Tafuta

2026.01.19 WYD SEOUL 2027: Uzinduzi wa Kwaya na Okestra. 2026.01.19 WYD SEOUL 2027: Uzinduzi wa Kwaya na Okestra. 

Kwaya ya WYD,Seoul 2027,yazinduliwa:Kuhudumia Ibada Kuu za Siku ya Vijana Duniani

Misa ya Uzinduzi wa Kwaya na Okestra ya WYD Seoul 2027 iliadhimishwa Januari 17 saa 12:00 jioni katika Kikanisa cha Familia cha Kanisa Kuu la Myeongdong.Askofu Mkuu Peter Chung,wa Seoul,alikuwa mshereheshaji mkuu,akiungana na mapadre wa Kamati ya Maandalizi siku ya WYD huko Seoul 2027 (LOC)katika sherehe ya pamoja.

Vatican News

Katika kuendelea na maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani(WYD) ijayo, Misa ya Uzinduzi wa Kwaya na Okestra ya WYD Seoul 2027 iliadhimishwa Januari 17 saa 12:00 jioni katika Kikanisa cha Familia cha Kanisa Kuu la Myeongdong nchini Korea Kusini. Askofu Mkuu Peter Chung, wa Jimbo Kuu la Seoul, alikuwa mshereheshaji mkuu, akiungana na mapadre wa Kamati ya Maandalizi mahalia ya WYD Seoul 2027 (LOC) katika sherehe ya pamoja.

Uzinduzi huo ulizingatia sherehe kuu za kiliturujia za Siku ya Vijana Dunianili( WYD) huko Seoul 2027, ambapo kundi hilo lilizinduliwa kwa ajili ya  huduma ya muziki  ambayo itakuza ushiriki wa maombi na kuwasaidia mahujaji kutoka ulimwenguni kote,  kuinua wimbo mmoja wa imani. Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu Chung aliwakaribisha wajumbe wapya waliochaguliwa na kutoa shukrani kwa kujitolea kwao kutumikia kupitia muziki Mtakatifu.

Nembo ya Siku ya Vijana huko Seoul 2027
Nembo ya Siku ya Vijana huko Seoul 2027   (Dicastero per i laici, la famiglia e la vita)

“Tumsifu Yesu Kristo, alianza mahubiri yake na kuongeza kuwa "Ni furaha kuwakaribisha nyote mliokusanyika hapa kutoa muziki katika huduma ya WYD Seoul 2027, na ninawashukuru, kweli, kwa uamuzi wenu wa kutumikia,” alisema, huku akibainisha kuwa uanachama ulionesha umri mpana wa kuanzia vijana hadi wale wenye miaka yao ya thelathini na kwamba waombaji walikuwa wametoka nchini kote, ikiwa ni pamoja na Jeju na majimbo mengine ya  kusini. Askofu Mkuu alisisitiza kwamba huduma yao haikuwa tu jukumu la muziki bali sadaka ya kiroho ambayo ingewaumba wanachama na wale watakaowahudumia.

"Kwa kila mmoja wenu, huduma hii, kwa namna moja, ni kwa ajili ya imani yenu wenyewe; lakini zaidi ya yote, ni huduma inayotolewa kwa Mungu na huduma inayotolewa kwa Kanisa," alisema, akiwahimiza waamini kuona miezi mirefu ya maandalizi kama safari iliyojaa neema. Akikumbuka maneno ya Baba Mtakatifu, Askofu Mkuu Chung alisisitiza uwezo wa kipekee wa muziki wa kubeba moyo kuelekea kwa Mungu na kuongeza ushiriki katika liturujia. "Papa Leo XIV alisema mnamo Desemba kuwa, 'Muziki ni kama daraja linalotuongoza kwa Mungu.'

"Ninaamini kujitolea na juhudi zenu zitawafanya nyinyi mafundi mnaojenga daraja hilo kwa washiriki wa WYD Seoul 2027," alisema. Pia Askofu Mkuu alisisitiza maana ya kikanisa ya muziki wa liturujia, akiwakumbusha waamini kwamba huduma yao ilitokana na sala ya Kanisa. "Wito huu si tu mwongozi wa kuongeza kwenye wasifu; ni wito wa kujitoa, kwa Mungu, kwa Kanisa, na kwa vijana waliokabidhiwa kwetu. Muziki wa kiliturujia si pambo tu; ni sehemu muhimu ya liturujia," alisema.

Wajumbe wa Siku ya vijana 2027 wa Kwaya na Okestra wakishiriki misa ya  Uzinduzi 

Baada ya mahubiri, Sherehe ya kuzinduliwa rasimi ilifanyika, ikiwa ni pamoja na Ahadi ya Wanachama hao lwa kutoa Tamko la Msingi, na Kutangazwa kwa Sheria Ndogo na Askofu Mkuu Chung. Sherehe hiyo pia ilijumuisha kuanzishwa kwa Mkurugenzi wa Timu ya Muziki ya WYD Seoul 2027 LOC, Padre John Ho-young Choi, ambaye aliwasilishwa kama mkurugenzi aliyepewa jukumu la kuongoza huduma ya muziki ya Siku ya Vijana (WYD)katika maandalizi ya tukio hilo.

Kufikia Misa ya Uzinduzi, Kwaya ilikuwa na wanachama 126 (kundi la sauti mchanganyiko lenye sehemu nne), na Okestra ilikuwa na wanachama 78, ikiwa ni pamoja na vyombo 68 vya Magharibi na vyombo 10 vya kitamaduni vya Kikorea. Kundi hilo lililenga kukua hadi wanakwaya 200 na wanakwaya 100, huku majaribio ya ziada yakipangwa kufanyika Januari 31, huku likiendelea kuimarisha msingi wake wa muziki na kiroho kwa sherehe za kiliturujia za WYD Seoul 2027.

Kuhusu timu ya Kwaya na nyimbo 

Timu ya Muziki ya WYD Seoul 2027 LOC ilisimamia uendeshaji wa Kwaya na Orkestra ya WYD Seoul 2027 na kuratibu Shindano la Nyimbo za Tukio la  WYD Seoul 2027, ambalo lilikuwa linaendelea mbele hadi mzunguko wa mwisho. Nyimbo tano za mwisho zilipaswa kuwasilishwa kwa Kiti Kitakatifu kwa ajili ya kutoa kauli ya mwisho na  baada ya hapo zitakazofaa  ziweze kuendelezwa.

Picha ya pomoja na Askofu Mkuu baada ya uziduzi wa Kwaya itakayoimba siku ya vijana(WYD Seoul 2027 Choir & Orchestra)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Bofya hapa tu:Just click here

19 Januari 2026, 09:28