Tafuta

Basilika ya Kuzaliwa kwa Bwana huko Yerusalemu. Basilika ya Kuzaliwa kwa Bwana huko Yerusalemu.   (©Custodia di Terra Santa)

Wito wa Noeli katika Makanisa ya Yerusalemu

Katika Ujumbe wa Noeli,Mapatriaki na wakuu wa Makanisa ya Yerusalemu,wanawaalika waamini wasichangenye kusitisha mapigano na amani ya kweli.Kiini chake ni Kuzaliwa kwa Kristo kama ishara ya matumaini na wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono amani ya haki,inayotokana na hadhi ya binadamu.

Vatican News

Katika nchi ya Mashariki ya Kati ambayo bado ina migogoro na ukosefu wa utulivu, mapatriaki na wakuu wa Makanisa ya Yerusalemu wametoa ujumbe wao wa kiutamaduni wa Sherehe za NOELI, wakisisitiza kwamba amani haiwezi kupunguzwa kuwa kusimamishwa tu kwa uadui, bali lazima iambatane na haki, upatanisho, na heshima kwa haki za msingi. Wakifungua maandishi  yao kwa  kurejea Barua kwa Waebrania isemayo:"Tumezungukwa na wingu kubwa la mashahidi, na tupige mbio kwa uvumilivu katika mashindano yaliyo mbele yetu, tukimkazia macho Yesu", viongozi Wakristo wanawaalika waamini kubaki imara katika tumaini hata wakati wa mateso makubwa zaidi.

Bethlehemu,ishara ya tumaini kwa Ulimwengu uliojeruhiwa

Kiini cha ujumbe huo ni maana ya Utu wa Kristo huko Bethlehemu, unaowasilishwa kama ishara ya tumaini lililozaliwa katika moyo wa udhaifu wa mwanadamu. Kama ilivyo kwa wachungaji usiku wa Noeli leo pia ujumbe wa Injili unatualika tusikubali hofu na kukata tamaa.

Kusitisha mapigano haimaanishi Amani

Wakati wanakaribisha usitishaji mapigano, ambao umeruhusu jumuiya nyingi kusherehekea siku kuu kwa uhuru zaidi, Mapatriaki wa Kanisa wanaonya dhidi ya hatari ya "amani bandia," wakikumbuka maneno ya nabii Yeremia: "Amani, amani, lakini hakuna amani." Kulingana na ujumbe huo, licha ya amani, vurugu, waathiriwa, na ukiukwaji wa uhuru unaoendelea katika Nchi Takatifu na nchi jirani.

Mawazo kwa wanaoteseka

Wakuu wa Makanisa wanarudia mshikamano wao na wale wote walioathiriwa na mgogoro huo na kuwaomba Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema kudumu katika sala na kujitolea kwa amani halisi na ya kudumu. Ujumbe huo unamalizika kwa salamu za Noeli kwa Jumuiya Mahalia na Wakristo ulimwenguni kote, kwa matumaini kwamba kuzaliwa kwa Yesu huko Bethlehemu kunaweza kufufua hamu ya upatanisho na haki.

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.

23 Desemba 2025, 11:31