Huduma ya Kichungaji ya Uhamaji wa Binadamu:chanzo cha matumaini!
Yamile López na Sr. Christine Masivo CPS – Vatican.
“Wale wote wanaohama wanatakiwa kupendana kwa sababu sisi sote ni ndugu, sote ni viumbe hai wenye kasoro au na wema, lakini sote ni sawa,” alijibu Camilo alipotakiwa kutafakari jinsi maisha yake yalivyokuwa akiwa mhamiaji. Na hivyo, kwa kifupi, alifafanua jinsi uhamiaji unapaswa kueleweka, utume ambao masista Wafransiskani wa Maria Asiye na dhambi wanaitikia kupitia huduma ya kichungaji ya uhamaji wa binadamu. Miaka 30 iliyopita, jimbo la Piedras Negras, lililoko kwenye mpaka wa Mexico na Marekani, lilianzisha hosteli kwa ajili ya raia waliofukuzwa kutoka nchi nyingine. Wakati huu kwa sababu ya uhitaji uliopo, imebadilika na kuwa Nyumba ya Wahamiaji wa Mpakani Yenye Heshima, ikizingatia kuwapa wale wenye matumaini ya kujenga maisha bora ya baadaye.
![]()
Kituo henye hadhi cha wahamiaji,ambacho Watawa wanatoa faraja kwao.
Dhamira ni kufanya kazi pale ambapo kuna uhitaji mkubwa zaidi
Mara ya kwanza Sr. Isabel kufanya kazi na wahamiaji alikuwa kwenye Mkutano wa Kidini wa El Salvador (CONFRES), kazi ambayo ilizingatia zaidi hatari za uhamiaji. Kisha alisafiri safari kupitia njia ya wahamiaji na kukaa katika makao manane kuanzia Guatemala hadi Ixtepec, nchini Mexico. Mnamo 2018, alisafiri kwenda Bogotá, na pamoja na watawa wengine, walitoa usaidizi maalum kwa wahamiaji wa Venezuela, ambao walikuwa wakifika kwa wingi nchini Colombia wakati huo.
"Nilikwenda kwenye kituo cha Salitre kila asubuhi ili kuwakaribisha wahamiaji wote wa Venezuela waliofika, kuwaongoza, kuwapa maji safi na mkate, kusoma neno la Mungu pamoja nao, kufanya sherehe, na pia kuwaelekeza wasichana kwa mapadre wa Scalabrini," alisema mtawa huyo aliyeguswa na hali ya wasichana hao. Aliongeza kusema kwamba, "Wanawake wenye haya waliofika hapo, walijua kwamba walikuwa wameletwa na kununuliwa kufanya kazi ya ukahaba Bogotá. Kwa hivyo tulichukua fursa hiyo kuwahamasisha kujua kwamba hiyo ni biashara haramu ya binadamu.” Miezi michache baadaye, aliondoka kwenda Mexico pamoja na watawa wawili.
![]()
Ingawa idadi ya wahamiaji wakati mwingine huzidi uwezo wa kituo hicho,sisi hujaribu kila wakati kutoa msaada unaohitajika kwa njia fulani.
Mshikamano hufufua matumaini
Katika kipindi hicho, masista hao walisema historia nyingi za uchungu wakiwa wanafanya utume wao na wahamiaji, ikiwemo waliokuwa wakitumikia na machungu yote waliyoyapata wakati wa janga la Uviko-19. Piedras Negras ni mahali pa watu wema, waliojitolea na wenye ushirikiano mwema. Katika kipindi hicho, Parokia pia walijiunga nasi katika kuwahudumia wahamiaji, kuwapa chakula na kuendelea kuwasaidia," Sr Isabel alisisitiza. Ni kupitia maongozi ya Mungu tu, ndipo alipata maelezo wakati anafikiria kuhusu maana ya kuwatunza karibu wahamiaji elfu moja kila siku. Kulikuwa na chakula, godoro, blanketi, matibabu, na faraja ya kiroho kwa kila mtu; kwa hilo, anawashukuru wafanyakazi wengi wa kujitolea, Parokia, Madaktari Wasio na Mipaka, na Shirika la Wafransiskani kwa ajili ya Wahamiaji.
Kama mtawa, sala za kila siku na kupitia kwa maombezi ya Wafransisko humsaidia kukabiliana na uchungu wa wahamiaji. Hali kama zile za wanawake wajawazito walioazimia kuvuka mto huo kwa kudanganywa kwamba, ikiwa mtoto atazaliwa Marekani, atapata uraia. Wengine wakiwa waathiriwa wa ubakaji au utekaji nyara, ambao waliuzwa na kufanikiwa kujikomboa hadi kufikia kaskazini. Wanawakumbuka wote, na wengi humpigia simu kumshukuru kwa sababu wataweza kutimiza ndoto zao.
![]()
Kwa njia ya uchungaji wa kibidamu,Watawa Wafransiskani wanaishi karama ya kimisionari ya Mwanzilishi wao,Mwenyeheri Maria Caridad Brader
Uhamiaji na Mwenyeheri Maria Caridad Brader
Camilo aliamua kuondoka katika nchi yake ili kutafuta maisha bora zaidi kwa ajili yake, mama yake, na dada yake. "Ujumbe ninaotaka kuwaachia akina mama wote (akimaanisha watawa) ni kwamba wasifeli katika kazi hii nzuri na kubwa wanayofanya na wahamiaji wote, sitasahau siku ambayo uhuru wa nchi yangu uliadhimishwa, walinisherehekea kwa chakula maalum cha mchana, na bendera na vyakula vya kawaida na maelezo mengi." Uhamiaji ni ukweli unaoitikiwa na huduma ya kindugu na sinodi. Mwanzilishi wa Shirika lake, Mwenyeheri Maria Caridad Brader, alikubali maisha ya kimisionari katika wakati wake na akaiacha nchi yake ya Uswisi ili kuwafanyia kazi watu ambao, mwishoni mwa karne ya 19, walisahaulika katika Ecuador na Kolombia.
"Nafikiri Mama Caridad angeanzisha nyumba ambayo watawa wangeishi na kuhudumu katika maeneo yote ya mpakani, kwa sababu ndivyo alivyofanya. Katika historia, tunayo baadhi ya mifano ambayo, kulipokuwa na hali ya vita, shule yake ilifungwa na kugeuzwa hospitali, na Masista wakawa wauguzi wa kuhudumia majeruhi." Alihitimisha, "Ni roho hii ya umisionari ya Mama Caridad ambayo inatutia moyo kila siku huko Piedras Negras."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.