Tafuta

Mwaka Jana tarehe 10 Januari 2025 lilizinduliwa Kanisa la Ubatizo wa Bwana mahali pajulikanapo(Al-Maghtas).Aliyeongoza ibada hiyo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Parolin. Mwaka Jana tarehe 10 Januari 2025 lilizinduliwa Kanisa la Ubatizo wa Bwana mahali pajulikanapo(Al-Maghtas).Aliyeongoza ibada hiyo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Parolin. 

Bethania ng'ambo ya Yordani, mahali Yesu alibatizwa

Wakati Mama Kanisa akiadhimisha ya ubatizo wa Bwana,katika mji wa Al-Maghtas,huko Jordan,uchimbaji wa akiolojia uligundua mabaki ya makanisa,vikanisa,mapango ya watawa na mahali pa kubatizia mahali pa ibada palipohusishwa na Ubatizo wa Yesu.Mnamo 2015 eneo hili liliandikwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.Mapapa watatu walifanya hija huko:Mtakatifu Yohane Paulo II,Benedikto XVI na Papa Francisko

Na Padre Pawel Rytel-Andrianik – Al-Maghtas.

Injili ya Yohane inasema kwamba Yohane Mbbatizaji alibatiza ng'ambo ya Yordani: “Hili lilitokea Bethania ng'ambo ya Yordani, ambapo Yohane alikuwa akibatiza” (Yh 1:28). Pia inasema: “Akaondoka tena ng'ambo ya Yordani hadi mahali ambapo Yohane alikuwa akibatiza hapo kwanza, na akakaa huko” (Yh 10:40). “Bethania ng'ambo ya Yordani” si Bethania karibu na mlima wa Mizeituni, ambao Yesu alitembelea mara nyingi, bali Bethania nyingine. Origen wa (karne ya 3), John Chrysostom wa (karne ya 4) na Wakristo wa wakati huo walisisitiza kwamba "Bethania ya ng'ambo ya Yordani" wakati huo ilijulikana kama Bethabara. Jina hili linaonekana katika baadhi ya hati za Injili ya Yohane zinazorejea hasa "Bethania ng'ambo ya Yordani" (Yh 1:28). Pia linaonekana kwenye ramani ya Madaba ya karne ya sita, ambayo inabainisha kwa njia hii mahali pa Ubatizo wa Yesu. Bethabara pia imetajwa katika Talmud. Leo mahali hapa panajulikana kama Al-Maghtas, ambayo kwa Kiarabu inamaanisha "ubatizo" au kuzamishwa.

Ushahidi wa Akiolojia

Hadi mwanzoni mwa karne ya 4, Ukristo, mara nyingi uliteswa katika Milki ya Kirumi, haukuweza kujenga mahali rasmi pa ibada. Hata hivyo, Wakristo wa Karne za Kwanza walipitisha kutoka kizazi hadi kizazi kumbukumbu ya maeneo yanayohusiana na maisha ya Yesu. Kati ya mwisho wa karne ya 5 na mwanzo wa karne ya 6, Mfalme wa Byzantine Anastasius I Dicorus alikuwa na Kanisa la Kwanza lililowekwa wakfu kwa Yohane Mbatizaji katika eneo ambalo sasa linajulikana kama Al-Maghtas. Kanisa hili liliharibiwa na mafuriko na matetemeko ya ardhi. Jengo hilo lilijengwa upya mara kadhaa, lakini labda kufikia karne ya 7-8 ni magofu tu yaliyosalia. Mhujaji mmoja wakati huo, aliyejulikana kama Theodosius (karibu mwaka  530), aliandika kuhusu kanisa hilo: "Kilomita tano kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, mahali ambapo Bwana alibatizwa, kuna nguzo ya pekee, ambayo msalaba wa chuma umewekwa; pia kuna kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji, lililojengwa na Mfalme Anastasius. Kanisa hilo ni refu sana, limejengwa juu ya vyumba vikubwa kwa sababu ya mafuriko ya Mto Yordani." 

Katika eneo hili, Basilika ya Utatu Mtakatifu pia ilijengwa. Jina la Kanisa hilo linakumbusha ukweli kwamba wakati wa ubatizo wa Yesu Utatu ulifunuliwa: Mungu Baba akizungumza kutoka mbinguni na Roho Mtakatifu katika umbo la njiwa juu ya Yesu. Uchimbuzi wa akiolojia unaonyesha kwamba lilikuwa kanisa kubwa, lenye urefu wa angalau mita 27 na upana wa zaidi ya mita 15, ingawa leo ni magofu machache tu yaliyosalia. Mbali na makanisa haya, wanaakiolojia wamegundua Basilika ya chini, mapango ya watawa, makanisa, michoro ya mosaic, sakafu za marumaru, na mahali pa kubatizia penye umbo la msalaba, vyote vimejengwa karibu na kila kimoja katika eneo ambalo sasa linajulikana kama "Bethania ng'ambo ya Yordani" huko Al-Maghtas. Karibu na Al-Maghtas, uchimbaji pia umegundua kilima cha Tell al-Kharrar, kinachojulikana kama Kilima cha Elijah (Jabal Mar Elias), kilichounganishwa na nabii Elijah. Katika kipindi cha Byzantine, labda katika karne ya 5, Monasteri ilijengwa hapo kwa heshima yake.

UNESCO: Thamani bora kwa ubinadamu

Mnamo 2015, eneo la "Bethania ng'ambo ya Yordani" (Al-Maghtas), ikiwa ni pamoja na Tell al-Kharrar, liliongezwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO. Tovuti rasmi inasema: “‘Bethania ng’ambo ya Yordani’ ina umuhimu mkubwa wa kidini kwa madhehebu mengi ya imani ya Kikristo, ambayo yamekubali eneo hili kama mahali ambapo Yesu wa Nazareti alibatizwa na Yohane Mbatizaji. Rejea hii iliwahimiza vizazi vya watawa, watawa wa kike, mahujaji na makuhani kuishi na kutembelea eneo hilo, na kuacha ushuhuda wa ibada yao na shughuli za kidini, kuanzia kati ya karne ya 4 na 15.

Mapapa huko ‘Bethania ng’ambo ya Yordani’

Baba Mtakatifu wa kwanza kutembelea Al-Maghtas alikuwa Mtakatifu Yohana Paulo II wakati wa Jubilei ya Mwaka 2000. Baba Mtakatifu Benedikto XVI alitembelea eneo hilo mwaka 2009 na kuzindua ujenzi wa Kanisa hilo akikumbuka ubatizo wa Yesu huko Yordani. Mwaka 2014, Baba Mtakatifu Francisko alitembelea eneo hilo na kukutana na wakimbizi wa Syria na Iraq, watoto wagonjwa, na watu wenye ulemavu waliopata kimbilio huko Yordani. Kanisa jipya la Ubatizo wa Bwana liliwekwa wakfu kwa heshima mnamo Januari 2025. Akimwakilisha Baba Mtakatifu Francisko  Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, aliongoza sherehe hiyo. Kwa sasa ni Kanisa kubwa zaidi  Katoliki huko Jordan, na eneo hilo pia linajumuisha makanisa ya madhehebu mengine ya Kikristo.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

12 Januari 2026, 10:47