Utume wa huruma ya watawa Wavincent kwa watoto nchini Urusi
Na Sr. Christine Masivo, CPS & Sr. Jana-Pavla Halčinová, DC
Mapadre wa Vincent walifika Urusi huko Nizhnyj Tagil mnamo 1997 kutoa huduma ambapo watu wachache kwa idadi ya watu walikuwa Wakristo. Kile kilichoanza kama jibu kwa watoto wenye njaa kikawa huduma ya huruma ya kudumu. Sr. Antonia Lednicka, Binti wa Upendo wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo (DC), ambaye anatoka Slovakia, amekuwa mtawa kwa miaka 30 na amehudumu nchini Urusi kwa miaka 23. “Padre Tomaž Mavrič, CM, mmoja wa waanzilishi, akiguswa na hali ya kuwaona watoto wakizurura mitaani, wakiwa na njaa, baridi, na wamesahaulika, alikuwa na wasiwasi na akazungumza kuhusu suala hilo na waamini wa parokia, kisha na mkuu wa shule, Natalia Petrovna, wa shule na akaanza ushirikiano wa Parokia Katoliki na taasisi za serikali. Wavincent walianza kutoa milo ya moto kwa watoto ambao hawakuweza kumudu chakula cha mchana, na kusababisha mpango wa upendo na imani katika vitendo. Waamini wa Parokia na mapadre walianza kwa kuwalipia watoto 50-80 chakula cha mchana shuleni ambao hawakuweza kumudu.
Mabinti wa upendo nchini Urusi
"Padre Tomaž aliwaomba watawa wahudumie," alisema Sr. Antonia. "Walifika mwaka 2000 kutoka Slovakia na kuanza Huduma ya Klabu ya Watoto, na kuwa kimbilio, darasa na makazi ya pili kwa mamia ya watoto wa eneo hilo. Kuanzia na mikutano ya kila juma, sasa wanahudumu kwa siku tano kila Juma." "Zaidi ya watoto 1,500 wamefaidika na klabu hii," alibainisha Sr. Antonia. "Kwa baadhi, ni mwaka mmoja, na kwa wengine, ni maisha yao yote ya shule." Dhamira ya klabu ilikuwa kutoa upendo, utulivu, na mwongozo kwa watoto ambao hawakuwa nao. "Watoto wengi hawakuwa waumini. Hatua kwa hatua, tuliwasaidia Waorthodox na Waislamu, lakini hilo halikuwa suala; tulihitaji kuwaonesha kwamba mtu anawapenda," anarudia Sr. Antonia.
![]()
Sr. Elisabeth akitoa madawa kwa mgonjwa wa kifua kikuu
Ushuhuda wa Ulyana
Ulyana, mnufaika mwenye umri wa miaka 34, anathibitisha utunzaji wa Vincentian. "Nina kumbukumbu nzuri za utoto wangu," anatabasamu. "Sote tulienda pamoja kuteleza kwenye kilima wakati wa baridi au kupanda milima. Hilo lilikuwa la kufurahisha, la starehe, na la nyumbani; nilikuwa na furaha zaidi kuliko hapo awali." "Nilitoka katika familia isiyofanya kazi vizuri," anasema. "Sikufundishwa wema na upendo, lakini klabu ilisaidia katika ukuaji wangu kama mtu. Iliunda ubunifu na kipaji changu, kwa hivyo sasa mimi ni mbunifu na ninashukuru klabu ya watoto."
Dhamira pana
Mabinti wa Upendo pia huwahudumia wasio na makazi huko Nizhnyj Tagil, hutembelea makazi ya wenyeji kila siku, na husaidia usafi na ujenzi upya wa majengo ambapo watu wasio na makazi wanaishi. Pia huhudumu katika hospitali ya kifua kikuu ya serikali. "Wagonjwa wengi wa kifua kikuu hawana makazi na huja bila hati," Sr. Antonia anaelezea. "Tunawasaidia kupata hati za kisheria ili wapate manufaa ya kijamii au kuhamia vituo vingine baada ya kuruhusiwa." Masista hutumia gari lao kusafirisha wagonjwa hadi ofisini na kugharamia gharama zote. Mara moja kwa mwezi, hupeleka chakula katika zahanati ya wagonjwa wa kifua kikuu, kama motisha kwa wagonjwa kuja kwa uchunguzi wa kimatibabu wa kawaida. Wanatoa huduma ya kichungaji kwa waumini katika parokia, hufanya katekesi, na mara kadhaa kwa mwaka hufanya mikutano kwa waumini katika hafla na sikukuu mbalimbali.
Usaidizi katika nyakati ngumu
Programu zao za hisani zinahitaji fedha, ambazo wanazipata kupitia ruzuku kutoka Mkoa wa Slovakia wa Vincentians, na pia kutoka kwa michango kutoka kwa watu wa eneo hilo wakati wa ukusanyaji wa chakula wa kila mwaka wa ‘Mfuko wa Mtakatifu Vincent’. “Watu ni wakarimu sana, kwa sababu wanajua chakula kitatumika kwa maskini,” anasema Sr. Antonia huku akitabasamu kwa shukrani. Wanaandaa maonesho kwa hafla mbalimbali kama vile Noeli, Pasaka, na siku ya heshima kwa wazee.
Sr. Vojtecha na Sr. Michaela na watu wasio na makazi
Katika Omsk
AskofuJoseph Werth, SJ, wa Jimbo la Novosibirsk, aliwaalika masista katika jiji la Omsk mnamo 2010. Katika jiji la Siberia, masista wa Vincent hufanya kazi katika Parokia mbili, wakifundisha katekisimu kwa watoto na watu wazima. Pia wanawahudumia watu wasio na makazi na wagonjwa wa kifua kikuu katika Shirika la Upendo la Kikatoliki huko Omsk, huku wakitoa msaada wa kiroho kwa wafanyakazi wa upendo familia, na watoto. "Pamoja na Padre tunakwenda kwenye parokia zinazozunguka, wakati mwingine zaidi ya kilomita 100, mbali," alisema Sr. Antonia.
![]()
Sr. Vojtecha kuwafikishia chakula watu wasio na makazi
Furaha na Mapambano
Sr. Antonia anatafakari kuhusu mapambano ya kina na matumaini ya utulivu ndani ya jamii yake, ambapo hofu, umaskini, na matatizo ya kifamilia yanabaki kuwa changamoto za kila mara. Licha ya idadi ndogo ya Wakatoliki, masista wanamjua kila mtu kibinafsi na wanapata furaha kubwa katika kuona kizazi kikikua, wakiwaona watoto wa wale aliowahi kuwahudumia. Kwa zaidi ya miaka ishirini, misheni ya masista wa Vincentian nchini Urusi imekuwa na mizizi katika matendo madogo ya upendo na uwepo kwa ajili ya misheni iliyoongozwa na upendo wa Mungu.
![]()
Sr. Kaja katika moja ya kituo cha mafunzo na mikutano kwa wafanyakazi katika eneo la upendo
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here