Jumuiya ya Taizé,mkutano ujao wa vijana nchini Poland
Vatican News
Mkutano ujao wa vijana wa Jumuiya ya Taizé utafanyika kuanzia tarehe 28 Desemba2026, hadi Mosi Januari 2027, huko Łódź, Poland. Ndugu Matthew, Mkuu wa Jumuiya ya Kiekuemene ya Taizé, alitangaza habari hiyo tarehe 30 Desemba jioni wakati wa masifu ya jiono katika mkutano wa jumuiya hiyo , ambao unahitimishwa Mosi Januari 2026 jijini Paris nchini Ufaransa.
Mahali pa mfano
Taarifa kutoka Jumuiya ya Taizé inakumbusha kwamba mkutano wa kwanza huko Poland (Wrocław, 1989-1990) uliambatana na kuanguka kwa Pazia la Chuma. Mkutano huu ujao wa Ulaya, wa sita huko Poland, ni mwaliko wa kuendelea kujenga amani ndani yetu na duniani. Kama Ndugu Matthew anavyopendekeza katika barua yake ya 2026, "kupitia wengine, tunaweza kushangaa kugundua kitu ambacho hatungekipata peke yetu."
Hamu ya Amani
Wakati huo huo, Mkutano wa 48 wa Taizé wa Ulaya huko jijini Paris, ukliwaleta pamoja vijana 15,000 kutoka Ulaya na ulimwenguni kote, amba ondano mwake walikuwemo takriban Waukraine 1,000 ambao, Jumuiya ilisisitiza kuwa "kupitia ushiriki wao wanaelezea hamu yao ya amani na undugu katika nchi yao iliyokumbwa na vita." Vijana wamekaribishwa katika familia au wamekaribishwa katika parokia.
Mkesha ulifanyika jioni ya tarehe 31 Desemba 2025 ukifuatiwa na "Siku kuu ya Mataifa." Mnamo Januari 1, ratiba ta chakula cha mchana cha mwisho kufanyika katika parokiani au na familia menyenyeji, kabla ya kuaga kwa mwisho, lakini ikuwatakia kuonana tena yaani “kwaheri ya kuonana”
Wajenzi wa Maridhiano
Papa Leo XIV aliwatumia ujumbe vijana waliokusanyika na jumuiya ya Taizé katika siku za hivi karibuni akiwa na ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin. Mwaliko wa Papa Leo ni kuwa "mahujaji wa uaminifu, wajenzi wa amani na maridhiano, wenye uwezo wa kuleta tumaini la unyenyekevu na furaha kwa wale walio karibu nawe."
Jumbe zingine pia zilitoka kwa Patriaki wa Kiekumeni wa Constantinople Bartholomew, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana António Guterres, na Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula von der Leyen. Maandishi hayo yalikumbuka kichwa na maana ya barua ya 2026 iliyoandikwa na Ndugu Matthew, ambayo inakumbusha swali, "Mnatafuta nini?", lililoulizwa katika Yohane 1:38 na Yesu kwa wanafunzi wa kwanza.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here