Tafuta

205.12.27 Jumuiya Mtakatifu Egidio. 205.12.27 Jumuiya Mtakatifu Egidio. 

Jumuiya ya Mt.Egidio,Noeli na maskini katika meza inayowakaribisha wote

Watu elfu themanini nchini Italia na laki mbili na hamsini duniani kote walikaa chakula cha mchana mnamo Desemba 25 ili kupata sherehe nzuri zaidi ya mwaka pamoja.Ilikuwa mwaka 1982 wakati meza ya chakula ilipowekwa kwa mara ya kwanza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria huko Trastevere na tangu wakati huo meza hiyo imepanuka hadi kufikia sehemu tofauti za dunia.

Vatican News

Watu elfu themanini nchini Italia na laki mbili na hamsini duniani kote walikaa mezani katika Siku ya Noeli ili kupata sherehe nzuri zaidi ya mwaka pamoja. Wakujitolea walijiunga na wasio na makazi, wazee wanaoishi peke yao, familia zenye uhitaji, wakimbizi waliokuja Italia: wote wakiwa na furaha kuwa pamoja, hata kama walikuwa kutoka asili tofauti na wakiwa na hadithi tofauti, mara nyingi ngumu, nyuma yao. Hii ni Noeli ambayo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio huandaa kila mwaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria huko Trastevere: tafakari ya kile ambacho kimetokea nje ya Roma.

Meza ya kirafiki Jumuiya ya Mtakatifu Egidio
Meza ya kirafiki Jumuiya ya Mtakatifu Egidio   (ANSA)

Tangu 1982, watu wengi zaidi wamekusanyika kuzunguka meza

Meza zilizopambwa kwa ajili ya siku kuu, tabasamu, kukumbatiana, zawadi za kibinafsi na utulivu wa wale wanaohisi kuwa sehemu ya familia. Miongoni mwa wageni kwenye chakula cha mchana pia walikuwa baadhi waliookolewa kutoka kwenye janga la kibinadamu huko Gaza. Kwa karibu saa mbili, walizungumza na kusherehekea kwa kutumia menyu ya kiutamaduni: lasagna, mkate na nyama, dengu, na panettone. Ilikuwa mwaka 1982 wakati meza ya sherehe ilipowekwa kwa mara ya kwanza katika Basilika ya Mtakatifu Maria huko Trastevere, na tangu wakati huo, meza hiyo hiyo imepanuka hadi kufikia sehemu tofauti za dunia.

Daima na wale wanaohitaji

"Noeli hii," alisema Andrea Riccardi, mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambaye alikuwepo kwenye chakula cha mchana, "hakuna mtu asiyejulikana, lakini kila mtu anajulikana, katika familia ambayo haimsahau mtu yeyote. Kwa wale ambao hawana sauti, kwa wale ambao hawana nyumba, kukusanyika hapa pamoja huimarisha matumaini na ni ujumbe wa amani ambao ulimwengu unahitaji leo." Kwa sababu, kama rais wa Jumuiya, Marco Impagliazzo, alivyosema, "siku hii inaambatana na kila siku ya mwaka ambapo Mtakatifu Egidio inasimama kando ya wale wanaohitaji, wale wanaoishi mitaani, lakini pia wale kutoka mbali wanaohitaji kukaribishwa na kuunganishwa."

Meza ya kirafiki kwa maskini
Meza ya kirafiki kwa maskini   (ANSA)

Kila mmoja akiwa na hadithi tofauti

Miongoni mwa wageni wengi, waliotambulishwa na kuhani wa parokia ya Mtakatifu Maria huko Trastevere,Padre Marco Gnavi, alikuwa Sofia, 92, ambaye amekuwa akihudhuria chakula cha mchana cha Noeli kwa miaka 30 na ambaye alishuhudia "upendo wa jumuiya hii, akiiwasilisha kwenu nyote." Au kama Nidal mdogo, ambaye anatoka Gaza na ametumbuiza  wimbo wa chekechea wa Gianni Rodari ambao anaurudia kwa imani kubwa. Pia walikuwepo watu wengine kutoka nchi zilizojaa migogoro, kama vile Sudan, Somalia, na Afghanistan, watu ambao hapo awali walikuwa hawana makazi ambao sasa wamepata makazi, na Anoir, ambaye asili yake ni Moroko, ambaye hivi karibuni alipata uraia wa Italia. "Pamoja," alihitimisha Padre Gnavi, "tulisherehekea Noeli, lakini pia mustakabali wenye furaha zaidi kwa kila mtu, kwa mji wenye utu zaidi na maisha yaliyojaa ndoto."

Meza ya kirafiki na maskini
Meza ya kirafiki na maskini   (ANSA)

Chakula cha mchana cha Jumuiya yote ya Mtakatifu Egidio kinawezekana kutokana na usaidizi wa bure wa watu wa kujitolea na shirika upendo(linalofanya kazi, Desemba 27). Mipango mingi pia imepangwa kwa siku zijazo, katika kipiondi chote cha Noeli pamoja na usambazaji wa milo na zawadi pia katika magereza. Hii ilifanyika Desemba 27,  Siku vifurushi huko Roma, katika magereza ya Rebibbia na Regina Coeli.

27 Desemba 2025, 15:04