Kenya:Watawa"Marafiki wa Walevi,"wanasaidia Kupambana na Uraibu
Sr. Michelle Njeri,OSF.
Kituo cha Watakatifu Wasio na Hatia(Holy Innocents BPSS Centre), ni kituo cha kidini cha urekebishaji na hurudishaji na matibabu ya magonjwa ya akili kilichoanzishwa na Askofu Salesius Mugambi, Askofu wa Jimbo la Meru, na Sr. Veronica Nkirote Rukunga, Mwanzilishi wa Shirika la Masista Shirika la Watumishi wa Watakatifu Wasio na Hatia, Shirika linalohudumia kituo hicho. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2021, ambacho kinashughulikia mojawapo ya matatizo makubwa ya kijamii nchini Kenya: ulevi, matumizi ya dawa za kulevya na changamoto zinazoongezeka za afya ya akili. Wakiwa na dhamira ya kuponya waliojeruhiwa katika jamii kwa upendo, huruma isiyo na hukumu, masista wameunda nafasi salama ambapo maumivu hukutana na kusudi na kuvunjika hukutana na matumaini.
Askofu Salesius Mugambi wa Meru na Sr Veronica Nkirote Rukunga,Mkurugenzi wa Kituo cha Watakatifu Wasio na Hatia(BPSS),Timau
Utume ulizaliwa kwa imani na huruma
Sr. Veronica Nkirote Rukunga alieleza zaidi sababu za kuanzisha kituo hicho kuwa: "Shirika la masista wa Watakatifu Wasio na hatia, hujibu mahitaji ya wanajamii waliojeruhiwa zaidi. Karama yetu inaongozwa na Mama Yetu wa Huzuni, aliyesimama na mwanaye alipokuwa katika mateso kama vile masista sasa tunasimama karibu na wale wanaopambana na uraibu na magonjwa ya akili. Tangu mwanzo, watu wengi wamekuja kwa ajili ya matibabu na wameunganishwa tena katika jamii. Kama masista tunakabiliana na majanga ya siku hizi: matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya," alisisitiza. Kituo cha Masista wa Watakatifu Wasio na Hatia (Holy Innocents Center BPSS), hufanya kazi kwa saa 24 kwa siku, ikitoa huduma kamili chini ya nguzo nne za BPSS: kibayolojia, kisaikolojia, kijamii na kiroho. Njia hii inahakikisha kwamba wagonjwa wanatibiwa sio tu kimwili, lakini kwa ujumla, kwa heshima na huruma.
Kuponya mwili, akili na roho
Huduma zinazotolewa katika kituo hicho ni za kina na za makusudi. Sr. Purity Mathenge, Msimamizi, alielezea wigo la kazi yao katika kituo hicho. "Tangu 2021, tumekuwa tukitoa huduma kwa wagonjwa wa nje na wagonjwa waliolazwa, huduma kwa wagonjwa wenye shida ya akili, matibabu ya mtu binafsi na ya kikundi, kuondoa sumu ya matibabu na mwongozo wa kiroho," alisema. Tangu wakati huo, masista wameshuhudia mabadiliko ya maisha ya watu. "Mtu mmoja tuliyemtoa mitaani sasa ameajiriwa, na mwingine aliyepona sasa ni mmoja wa wafanyakazi wetu. Hatua hizi zinatufanya tuendelee," alisema Sr Purity. Wanafanya kazi na madaktari wa magonjwa ya akili, wauguzi, wanasaikolojia, mafundi wa maabara, washauri, na wafanyakazi wa kijamii. Kila mtu ana jukumu lake. Na kila mara tunaomba kwamba washirika zaidi na watu wema watajiunga nasi,” alibainisha Sr. Purity.
Sr. Purity Mathenge katika ushauri na Kelvin Mwega na Ann Wangari,wahudumu wa Kituo cha Watakatifu Wasio na Hatia(BPSS).
Sayansi na utunzaji wa kitaalamu hukutana na uponyaji wa kiroho
Katika kiwango cha kliniki, kituo hicho hutoa utunzaji wa muundo na wa kibinafsi. Kelvin Mwega, mwanasaikolojia wa kimatibabu na Mkuu wa huduma za kliniki katika Kituo hicho, alieleza kuwa: "Tunafanya uchunguzi wa kimaabara kwa viungo muhimu kama vile ini na figo kabla ya kulazwa. Kwa kuzingatia mahitaji ya mtu binafsi, tunatoa msaada wa kitabibu wa kuondoa sumu mwilini na matibabu ambayo yanajumuisha msaada wa kibayolojia, kisaikolojia, kijamii na kiroho."
Tiba ya familia na mafunzo ya stadi za maisha,pia ni sehemu ya mpango huo
"Baada ya kuwaruhusu wagonjwa kurudi nyumbani punde wanapopata nafuu, sisu huwatembelea wagonjwa nyumbani na kuwafuatilia ili kuzuia kuangukia tena katika matumizi ya madawa ya kulevya au pombe," alisema Bwana Mwega. Motisha wake ni wa kibinafsi sana. "Kinachonisukuma ni kuona watu wanapona, watu ambao jumuiya ilikuwa imekata tamaa kwao na wao wenyewe pia. Inanipatia matumaini na ujasiri. Hakuna hali isiyoweza kurekebishwa. Ni suala la muda tu. Matibabu ya hurekebishwaji inafanya kazi.”
Jumuiya inayojali
Kazi hii ya kubadilisha maisha imewapatia moyo wengi walio nje ya kuta za watawa kujiunga na huduma hii.Vincent Mutwiri, mshiriki mlei wa Shirika hilo, ni miongoni mwao. “Tunawaunga mkono Masista wa Shirika la Watumishi wa Watakatifu Wasio na Hatia kwa sababu karama yao ni ya kipekee na inahitajika haraka,” alisema. “Tunakwenda mahali ambapo masista hawawezi kwenda kutoa huduma na msaada wao katika jumuiya.” Masista mara nyingi huitwa “Marafiki wa Walevi.” Bwana Mutwiri alisema ni cheo wanachobeba kwa unyenyekevu. “Upendo wao unaokoa maisha, na jamii inashuhudia," alisema.
Sr. Joan: "Hamko peke yenu"
Mtoa huduma katika kituo hicho Sr. Joan Nyakato anawaalika wote wanaopambana na uraibu(utumiaji wa madawa ya kulevya) au shida ya afya ya akili kuwasiliana na kuwaeleza wengine matatizo yao. “Njooni, tuzungumze. Sote tunahitaji akili timamu na maisha. Huo sio mwisho wa maisha, hamko peke yenu. Tuko tayari kukushika mkono,” alisema. Sr. Joan aliongeza kuswma kuwa: “Kila mtu anakaribishwa kutoa wakati, rasilimali, au nguvu. Kwa pamoja, tunaweza kuziba pengo na kuwasaidia kaka na dada zetu kuachana na uraibu.”
Wito wa Huruma
Katika ulimwengu ambapo uraibu (hutumiaji wa madawa ya kulevya) na ugonjwa wa akili mara nyingi huleta unyanyapaa na ukimya, Masista, wafanyakazi wao, na washirika wao wa kawaida wanaionesha Kenya na Ulimwengu kwamba hakuna aliye zaidi ya kukombolewa. Wito wao ni rahisi na wa haraka: hebu tutembee pamoja kuelekea jamii yenye kiasi, iliyopona, na yenye huruma, maisha moja baada ya nyingine.