na wanategemea masafa ya radio kuwasikia wale wanaozungumzia matatizo yao." Na idadi ya watu wa Lubumbashi, jiji la tatu kwa ukubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ambalo lina matatizo mengi. Kwanza kabisa, vita vinavyozidi kuwa vya umwagaji damu kati ya jeshi la kawaida na kundi la waasi la M23, ambalo linaathiri vibaya Mkoa wa Kivu Kaskazini hasa. Lakini sio hayo tu.
"Mitaa inatetemeka"
Na "Sisi kweli ni sauti ya wasio na sauti," alielezea Padre Matthias Amani, Msalesian na Mwanashirika katika kituo kilichoanzishwa na Shirika lake mnamo rtarehe 15 Agosti 2014, ambacho kilitokana na majivu ya kituo kingine cha radio kutoka miaka ya 1960. Masafa ya Radio Don Bosco yanaenea zaidi ya Lubumbashi na katika miji mingine katika Mkowa wa Katanga ya Juu, kama vile Likasi na Kasumbalesa cha mwisho kilijengwa hatua chache kutoka mpaka na Zambia. Miongoni mwa vipindi vyake vikuu ni kimoja chenye kichwa: “Mitaa inatetemeka.” Kinawaonesha wasikilizaji wakiripoti moja kwa moja au mbashara kuhusu mambo ambayo si sahihi: kuanzia utekaji nyara na magenge ya wahalifu hadi ukosefu wa maji. "Na wakati mwingine mamlaka husikiliza na kuingilia kati, kuja kusaidia," alifichua Padre Amani. Roho ya kituo, hatimaye, ni kuwa chombo cha kuhudumia jamii, ambacho moja ya malengo yake makuu ni kuelimisha vijana, ambao, kulingana na takwimu za hivi karibuni, wanawakilisha asilimia 60 ya idadi ya watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Sauti ya Kanisa na mwelekeo wa kijamii na kisiasa
“Kituo chetu hakitafuti tu kuongeza uelewa wa Don Bosco na kazi za Wamisionari Wasalesian, lakini pia kina kazi muhimu ya kukuza elimu ya wavulana na wasichana. Hapo awali, hakukuwa na kituo cha radio chenye kusudi hili: kulikuwa na vile vilivyokuwa vikiripoti tu mambo ya wanasiasa wa eneo hilo.” “Baada ya muda, aliongeza Padre Amani, Radio Don Bosco pia imekuwa sauti ya Kanisa na hakika haijaacha mwelekeo wake wa kijamii na kisiasa, ambao unajitokeza kupitia matangazo yanayohusu afya ya umma, watoto wa mitaani, haki, na matendo ya upendo, pia usalama: "Hasa huko Lubumbashi, kuna hofu ya utekaji nyara na magenge, ambayo mara nyingi hutokea usiku. Kwa hivyo, kituo chetu cha radio huandaa mijadala ambapo tunaweza kujadili hali halisi.”
Changamoto za Radio
Padre huyo alisisitiza kwamba “Bila shaka, tunawaalika wawakilishi wa serikali, pamoja na wale kutoka asasi za kiraia na wanachama wa upinzani." Mijadala hii ya wazi hairushwa kamwe katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, alisisitiza. "Kwa sababu hatutaki kamwe kuingia katika masuala ambayo yanaweza kusababisha mgawanyiko. Tunajaribu kumpa kila mtu sauti." Radio Don Bosco hakika imekuwa na shida zake na nguvu ya kisiasa hapo awali. "Usipozungumza sana kuhusu siasa, zinakuacha peke yako. Vinginevyo, wasipomkamata mtu na kumpeleka gerezani, kodi zako zitaongezeka, na una hatari ya kulazimika kuzima redio. Vituo vingi vimezima vipeperushi vyao. Na Radio Don Bosco pia imekuwa na matatizo haya."
"Lazima tulete amani kwa kusikiliza na kuwaacha jamii kuzungumzia amani"
Hata hivyo, shinikizo kubwa halijamzuia Padre Amani na wale wanaofanya kazi naye kutoka kwa kanuni moja thabiti: kuendelea kuwa taa ya amani katikati ya kusahaulika kwa vurugu za mzozo. "Ni dhamira yetu: lazima tulete amani kwa kusikiliza na kuwaacha makabila yote ya watu wetu wanaotaka amani wazungumze. Kwa sababu sote ni Wakongo." Ingawa Padre Amani, ambaye yuko Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, umbali mfupi kutoka kitovu cha mzozo, sasa hawezi kuripoti kuhusu kinachoendelea kwa sababu za busara na usalama, anaendelea kuwafahamisha wasikilizaji wake kadri awezavyo: "Siwezi kutuma habari kuhusu serikali, lakini ninaweza kuzungumzia kinachoendelea katika jumuiya zetu. Kwa mfano, vita vilipoanza, tulizungumzia kuhusu jumuiya zetu za Kisalesian, ambazo tulilazimika kuzifunga." Mbali na hilo, katika eneo hilo lenye joto kali, hakuna hata taarifa yoyote ya bure. "Sijaona waandishi wa habari wowote hapa wenye uwezo wa kuripoti kwa uhuru kuhusu kinachoendelea. Kwa bahati mbaya, haya ni matunda ya vita."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here