Zambia:Watawa 16 wa Mashirika wahitimimu katika Kituo cha Kimataifa cha Utafiti,Kalundu
Na Paul Samasumo – Vatican.
Watawa 16 kutoka Mashirika tofauti na nchi mbali mbali za Afrika hivi karibuni walihitimisha kozi ya uongozi na malezi yenye mabadiliko, katika Kituo cha Mafunzo ya Kimataifa cha utafiti kilichoko Kalundu nchini Zambia. Mgeni rasmi, alikuwa Sr Valeria Kabaso wa Shirika la Mtakatifu Charles Borromeo na Rais wa Shirikisho la Mashirika ya Kitawa nchini Zambia(ZAS,)ambaye aliwapongeza wahitimu, akiwasihi kutumika kama miale ya matumaini katika jamii: "Kuweni mabalozi wa matumaini kwa Kituo cha Mafunzo cha Kalundu. Kuwa tumaini ambalo ulimwengu unasubiri," alisema.
Muktadha wa kiutamaduni na kidijitali
Sr Kabaso alisisitiza umuhimu wa malezi kamili kwa wanawake watawa wa leo hii. "Mifumo ya hivi karibuni ya malezi inazingatia kuunganisha nyanja za kibinadamu, kiroho, kiakili, na kichungaji. Sista aliyefundwa vizuri leo si tu kwamba anasali bali pia ni mwerevu kihisia, anafahamu kijamii, na ana uwezo wa kuongoza katika muktadha wa kiutamaduni na kidijitali," alielezea. Akitafakari umuhimu wa mahafali haya ya 45, Sr Mishael Manianga, Nwabashirika la Roho Mtakatifu na Mkurugenzi wa Kituo hicho, alitoa shukrani kwa Balozi wa Vatican kwa kusherehekea Misa ya mahafali na kuheshimu tukio hilo kwa uwepo wake. Kuhudhuria kwake, alisema, “kulikuwa ushuhuda wa ukaribu wa Baba Mtakatifu Papa Leo XIV na wanawake watawa.”
"Mheshimiwa Askofu Mkuu Gian Luca Perici, Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi, tunaheshimiwa sana na uwepo wako. Ziara yako leo inatukumbusha ushirika wetu na Kanisa la Ulimwengu na Baba Mtakatifu. Kupitia kwako, tunahisi msaada na ukaribu wa Papa Leo XIV, ambaye anatufundisha kwamba wanawake waliowekwa wakfu ni miale ya matumaini—waliojitolea kuunda mioyo, kuhamasisha mawazo, na kukuza hadhi ya utu," alisema Sr Mishael.
Kuhudumia Bara la Afrika
Akizungumza na Vatican News, Sr Felista Nyirongo, Msimamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Utafiti cha Kalundu na Sista wa Shirika la Upendo, alielezea dhamira ya kituo hicho. Alikielezea kama taasisi isiyo ya faida inayomilikiwa na Shirikisho la Umoja wa Watawa nchini Zambia(ZAS,) iliyojitolea kuunda viongozi wa kidini wanawake waliojumuishwa na waamini walei na walezi. Kwa miaka mingi, mpango wa uongozi na malezi wa miezi kumi na moja umewavutia masista kutoka nchi nyingi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Zambia, Sudan Kusini, Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Lesotho, Liberia, Tanzania, Zimbabwe, Eritrea, Uganda, Ghana, Msumbiji, Angola, Malawi, na Namibia.
Baadhi ya wahitimu katika kituo cha mafunzo cha Kalundu (©Zambia Association of Sisterhoods)
Mahafali ya mwaka huu si tu kwamba yanaashiria hatua muhimu kwa wanawake watawa wa Kiafrika lakini pia yanaashiria kujitolea kuendelea kuwahudumia na kuwawezesha wanawake wa Kiafrika wenye ujuzi unaofaa kwa ulimwengu wa leo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here