Tafuta

Dhori , sherehe ya Mama Maria, India Dhori , sherehe ya Mama Maria, India 

Wakristo wa Kalkuta wazindua mpango wa mazishi yenye heshima kwa wote

Jumuiya ya Wakristo huko Kalkuta,nchini India,yazindua mpango mpya uliojitolea kumpatia kila mtu,bila kujali hali yake ya kiuchumi,mazishi yenye heshima inayostahili.

Na Christine Masivo, CPS. - Vatican.

Katika kumbukumbu ya Siku ya Marehemu wote,  itadumu kwa muda mrefu zaidi ya siku moja  kwa Jumuiya ya  Wakristo huko Kalkuta, nchini India. Na kama ilivyo kwa wakristo wakatoliki ambao kwa mwezi Novemba huwakumbuka wapendwa. Kwa uzinduzi wa mpango wa "Shamman Samadhi" (mazishi yenye heshima), wanaendelea kuwapa watu heshima wakati wa kifo chao. Kulingana na Bodi ya Mazishi ya Kikristo ya Kalkuta, mpango huu unakusudiwa kuwa, "ishara ya huruma na ujumuishaji", na uliwaleta pamoja wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo.

Kila mmoja anastahili mazishi yenye heshima

Bodi ya Mazishi ya Kikristo ilielezea lengo la mpango wa "Shamman Samadhi" ni kuhakikisha kwamba kila mtu, bila kujali hali yake ya kiuchumi na kijamii, anapewa mazishi yenye heshima na ya bure. Kulingana na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari (Fides), sehemu ya makaburi ya kihistoria ya Kikristo ya Kalkuta huko Mullickbazar, kando ya Barabara ya mzunguko wa chini  ilitengwa kwa ajili ya familia ambazo haziwezi kumudu gharama za mazishi. Eneo hilo pia litakuwa wazi kwa ajili ya kupokea miili ya wale waliofariki wakiwa wameachwa, kama vile waliotengwa, bila jamaa au wapendwa wa kuwatunza.

Utume wa kijamii

Shirika la kitawa lililoanzishwa na Mtakatifu Teresa wa Wamisionari wa upendo pia inahusika katika mpango huu kwani karama yao pia inajumuisha kuwasaidia wanaoaga na walioachwa, Shirika hili lilieleza pia kwamba mpango wa "Shamman Samadhi" umekuza utume wao wa huruma kwani inasisitiza wafu kupata mazishi yenye heshima na amani. Wamisionari wa upendo pia wanahusika katika mpango huu kwani dhamira yao pia ina maana ya kuwasaidia wanaokufa na walioachwa, (AFP). Serikali ya jiji la Kalkuta ilikaribisha mradi huo na kusema itachangia kutoka kwa mfuko wake wa maendeleo. Eneo la makaburi yaliyotengwa kwa ajili ya mpango huu limegawanywa katika makundi, moja kwa watu wazima na jingine kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitatu.

Bodi ya Mazishi ya Kikristo imechukua jukumu la kutunza makaburi na imesisitiza kujitolea kuwahudumia wakazi walio katika mazingira magumu zaidi ya Kalkuta "kwa huruma, heshima, na uwajibikaji wa kiraia". Bodi pia ilitangaza kwamba mahali pengine pa kuzikwa patawekwa katika Makaburi ya Tollygunge mapema mwaka wa 2026, na kupanua mpango huo. Zaidi ya hayo, Bodi ya Mazishi ya Kikristo iliomba serikali ya jiji igawanye ardhi kwa ajili ya ujenzi wa makaburi mapya ya Kikristo kwani maeneo ya sasa yanaanzia enzi ya Uingereza na yamejaa kabisa.

Marehemu wote Kalkuta
04 Novemba 2025, 17:26