Jimbo la Sion,Uswiss limesitikishwa na mkasa wa ajali ya moto huko Crans-Montana
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jimbo la Sion huku Uswiss, limapatwa namshtuko wa mkasa wa ajali ya mlipuko wa moto uliotokea usiku wa kufunga mwaka tarehe 31 Desemba 2025 katika bar ya“Le Constellation"huko Crans-Montana, Kaskazini mwa Uswiss. Katika taarifa yao iliyochapishwa tarehe 1 Januari 2026, inabainisha kuwa: “Kwanza kabisa, inaelezea wasiwasi wake, mshikamano, na huruma kwa waathiriwa wote, wapendwa wao, na familia zao. Usiku huu, ambao ungepaswa kuwa tukio la kusherehekea, umegeuka kuwa janga baya kwa mamia ya watu. Mawazo na sala zetu ziko pamoja nao.”
Idadi ya awali ya vifo kutokana na mkasa wa mkesha wa Mwaka Mpya huko Crans-Montana imeongezeka hadi 47 wamekufa na 113 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa katika hali mbaya. Mamlaka ziliripoti vifo lakini hii bado inapaswa kuzingatiwa kuwa ya muda kutokana na hali mbaya za majeruhi wengi waliopelekwa hospitalini. Mamlaka ya Uswisi yanaamini moto huo unatokana na tukio la "kuungua kwa moto", kuenea kwa kasi na kwa nguvu kwa miale ya moto. Umri wa wastani wa waliohudhuria sherehe iliyoandaliwa kusherehekea kuwasili kwa 2026 katika ukumbi maarufu katika eneo la mapumziko ya kuteleza kwenye theluji , huko Crans-Montana, Uswiss linalomilikiwa na wanandoa wa Kifaransa, ulikuwa na umri wa miaka 20. Ufikiaji wa Bar hiyo uliruhusiwa kuanzia umri wa miaka 16.
Jimbo la Sion linatoa shukrani kwa msaada wa huduma
Kwa njia hiyo Jimbo pia linatoa msaada na shukrani zake kwa wote waliohusika kwa njia mbalimbali katika kuwasaidia waathiriwa, wote waliokuwa mjini na katika hospitali mbalimbali zilizopelekwa majeruhi: wafanyakazi wa matibabu, polisi, na mamlaka za kiraia na mahakama. “Katika siku hii ya mwaka, ambayo kwa kawaida inajitolea katika Kanisa Katoliki kwa ajili ya Sherehe ya Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, na kwa maombi ya amani duniani kote, tunawakabidhi kwa njia ya pekee waathiriwa wote na wapendwa wao kwa huruma ya Bikira Maria,na tunaomba kwamba familia zilizoathiriwa ziweze kupokea, katikati ya huzuni yao, maneno ya kufariji ya huruma na usaidizi.”
Operesheni Ngumu za Utambuzi
Idadi hiyo pia inajumuisha watu kadhaa waliopotea, wakiwemo Waitaliano sita; Mwanasheria Mkuu wa jimbo hilo, Beatrice Pilloud, alisema kwamba rasilimali muhimu zimekusanywa "ili kuwatambua waathiriwa na kurudisha miili yao kwa familia zao haraka iwezekanavyo." Familia nyingi bado hazina uhakika kuhusu hatima ya waathiriwa siku moja baada ya moto mkubwa huko Crans-Montana: utambuzi wa miili 40 bado unaendelea, msemaji wa polisi alisema na kwamba kazi hiyo inaweza kuchukua siku kadhaa, kutokana na idadi kubwa ya waathiriwa na hali ya miili hiyo. Wakati huo huo, mamlaka zinawasiliana nao kwa karibu na pia zinatoa msaada wa kisaikolojia.