Tafuta

2024.09.30 Prof. Wolfgang Palaver, Rais wa Pax Christi Austria. 2024.09.30 Prof. Wolfgang Palaver, Rais wa Pax Christi Austria.  (Gudrun Sailer)

Pax Christi Austria:Papa anatoa mwaliko wa kinabii wa kutumaini mwisho wa vita

Mtaalimungu Wolfgang Palaver,rais Austria wa kitengo cha Shirika la kimataifa(Pax Christi),alitoa maoni kuhusu Ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya Amani Duniani wa mnamo Januari 1, 2026,akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican. Ametiwa moyo sana "kufanyia kazi ulimwengu wenye haki zaidi," lengo ambalo halipaswi kuchukuliwa kuwa la kipekee: "Kristo Mfufuka anashinda imani ya kifo na anatufundisha kwamba kuishi bila vurugu kunawezekana."

Na Gudrun Sailer – Vatican.

Amani si utopia, lakini inahitaji ujasiri fulani kutumaini, hata dhidi ya matumaini yote, kwamba itatimia. Hii ndiyo sababu ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya 59 ya Amani Duniani, Januari 1, 2026, "ni wa kinabii, kwa sababu haujiruhusu kuathiriwa na ushahidi kwamba matumaini yanapungua kila mahali, na hauachi amani katika ulimwengu wa utopia." Hivi ndivyo Wolfgang Palaver, rais wa Pax Christi Austria  Shirika la Kimataifa na Profesa mstaafu wa Mafundisho ya Kijamii ya Kikristo katika Chuo Kikuu cha Innsbruck, anavyotafsiri maandishi ya Papa Leo XIV kuwa: kama msimamo wazi dhidi ya kujiuzulu na dhidi ya sera ya kimataifa inayozidi kutawaliwa na mantiki ya nguvu.

Amani ya Kristo Aliyefufuka

Kiini cha ujumbe huo  wa Siku ya Amani ni mtindo tayari ambao ulitamkwa na Papa Leo XIV,  jioni ya kuchaguliwa kwake mnamo tarehe 8 Mei  2025, na sasa umefafanuliwa tena kuwa: "Hii ni amani ya Kristo aliyefufuka, amani isiyo na silaha, amani inayoondoa silaha, ya unyenyekevu, na inayodumu. Inatoka kwa Mungu, Mungu anayetupenda sote bila masharti." Palaver alisisitiza umuhimu wake wa kitaalimungu na kimaadili: "Kwa msisitizo juu ya 'amani isiyo na silaha,' Papa alirejea waziwazi ujumbe wa kiinjili wa kutotumia nguvu kwa Yesu; akizungumza badala ya 'amani isiyo na silaha,' inaonesha njia halisi za kujikwamua na vurugu". Katika ujumbe wa Siku ya Amani Duniani, "kama mtaalamu wa maadili ya amani, nisingeweza kutarajia zaidi kihalisi", alibainisha Mtaalimungu  huyo wa Austria.

Kashfa ya Dini inayohalalisha Vita

Kukemea kwa Papa matumizi ya dini kuhalalisha vita na utaifa pia ni jambo la kuchochewa sana, bila kusita akiita "aina ya kufuru inayoficha Jina Takatifu la Mungu." Palaver alikubali kuwa: "Katika kukataa utaifa unaochochewa na dini na matumizi mabaya ya jina la Mungu kuhalalisha vurugu, Papa alielezea kwa usahihi kazi kuu ya jumuiya za kidini katika kuimarisha amani." Kwa maana hiyo, mazungumzo ya kiekumene na ya kidini yanabaki kuwa zana muhimu, hasa baada ya mashambulizi yanayochochewa na dini.

Kuhifadhi Majeraha ya Vita Vikuu

Hoja nyingine muhimu katika ujumbe wa Papa Leo XIV wa amani inahusu jukumu la vyombo vya habari na taasisi za elimu. Palaver alirudia kutoa onyo la Askofu wa Roma dhidi ya kuacha  utamaduni wa ukumbusho, ambao badala yake unapaswa kuweka ufahamu hai wa uharibifu wa vita viwili vya dunia. Papa Leo XIV pia alikumbuka usemi wa Papa Francisko wa "Vita vya Tatu vya Dunia vilivyogawanyika vipande vipande  na alitaja  ongezeko kubwa la matumizi ya kijeshi duniani.

Palaver alisema, "Tukiongeza gharama kubwa za silaha, inaonekana wazi kwamba tuko katika mzunguko hatari wa vurugu."Kwake, yeye kuonesha wazi hali hii ni kazi kuu ya vyombo vya habari na taasisi za elimu. Lakini hiyo haitoshi. "Kuelezea hatari hiyo tu kunaleta hatima isiyo na matumaini ambayo ingeongoza moja kwa moja kwenye shimo," alisema rais wa Pax Christi Austria. Hapa mwelekeo wa kitaalimungu wa ujumbe unatumika: "Tunahitaji nuru ambayo Aliyefufuka ametupatia, ambayo inatuhakikishia kwamba amani inawezekana." Pamoja na mtazamo halisi wa ulimwengu, Palaver alisema, "amani lazima iwe 'kanuni' kama Papa alivyosema kihalisi, ya njia yetu ya kutazama uhalisia. Ni kwa mtazamo huu tu ndipo tumaini lenye uwezo wa kuongoza kujitolea halisi kwa amani linaweza kuzaliwa.

Kutia moyo kwa waleta amani wote

Kwa upande wa Palaver, miezi ya kwanza ya upapa wa Papa Leo XIV ulionesha wazi mwelekeo huo. Papa, amekuwa wa kutia moyo na msaada" kwa Pax Christi, na ujumbe wake kwa Siku ya Amani Duniani unatoa nguvu na motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya ulimwengu wa haki na amani zaidi. Hii ndiyo njia iliyochukuliwa miaka themanini iliyopita na harakati ya Pax Christi yenyewe, iliyozaliwa kutokana na maridhiano kati ya Wakatoliki wa Ufaransa na Ujerumani baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na sasa ipo katika kila bara, alihitimisha.

PAX CHRISTI
02 Januari 2026, 15:05