Tafuta

Askofu Hiiboro Kussala wa Jimbo Katoliki la Tombura -Yambio, Kusini mwa  Sudan. Askofu Hiiboro Kussala wa Jimbo Katoliki la Tombura -Yambio, Kusini mwa Sudan. 

Jimbo Katoliki la Tombura–Yambio limekuwa alfajiri Mpya kwa miito ya kikuhani!

Imani,Tumaini na Huduma yachukua Mizizi. Na hii ni furaha iliyotanda kwenye jimbo Katoliki ya Tombura–Yambio huku,hatua muhimu ya kihistoria kwa kuwekwa wakfu kwa mapadre wanne wapya na mashemasi sita,katika nchi ambayo imegubikwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya karibuni.

Sr. Christine Masivo – CPS – Vatican.

Sherehe ya kuwaweka wakfu Mapadre wanne na Mashemasi Sita katika jimbo la Tombura–Yambio hivi karibuni katika mwanzo wa mwaka tarehe 4 Januari 2026 ilisimama kama ishara yenye nguvu ya umoja na ufufuko wa kiroho, ikiakisi utume unaokua wa Kanisa na kujitolea kwake kumtumikia Mwenyezi Mungu na jamii.

Kuwekwa wakfu wa kishemasi na kipadre huko Sudan Kusini
Kuwekwa wakfu wa kishemasi na kipadre huko Sudan Kusini

Akiongoza sherehe hiyo Takatifu, Askofu Eduardo Hiiboro Kussala wa Jimbo hili alielezea “kuwekwa wakfu kama wakati muhimu katika maisha ya jimbo hilo”, na akatoa shukrani za dhati kwa “unyenyekevu,” akimshukuru “Mungu kwa zawadi ya mapadre na mashemasi wapya katika jimbo.” Alisisitiza kwamba “wito wao unaimarisha utenda kazi wa kichungaji wa Kanisa vema na ushuhuda wa imani miongoni mwa watu.”

Kuwekwa wakfu wa kikuhani
Kuwekwa wakfu wa kikuhani

Shukrani za dhati

Askofu alitoa heshima maalum kwa Parokia ya Mtakatifu Augustine, akiipongeza kwa “kujitolea kwao ili kufanikisha sherehe hii kwa hali na mali na kwa ukarimu wao kwa mpangilio wao kipekee.” Pia alitambua “michango muhimu ya Baraza la Watawa la jimbo na Utawala, kwaya, vikundi vya kitume, wanaume na wanawake, makuhani, makatekista, wahudumu wa kiliturujia, timu za usalama, na watu waliojitolea. Jitihada yao ya pamoja, alibainisha na ilionyesha vyema nguvu ya ushirikiano ndani ya Kanisa.”

Furaha ya kuwekwa wakfu
Furaha ya kuwekwa wakfu

Ushirikiano

Umuhimu wa tukio hilo ulienea zaidi ya mizunguko ya kikanisa, ukivutia uwepo wa viongozi kutoka Jimbo la Ikweta Magharibi, taasisi za serikali, mamlaka za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali, na sekta ya elimu. Askofu Kussala alisisitiza “ushiriki huu mpana kama mfano mzuri wa ushirikiano kati ya Kanisa na Jimbo, wakiwa wameungana katika kutafuta manufaa ya wote.”

Mashemasi wa Yambio Sudan Kusini
Mashemasi wa Yambio Sudan Kusini

Katika mahubiri yake kwa waamini, Askofu huyo alitoa wito wa maombi, nia njema, na usaidizi kwa jimbo, hasa kwa mapadre wapya waliowekwa wakfu wanapoanza huduma yao. Aliwatia moyo kutumikia kwa unyenyekevu, huruma, na uaminifu, kufuata moyo wa Kristo na kujitolea katika dhamira ya kujenga amani katika nchi inayotamani upatanisho na utulivu.

Mapadre wapya huko Yambio, nchini Sudan Kusini
Mapadre wapya huko Yambio, nchini Sudan Kusini

Askofu Kusala alielezea tukio hili linaashiria wakati wa kuyafanya mambo upya na kwa matumaini, upadrisho huo unaashiria sura mpya wa jimbo Katoliki ya Tombura-Yambio. Likiwa limeimarishwa na miito mipya, Kanisa la mahali hapo linasonga mbele kwa kujiamini, likiwa limefanywa upya katika imani, limeungana katika kusudi, na limetiwa moyo kuwatumikia watu wa Mungu kwa upendo.

UPADRISHO YAMBIO SOUTH SUDAN
08 Januari 2026, 13:38