Tafuta

Kama Yesu alivyoteseka Msalabani hadi Kifo chake, na leo hii wafuasi wake katika baadhi ya nchi wanaendelea kuteseka na kufa. Kama Yesu alivyoteseka Msalabani hadi Kifo chake, na leo hii wafuasi wake katika baadhi ya nchi wanaendelea kuteseka na kufa. 

Idadi ya Wakristo wanaoteswa Duniani kote imeongezeka hadi milioni 388

Mkurugenzi wa chombo cha Uangalizi cha ‘Open Door’,alitoa ripoti ya kuakisi ulimwengu kwa mwaka 2026,akionesha rekodi mpya ya unyanyasaji dhidi ya wakristo.Christina Nani alizungumza na Radio Vatican kuwa, “wengi wa waathirika ni wanawake na watoto,huku akibainisha wasiwasi wake kwa maeneo ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Na Valerio Palombaro & Marco Guerra -Vatican.

Idadi ya Wakristo waliokabiliwa na mateso na hatari ya kunyanyaswa na jeuri duniani kote,  imeongezeka kwa watu milioni 8, ikilinganishwa na mwaka 2025,  hii inafanya kufikia rekodi ya milioni 388. ‘Kwa bahati mbaya huu ni mwaka wa rekodi tena’ alibanisha hayo Cristinìan Nani, Mkurugenzi wa Open Doors, ambapo Jumatano tarehe 14 Januari 2026 ilichapisha Orodha ya uangalizi wa Dunia kwa mwaka 2026 kuhusu wakristo wanaoteswa ulimwenguni kote. ‘Kati ya milioni 388 wanaoteswa, milioni 201 ni wanawake au wasichana, wakati milioni 110 ni watoto chini ya umri wa miaka 15.

Vurugu na Ubaguzi

Kwa muktadha wa ripoti ya chombo cha Ungalizi cha ‘World Watch’, idadi ya nchi zenye kiwango cha manyanyaso dhidi ya wakristo unaweza kutajwa kuwa ‘mkali’, kwani imeongezeka kutoka 13 hadi 15.  Korea Kusini imetajwa kuwa nchi hatari zaidi dunia kwa kuwa mkristo. Nchi zilizotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha mateso kwa wakristo duniani ni pamoja na Somalia, Eritrea, Libya, Afghanistan, Yemen, Sudan, Mali, Nigeria, Pakistan, Iran, India, Saudi Arabia, Myanmar, na Syria.

Siria ilitajwa kutoka kwenye hali “mbaya” hadi kwenye hali ya “waliokithiri,” kwa mujibu ya uangalizi huo. Akizungumza na Vatican News, Nani alibainisha kuwa Wakristo wa Siria wapo kwenye hatari zaidi, kwa sababu ya mamlaka mpya ya kisiasa bado iko kwenye “mgawanyiko,” kama ilivyojidhihirisha kwa siku za hivi karibuni kwa mapigano huko Aleppo. “Kulingana na takwimu zetu, ni Wakristo 300,000 tu wanasalia huko Siria, yaani mamia ya maelfu chini ya miaka kumi iliyopita,” alibanisha.

Kuakisi Kusini mwa Jangwa la Sahara

Baada ya kupungua, idadi ya mauaji ya Wakristo imeongezeka tena, kutoka 4,476 hadi 4, 849 kwa siku. Nigeria inatajwa kuwa kitovu cha ghasia hizo, huku waathirika  3,490, takribani asilimia 70 ya jumla ya watu waliouwawa duniani.  Idadi ya wakristo waliokamatwa kwa asababu ya imani yao bado haijabadilika yaani (4,712 ukilinganisha na 4,744 mwaka 2024), huku idadi ya wakristo waliotekwa ikipungua kutoka 3,302 dhidi ya 3775 ya mwaka 2024). Mashambulizi kwa Kanisa pia yamepungua kutoka ( 7,679 hadi 3,632), na mashambulizi dhidi ya nyumba na maduka (kutoka 28,368 hadi 25,794), huku idadi ya wahanga wa unyanyasaji, ubakaji, na ndoa za kulazimishwa ikiongezeka (kutoka 3,944) hadi 5,202).

Mashahidi wa Uganda
Mashahidi wa Uganda   (Joachim Schäfer - Ökumenisches Heiligenlexikon)

Mkurugenzi wa ‘Open Door’ alibainisha kuwa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kama eneo linalohitaji uangalizi wa pekee katika orodha ya mwaka 2026, hasa kwa sababu ya uwepo wa “Serikali dhaifu,” ambazo huwaacha wakristo hatarini kwa vurugu. Kwa sasa, “Kitovu cha uzito wa Ukristo kimehamia Afrika, lakini papo hapo kimsingi kinashambuliwa,” alisema Bwana Nani, akizungumza juu ya bara ambalo theluthi moja ya idadi ya wakristo wanaishi. Sudan inatajwa kuwa miongoni wa nchi muhimu hasa, aliongeza kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe,lakini pia Nigeria, Mali, Niger, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemograsia ya Congo (DR) na Msumbuji. Mashambulizi ya Wakristo katika mazingira haya dhaifu, yana sababu mbalimbali ambapo mambo ya kiuchumi huchanganyika na mwelekeo wa kidini.

Mashambulizi Nchini Nigeria

Orodha ya Waangalizi ya 2026 iliwasilishwa Jumatano tarehe 14 Januari 2026 katika ukumbi wa Seneti ya Italia jijini Roma, ikiambatana na maelezo ya shahidi kutoka Nigeria, moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi kwa ukosefu wa usalama uliokithiri. Katika siku za hivi karibuni, chombo hiki cha Ungalisi (Open Door) kilikusanya maoni kadhaa kutoka kwa Wakristo walio na wasiwasi  juu ya uwezekano wa kulipiza kisasi kwa vikundi vya kigaidi baada ya shambulio la Noeli huko  Amerika, ikiripotiwa pia matukio ya hivi karibuni ya ghasia kusini mwa Nigeria. Hii ni pamoja na wahanga 14 wa mashambulizi ya Serikali ya Kiislamu ya Afrika Magharibi (ISWAP), katika Mkowa wa Adamawa mnamo tarehe 29 Decemba 2025, pamoja na makumi ya waathiriwa mikononi mwa watu wasiojulikana wenye silaha ambao walivamia sokoni huko Dema, katika Mkoa wa Niger, tarehe 4 Januari 2026.

Wakristo wanaoteswa

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

16 Januari 2026, 18:09