Tafuta

Mahujaji wakiwa kwenye foleni ya kutembelea masalia ya Mtakatifu Francis katika Kanisa la Chini la Basilika ya Kipapa na Conventi Takatifu ya Mtakatifu Francis huko Assisi. Mahujaji wakiwa kwenye foleni ya kutembelea masalia ya Mtakatifu Francis katika Kanisa la Chini la Basilika ya Kipapa na Conventi Takatifu ya Mtakatifu Francis huko Assisi.  (ANSA)

Assisi:Maelfu ya Mahujaji wafika kutoa heshima ya masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi

Maelfu ya watu wamefika kuona masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi,yaliyowekwa wazi kwa heshima ya kumbukizi ya miaka 800 tangu kifo chake. Kuanzaia tarehe 22 Februari hadi tarehe 22 Machi,mahujaji na waamini kutoka pande zote za dunia wataweza kusali mbele ya masalia hayo.

Na Christopher Wells - Vatican.

Takribani mahujaji 18,000 na wageni kutoka Ulimwengni kote, wamefika mbele ya masalia ya Mtakatifu Francis huko Assisi kuanzia Dominika tarehe 22, wakitumia fursa hii adhimu kutoa heshima kwa Mtakatifu huyu aliyependwa zaidi katika historia ya Kanisa. Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 800 ya kifo cha “Poverello,” yaani “Maskini” mabaki ya yule maskini mdogo wa Assisi, masalia ya mifupa ya Mtakatifu Francis yaliwekwa wazi katika Basilika ili kumuenzi. Hii ni mara ya kwanza kwa masalia ya Mtakatifu huyo kuwekwa hadharani, tangu yalipohifadhiwa ndani ya Basilika hiyo  mnamo mwaka 1230. Masalia haya yatabaki hadharani kwa umma kwa muda wa mwezi mmoja, kuanzia Februari 22 hadi 22 Machi 2026.

The relics of St Francis of Assisi

Masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi(ANSA)

Mazingira ya tafakari na Furaha

Padre Giulio Cesario,OFMConv alisema, maelfu ya watu wanaofika kwa mara ya kwanza Assisi kuona masalia ya Mtakatifu Francis wameingia kwenye “uwepo wa tafakari na furaha pia”kutoa heshima kwa masalia ya Mtakatifu Francis na kumsikiliza akiwanong’oneza ndani ya mioyo yao, neno jema na lenye kuchochea ukuaji,” alibainisha. Padre Cesario ni Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Konventi Takatifu ya Assisi, alitoa shukrani za dhati, kwa wale wote waliofika kuonyesha upendo wao kwa Mtakatifu Fransis na wale walioshirikiana na ndugu wafransiko kufanya tukio hilo kuwa halisi na udugu.

Pilgrims and visitors pass by the relics of St Francis

Wanahija na wageni wakipita mbele ya Masalia ya Mtakatifu Francis  (ANSA)

Uhuru kutoka “katika Fikra za Kiulimwengu”

Siku ya kwanza ya kuweka hadharan masalia haya, ilipewa heshima ya pekee kwa kuanza na adhimisho la Misa Takatifu iliyoongozwa na Mwakilishi wa Kipapa wa Makanisa ya Kipapa ya Assisi, Kardinal Angel Ferandez Artime na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume. Katika mahubiri yake, Kardinali alibainisha kuwa, Mtakatifu Francis alikuwa huru kutokana na “nadharia za kiulimwengu,” uhuru ambao hautafuti kumiliki vitu ila kujitolea kwa Mungu, uhuru usiotafuta kutawala bali kuhudumia. Kardinal alibainisha kuwa, kuthamini uhuru huu haina maana ya kutafuta kimbilio katika mambo ya kale, bali ni kukabiliana changamoto za wakati wa sasa. Akiongozwa na tafakari ya masomo ya siku, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashairika ya Kitawa na Vyama vya Kitume, aliwaalika waamini kujiuliza, tunapoanza kipindi cha Kwaresima kama “kama tunataka kuishi kwa kufuata mantiki ya kujitosheleza kwa mamlaka au kwa kufuata mantiki ya utii wa imani kwa Mungu.”

Cardinal Ángel Fernández Artime celebrates Mass in the Upper Church of the Basilica

Kardinali Ángel Fernández Artime aliadhimisha misa katika Kanisa kuu la Juu ya Basilika ya Mtakatifu Francis wa Assisi(ANSA)

Kushinda Vizingiti

Akirejea kutoka katika Injili  ya majaribu ya Yesu akiwa jangwani, Kardinali Artime, alibainisha kuwa Mtakatifu Francis pia alipitia majaribu kama haya, badala ya kuyachukulia kwa kiburi, uchu wa mali, na kujiridhisha mwenyewe, badala yake alichagua udogo, umaskini na utii. Mtakatifu Fransic alisema, “chagua kumwabudu Mungu peke yake.” Kardinali alibainisha kuwa, ushindi dhidi ya majaribu, hautuachi sisi kujifungia bali hutusaidia “kuwa wazi kwa mahitaji ya wengine,” akirejea kwa Kristo aliyetoka jangwani na kwenda kuhubiri habari za ufalme wa Mungu, na Fransic kwa kumfuasa Mungu alishinda majaribu na kuwakumbatia wenye ukoma pamoja na dada na kaka zake wengine. Kardinali aliendelea kuelezea uwiano ulipo kati ya maandiko na tendo la kuheshimu masalia ya Mtakatifu Francis, ambayo siyo tu tendo la kumbukizi, ila ni mwaliko mahususi wa kujiuliza sisi wenyewe “Je, jangwa langu liko wapi? Kuna majaribu gani ndani yangu? Ni wapi ambapo Mungu ananialika nifanye ushuhuda wa Imani?””

Relics of St Francis of Assisi

Masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi (AFP or licensors)

MIAKA 800 TANGU KIFO CHA FRANCIS

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

 

25 Februari 2026, 09:41