Venezuela,Maaskofu:tunaomba kwa ajili ya mema ya nchi,kwa ajili ya umoja na amani
Vatican News
"Tudumu katika maombi kwa ajili ya umoja": huu ndio ujumbe wa usaidizi na ukaribu ambao Baraza la Maaskofu wa Venezuela unawahutubia watu wa Mungu kupitia njia zake za mitandao ya kijamii. "Kwa kuzingatia matukio yanayoendelea leo katika nchi yetu, tunamwomba Mungu awape Wavenezuela wote utulivu, hekima, na nguvu," Maaskofu waliandika kufuatia shambulio la Marekani dhidi ya Caracas, lililoamriwa na Rais Donald Trump, kumkamata Rais Maduro na mkewe na kuwashtaki kwa shitaka la biashara haramu ya dawa za kulevya na ugaidi.
Tunaomba amani mioyoni na katika jamii
Maaskofu, wanaoonesha mshikamano wao na "waliojeruhiwa" na "familia za wale waliokufa," wanawaalika watu "kuishi kwa tumaini na maombi ya dhati kwa ajili ya amani" katika "mioyo yao na katika jamii." "Tunakataa aina zote za vurugu," maaskofu wanaongeza, wakihimiza "kukutana" na "kusaidiana." Wanatumaini "kwamba maamuzi yanayofanywa ni kwa manufaa ya watu kila wakati", na hatimaye wanamwomba Mama Yetu wa Coromoto awasindikize kila mtu katika safari yao.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.