Tafuta

2026.01.22 2026.01.22 Ziara ya vijana wa Bossey katika jengo la  Pio makao makuu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Radio Vatican. 2026.01.22 2026.01.22 Ziara ya vijana wa Bossey katika jengo la Pio makao makuu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Radio Vatican. 

Juma la Kuombea Umoja wa Kikristo 2026:Uekumeni na matokeo yake ya kudumu

Kuanzia India hadi Roma,kijana mmoja anayesoma katika Taasisi ya Uekumeni ya Bossey alitafakari kuhusu umoja na haki,pamoja na maana ya Umoja wa Kikristo katika Ulimwengu uliovunjika."Ikiwa kila mmoja wetu atafanya kazi kwa ajili ya umoja katika muktadha wake mdogo,utasababisha hilo kutendeka.”Uekumeni,ukiishi kwa uaminifu na uvumilivu,unakuwa nguvu tulivu,ile ambayo haipigi kelele,bali ya kudumu.

Na Francesca Merlo – Vatican.

Jijini Roma, wakati  wa Juma la  Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo, 18-25 Januari, Uekumeni unakuwa sehemu ya maisha ya kila siku, na Vataican ilijazwa na Wakristo wa madhehebu yote ili kuleta uhai katika Umoja wa Kikristo. Miongoni mwa waliohudhuria Juama hili ni Abel Punnoose, Mkristo mwenye umri wa miaka 29 kutoka India na mshiriki wa Kanisa la Waamini la Mashariki, alifika Roma kuhudhuria  hafla hii kama mjumbe kutoka Taasisi ya Uekumeni ya Bossey ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC). Kwa Juma moja, kikundi hicho kilijikita katika maisha ya Kanisa Katoliki, kulitana na Makardinali, kusali pamoja, na kukabiliana na tofauti ambazo bado zinaashiria Jumuaya za Kikristo.

"Hili ni Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo," Abel alisema katika mahojiano na Vatican News. "Tuko hapa kuelewa tunapotofautiana, na pia kufanya kazi kwa makusudi ua kuwa na umoja." Bossey si taasisi ya kitaaluma tu bali pia ni mahali ambapo umoja wa kiekumeni huishi kila siku, Abel alisema. Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali hushiriki sio tu madarasa, bali pia chakula, sala na maisha ya kawaida.

"Mwanzoni, tofauti zinaonekana sana," alishuhudia. "Lakini baada ya muda, tunagundua kwamba tuna mengi ambayo yanafanana zaidi ya yale yanayokugawanya." Sala ndiyo huwa kitu kinachogeuza mawazo finyu.  "Tukiwa pamoja katika maisha ya kiroho, inatupa motisha ya kuwa na umoja. Si safari rahisi, tuna siku zilozongumu lakinii kwa kujitolea na nia njema, kuishi kiekumeni kunawezekana.

The Bossey Delegation listen to a talk at Vatican News - Vatican Radio

Uwakilishi wa Bossey wakisikiliza katika makao ya Radio Vatican-Vatican News.

Ukristo uliogawanyika na ulimwengu uliogawanyika

Abel alisisitiza kwamba Umoja wa Kikristo, si jambo la ndani pekee. Lina matokeo kwa ulimwengu ambyo Kanisa lingependa kutumikia . Akimnukuu Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Duniani, Mchungaji Profesa Dkt. Jerry Pillay, Abel alikumbuka onyo kali: "Ukristo uliogawanyika hauna usemi kwa ulimwengu uliogawanyika." Katika jamii zilizogawanywa na siasa, tabaka, itikadi, na hofu ya mwingine, uaminifu wa shahidi wa Kikristo hujaribiwa kila siku. "Tukisema sisi ni sehemu ya Ufalme wa Mungu," aliendelea, "lazima tuoneshe waziwazi kwa maisha yetu." Mgogoro wa ndani wa mara kwa mara, alisisitiza, unadhoofisha ushuhuda wa Kanisa. Umoja, kwa upande mwingine, unakuwa aina ya tangazo.

Uhuru wa binadamu, huruma, na mshikamano na mateso, hujitokeza kama vipaumbele vya upamoja. Abel alizungumzia uhamiaji, mateso, na ugumu wa kiuchumi si kama masuala ya kufikirika, bali kama hali halisi zinazohitaji mwitikio wa umoja wa Kikristo. "Kuacha starehe kwa ajili ya wengine ni msingi wa imani yetu," alisema. "Katika madhehebu yote, hapa ndipo tunaweza kuungana kweli."

Kijana  Abel Punnoose katika mahojiano na Vatican News
Kijana Abel Punnoose katika mahojiano na Vatican News

Muktadha wa Kihindi: umoja huanza ndani

Kwa  upande wa Abel, maswali haya ni ya kibinafsi sana. Ukristo nchini India, alibainisha, unaanzia Mtakatifu  Thomas na una historia ndefu na ngumu, hasa katika jimbo lake la Kerala. Hata hivyo licha ya karne nyingi za uwepo, Wakristo wanabaki kuwa wachache - na migawanyiko inaendelea hata ndani ya Kanisa. "Inasikitisha kuona ubaguzi wa rangi upo ndani ya jamii za Kikristo," alisema. "Kama hatujatatua  ukosefu wa haki ndani yetu, tunawezaje kuwa mashahidi tunayeaminika ulimwenguni?" Wakati huo huo, anatambua ushiriki wa muda mrefu wa Kanisa katika elimu, haki ya kijamii, na kupunguza umaskini nchini India. Mengi yamefanyika, lakini mengi yamebaki. “Vijana lazima wachukue jukumu,” alisisitiza. “Lazima waende sehemu za mateso na kuwa na  msimamo.”

Kubadilishana zawadi kwa pamoja

Huko Bossey, Abel amepata nafasi sio tu ya kuzungumzia magumu haya bali pia ya kusikilizwa. Uekumeni, alisema, lazima uondoke kwenye ukosefu wa usawa wa zamani ulioundwa na historia ya ukoloni na kuelekea zawadi  kwa  uhalisi kati ya Kaskazini na Kusini. “Kusini mwa Dunia mara nyingi huhitaji usaidizi hata wa kimwili” alieleza lakini pia tuna mengi ya kutoa, roho yetu, utamaduni wetu na historia zetu.” Umoja wa kweli, anaamini, hukua kupitia kusikiliza sana na pia kupitia kutoa.

 

The Bossey Ecumenical Institute delegation with Pope Leo XIV

Wawakilishi wa Taasisi ya Kiekumeni ya Bossey wakiwa na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kukutana na Papa

Wakati wa kukutana na Papap Leo XIV ulikuwa wa maalum sana, wakati wa ziara yao kama wajumbe. “Alikuwa amesimama mbele yangu,” Abel alikumbuka. “Alitujulia hali na akatoa muda kuwa nasi. Unyenyekevu wake ulibaki ndani mwangu.”  Urahisi wa Papa Leo XIV  katika mkutano huo ndio ulioacha hisia halisi ya Abel. "Mtu katika nafasi yake hakuhitaji kufanya hivyo," Abel alisema. "Lakini alifanya hivyo. Hilo ni jambo ambalo nimejifunza na ningependa kuiga katika majukumu yoyote ninayoweza kuwa nayo siku zijazo, natumaini kuwa mnyenyekevu kama Papa Leo alivyokuwa nasi."

Hatua ndogo, mawimbi ya kudumu

Wanapomaliza ziara yao,  Abeli ​anatumaini ya mafanikio katika siku zijazo. Alisema huenda ajasione Umoja wa Kikristo wanaoujitahidi katika maisha yake. Lakini anaamini kwamba hiyo si sababu ya kukata tamaa. "Ikiwa kila mmoja wetu atafanya kazi kwa ajili ya umoja katika muktadha wake mdogo," alisema, "utasababisha hilo kutendeka.” Uekumeni, ukiishi kwa uaminifu na uvumilivu, unakuwa nguvu tulivu, ile ambayo haipigi kelele, bali ya mawimbi ya kudumu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

 

23 Januari 2026, 16:10