Tafuta

2026.01.16 Shule ya Muziki kwa watoto na barubaru wa huko Chiquitania,nchini Bolivia. 2026.01.16 Shule ya Muziki kwa watoto na barubaru wa huko Chiquitania,nchini Bolivia. 

Bolivia,Utume wa IDENTE:Kutoka vijijini kuna ukombozi wa vizazi vipya

Vijiji vilivyotengwa,utapiamlo na kuacha shule vinaashiria maisha ya kila siku huko Chiquitanía,ambapo wamisionari wamekuwepo tangu miaka ya 1980.Masista wamefungua nafasi za kukaribishwa na kujifunza.Hivyo,imani na utamaduni vinakuwa elimu,muziki,michezo na matumaini kwa watoto,vijana na familia.

Na Eleanna Guglielmi

Mwana wa urithi wa Kijesuit ambaye aliunganisha imani, sanaa, na muziki, Misheni ya Mtakatifu Miguelito huko Chiquitanía, nchini Bolivia, ilianza mwaka 1998, wakati wamisionari wa ‘Kristo Mwokozi’(IDENTE) walipochukua Chuo cha zamani cha kilimo kilichoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 kwa ajili ya watoto wa wakulima. Chuo hicho kimekuwa “Mji wa Monasteri” na kwa miongo kadhaa, kimewaelimisha mamia ya vijana katika taaluma za kiufundi na kibinadamu. Katika ramani hii ya mbali imeibua Okestra ya vijana inayohifadhi muziki wa Chiquita, shule ya mpira wa miguu, programu ya baada ya shule, ya  kusafiri, taasisi ya mafunzo, ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu, na miradi ya kulinda misitu na dawa za kijadi. Dhamira iliyounganishwa na maendeleo ya mwanadamu, ambapo utakatifu hupimwa na hatua ndogo ya kila siku.

Wamisionari wa kike na kiume kutembelea moja ya familia

Hadhi inaanzia kwenye benchi za shule

"Watoto wengi hufika shuleni bila kujua kusoma au kuandika," alisema Sr Amy Barilla, mmisionari wa Idente. "Hii ndiyo sababu programu za baada ya shule si za anasa, bali ni suala la utu: kuwapa fursa ya kuanza kutoka mwanzoni wa kiwa sawa na kila mtu." Watoto wengi kati ya umri wa miaka 5 na 13 huchelewa sana kusoma na katika somo la hesabu, wakihusishwa na utapiamlo, motisha duni, na ukosefu wa usaidizi wa kifamilia. Kwa vijana barubaru, kiwango cha wengi kuacha shule huongezeka, vinavyochochewa na umaskini, vurugu za majumbani, na ajira kwa watoto. Madarasa mengi yasiyo na rasilimali na mikakati, yanazidisha mgawanyiko. Vijijini kote vilivyotawanyika, mashamba dhaifu ya kilimo, na kilimo kinachokabiliwa na ukame hufanya maisha ya kila siku kuwa magumu zaidi.

Kwa msaada wa wamisionari wanazungukia nyumba za watoto ili kuwasindikiza kwenye masomo ya kiada 

Imani inakuwa taaluma na chakula

"Ndoto yetu ilikuwa kusindikizana na vizazi vipya bila kupoteza mizizi ya utambulisho wao," alisema Deisy Choque. Shule ya Muziki ya  Kwaya wa Mtakatifu  Miguelito" inakaribisha watoto na vijana 35 kutoka vijiji sita ambapo ala za muziki kama vile: violin, gitaa, na Kayamba huwa vyombo vya ukuaji wa kibinafsi na utamaduni. “Kayamba ilinisaidia kukua, na sasa nina ndoto ya kwenda Chuo Kikuu," alisema Maria Laura, mmoja wa wanafunzi. Pamoja na muziki, Shule ya Mpira wa miguu inawashirikisha vijana wapatao 250, ikibadilisha michezo kuwa fursa ya nidhamu na kuzuia hatari za kijamii. "Uwanjani, tunajifunza heshima na urafiki: ni familia ya pili," alisema Milos. Kupitia taasisi ya elimu endelevu, wamishonari, pamoja na wanaume, hutoa kozi katika ufundi, kilimo endelevu, na dawa za Kijadi kwa kuzingatia zaidi uhuru wa wanawake. "Kwetu sisi, utakatifu pia unamaanisha chakula, elimu, na heshima," anarudia Deisy Choque. "Imani haitangazwi kwa maneno pekee, lakini familia inapopata chakula cha kula na mtoto hupata nguvu ya kuendelea kusoma," anasema Jean Djeling.

Mizizi inayokuwa ya mustakabali

Chiquitanía bado ina kumbukumbu ya misheni za mapadre wa Kijesuit ambazo, tangu karne ya 17, zimeibua utamaduni wa asili na imara: maandamano, nyimbo, na sherehe za watakatifu walinzi zinaendelea kuashiria maisha ya jamii. "Kulinda ardhi yetu ni sehemu ya imani yetu," Milos alisisitiza. "Msitu mkavu wa Chiquitanía ni zaidi ya asili tu: ni kumbukumbu, utamaduni, na maisha kwa wale wanaoishi hapa." Kwa sababu hiyo, misheni inakuza uhifadhi wa misitu, elimu ya mazingira, urejeshaji wa dawa za kijadi, na mazoea endelevu ya kilimo. Wakati huo huo, misheni inakuza kujitolea kwake kwa mawasiliano ya kidijitali ili kuongeza uelewa wa kazi ya Mtakatifu Miguelito na kuvutia msaada kutoka kwa vyuo vikuu, watu wa kujitolea, na wafadhili.

Mamisionari wa kike na Kiume wa IDENTE na vijana baada ya shule

Utakatifu ni hatima ya pamoja

"Utakatifu si wazo la mbali, lakini ni uwezekano wa kila siku unaoonekana katika masomo, kazi, na maisha ya jumuiya," walisema Amy na Deisy. Uzoefu huo hautajirishi jamii tu, bali pia wale wanaojitolea kwao. "Kila wakati kijana kutoka Chiquitanía anapopata ufadhili wa masomo, ni kama vile jamii nzima imekubaliwa Chuo Kikuu," aliongeza Jean. "Hatuwafunzi watu binafsi tu bali  tunawekeza katika mustakabali wa pamoja." Mtawanyiko wa jamii, uhaba wa Mapadre, shida ya mafuta, na ukosefu wa huduma hubaki kuwa vikwazo vya kila siku. "Mara nyingi tunapaswa kupunguza usafiri wa watoto kwenda Mtakatifu  Miguelito, na sisi ndio tunaosafiri ili kufika vijijini," wamisionari walielezea. Hata hivyo macho yao yanabaki mbele: "Kwa imani, kujitolea, na mshikamano, hata nchi ya mbali inaweza kuwa chanzo cha mustakabali."

Ciquita, Bolivia.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

20 Januari 2026, 14:02