Tafuta

Askofu Mkuu Fulgence Muteba Mugalu, wa Lubumbashi(DRC). Askofu Mkuu Fulgence Muteba Mugalu, wa Lubumbashi(DRC). 

Askofu mkuu wa DRC akaribisha wito wa Papa wa kukomesha silaha

Askofu Mkuu Fulgence Muteba wa Lubumbashi na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Congo(CENCO),aliakisi ujumbe wa Papa Leo XIV wa Amani na ombi kuhusu kusitisha silaha hili kudumisha amani ulivyopokelewa nchini humo na pia kuzungumzia juu ya uzoefu wa Jubilei ya Matumaini katika jimbo kuu lake na matashi yake mema kwa mwaka ujao 2026.

Na Jean-Paul Kamba, SJ, - Vatican.

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi yenye miongo kadhaa ya migogoro na ukosefu wa utulivu, Ujumbe  wa Papa Leo XIV wa Siku ya Amani duniani kwa mwaka 2026 na wito wa "kusitisha silaha" umepata mwitikio na kupokelewa kwa kina. Hayo yaliwasilishwa na Askofu Mkuu Fulgence Muteba wa Lubumbashi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Congo (CENCO), akibainisha jinsi ulivyopokelewa kwa "furaha na shukrani nyingi" kwa sababu, dhana ya amani ni ukweli kwetu ambao tunautamani sana."

Akizungumza na Vatican News, Askofu Mkuu alisisitiza wigo kwa jumla wa maneno ya Baba Mtakatifu, ambayo yanaenea mbali zaidi ya mipaka ya Afrika.  Kwake binafasi anaamini kwamba, kwa kuzungumza mara kwa mara kuhusu amani, Papa anagusia "jambo muhimu sana ambalo linahusu si bara letu tu, bali ulimwengu mzima." Askofu Mkuu Muteba alisema jinsi ambavyo ametiwa moyo hasa na mwelekeo mpya wa mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii na kuendelea kwa umuhimu wa Waraka wa Laudato si'.  "Mustakabali wa dunia unategemea kulinda mazingira na kupambana na uharibifu wa kila kitu kinachotuzunguka", alionya.

Mwaka wa Matumaini wa Jubilei mjini Lubumbashi

Jubilei ya Matumaini inapokaribia mwisho, Askofu Mkuu alieleza jinsi ambavyo jimbo kuu lake liliishi mwaka huo “kwa imani kubwa,” ulioainishwa na kujitolea kwa nguvu kutoka kwa Wakristo, walimu, harakati za Kikatoliki, na wengineo. Huko Lubumbashi, jumuiya ziliishi nje ya safari ya jubilei kwa umakini mkubwa, zikiimarisha imani yao na kuamsha ari ya kimisionari, alibanisha.

Mwaka mpya wa matumaini

Akiendelea na  wito wa Papa Leo XIV , Askofu Mkuu Muteba alieleza matashi yake mema "kwamba mwaka ujao uwe na uhalisia na imani. Kwa kuzingatia “hali zenye utata” na ukosefu wa amani ya kweli, tumaini ni jambo la lazima. “Tunahitaji tumaini hili ili kuwasha upya imani ya waamini,” alisema, huku akisali kwa ajili ya “amani na matumaini zaidi.” Askofu Mkuu pia alisisitiza umuhimu wa sinodi kama njia ya ushirika. Alikumbuka jinsi “sinodi huturuhusu kuimarisha maisha yetu pamoja, zaidi ya vizuizi vya lugha, kiufundi, na changamoto zinginezo.”

Noeli, Umwilisho, hadhi ya mwanadamu na wito wa haraka wa amani

Askofu Mkuu Muteba alieleza kuwa katika mahubiri yake kwa ajili ya Misa ya Noeli, alisisitiza kuwa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu si kumbukumbu tu, bali ni uzoefu hai wa imani kumkaribisha Kristo, kumwabudu, na kumruhusu azaliwe ndani ya mioyo yetu. Kwa Askofu mkuu, fumbo la Umwilisho linafunua upendo wa Mungu usio na kikomo na heshima isiyoweza kuondolewa ya kila mwanadamu, ambayo ilimfanya kukuza mada kuu tatu. Kwanza, Noeli  inaakisi hadhi ya mwanadamu (Ubuntu): mwanadamu ana thamani zaidi kuliko utajiri wowote. Kwa maana hiyo, Askofu Mkuu Muteba alikemea unyonyaji usio wa haki wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akifananisha na aina mpya ya ukoloni wa kiuchumi. Zaidi ya hayo, anaomba kuheshimiwa kwa watu wa Kongo, kwa amani, na kwa ajili ya maendeleo shirikishi.

Pili, Mtoto aliyeko horini ni ishara inayotaka kuheshimiwa na kulindwa utu wa watoto wakiwemo waishio mitaani. Askofu Mkuu wa Lubumbashi analaani vikali ghasia, utekaji nyara, na uandikishaji wa kulazimishwa unaowakabili. Hatimaye, Yesu ndiye “Mwana-Mfalme wa Amani.” Katika kukabiliwa na vita ambavyo vimeharibu nchi yake kwa miongo kadhaa, Askofu Mkuu Muteba anatoa wito wa kukomesha ghasia mara moja na mazungumzo, upatanisho na msamaha. Anatoa onyo kwamba kukataa amani ni kukataa mpango wa Mungu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

30 Desemba 2025, 11:56