Tafuta

Askofu Hanna Jallouf. Msimaizi wa Kitume wa kanisa la Kilatini, nchini Siria Askofu Hanna Jallouf. Msimaizi wa Kitume wa kanisa la Kilatini, nchini Siria 

Siria:'Vita na kuhama tena visitokee Aleppo'

Askofu Hanna Jallouf,Msimamizi wa Kitume wa Aleppo,alilalamika kuhusu mapigano yanayoongezeka kati ya jeshi la Siria na Vikosi vya Kidemokrasia vya Siria katika maeneo yenye Wakurdi wengi.

Na Christine Seuss na Valerio Palombaro – Vatican.

Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14, Siria inahitaji utulivu, lakini "mambo hayaendi vizuri" huko Aleppo, kulingana na Askofu Hanna Jallouf, msimamizi wa kitume wa jiji hilo. Alizungumza na Vatican News kutoka mji wa Kaskazini mwa Siria, ambapo tangu tarehe 6 Januari 2026, mapigano makali yalianza tena kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wenye idadi kubwa ya Wakurdi wanaoitwa Vikosi vya Kidemokrasia vya Siria(SDF). "Mchungaji lazima awe na kundi lake katika nyakati ngumu,"aliongeza Askofu, akilalamika kwamba hali huko Aleppo inaonekana " kuzidi kuzorota zaidi."

Wengi wamejeruhiwa

Idadi ya vifo vya muda vya uhasama, ni watu watano wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa, wakiwemo raia, huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kuwa zaidi ya watu 30,000 tayari wamekimbia mji huo. Askofu Jallouf alitaja video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha maiti zikiwa zimelala chini ya magari mitaani. Jeshi la Syria limetangaza amri ya kutotoka nje katika vitongoji vya Sheikh Maqsoud na Ashrafieh na kuwaamuru wakazi wa maeneo kadhaa yanayotawaliwa na Wakurdi kuhama majumbani mwao kwa kutarajia mashambulizi dhidi ya SDF.

Kuwasaidia wale waliokimbia makazi yao

Hata hivyo mikondo ya misaada ya kibidamu miwili ilifunguliwa  ili kuwaruhusu watu kupita, Askofu Jallouf alisema. "Sisi kama Wakristo tumeweka maeneo matatu ya kuwahudumia waliokimbia makazi yao, mawili katika uaskofu wa Kilatini (moja katika chuo cha Nchi  Takatifu; jingine katika Kanisa la Matamshi)." Kanisa la Orthodox la Siria pia lilifungua moja katika uaskofu wao, huku Waislamu wakifungua misikiti minne. "Karibu watu 3,500 tayari wamechukuliwa, huku wengine wamepata hifadhi katika baadhi ya nyumba za kibinafsi au mahali pengine," alisema. "Mbali na kutoa mahali salama, tuliwapa blanketi na bidhaa muhimu."

"Tutegemee kwamba Bwana atatupa nguvu, ujasiri, na amani," alisema Askofu Jallouf, akielezea matumaini yake ya utulivu wa muda mrefu baada ya miaka 14 ya vita. "Tayari tumeteseka vya kutosha," alihitimisha Askofu. "Tusiwe na umwagaji wa damu au hofu tena. Tayari kuna Washami milioni 11 wanaoishi nje ya nchi: hakupaswi kuwa na wakimbizi zaidi."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

12 Januari 2026, 10:56