Masisita Wakarmeli:"maisha ni safari na siyo mwisho wa safari"
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tumekuwa na msemo wa Wahenga wetu waliosema kuwa: “Kifo cha Wengi ni Harusi." Hakika, sura hii ya harusi ya wanawali wanne walionekana wakiwa katika majeneza manne meupe mbele ya Madhabahu kwa ajili ya Misa ya Mazishi ya Masista hawa 4, baada ya kifo cha ghafla cha ajali iliyotokea Jumatatu jioni tarehe 15 Septemba 2025, kwa gari lao kugongana na lori uso kwa uso kusababisha vifo vitano aliwemo Dreva na na nusura Sista amnaye anapambana kati ya kifo na maisha. Msiba ambao umeleta simanzi kuu kwa Kanisa la Tanzania, Kanisa la Kenya, Kanisa la Italia na kwa hiyo Kanisa lote la Ulimwengu.
Masisita hawa walikuwa ni Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, ambao ni Mama Mkuu wa Shirika Sr Lilian Kapongo, Mshauri na Katibu Mkuu Sr Maria Nerina De Simone, wa Italia, Washauri wa Provinsi ya Afrika Mashariki, Sr Damaris Matheka na Sr Stellamaris Muthini, jina la dreva ni Bonifasi, wakati Sr Paulina Crisante Mipata, hali yake ni mbaya akiwa amelazwa Hospitali ya Bugando, Mwanza Tanzania. Tarehe 18 Septemba, miili yao ililetwa mjini Dar Es Salaam, katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, ikitokea Mwanza na kufikishwa katika Nyumba Mama ya Shirika huko Boko, Dar es Salaam kwa Maombolezo na mkesha.
Kwa hiyo, Ijumaa tarehe 19 Septemba 2025, Waamini wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Bagamoyo na Kanisa zima la Ulimwengu liliungana kwa pamoja kuwaombea Masista hao katika ibada ya Misa Takatifu katika Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja Boko, Jimbo Katoliki Bagamoyo. Misa hiyo iliongozwa na Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi OFM Cap. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akishirikiana na Maaskofu wengine sita wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC): Askofu Wolfgang Pisa OFMCap.Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo la Lindi, Askofu Eusebius Nzigilwa, Makamu Rais Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda, Askofu Titus Mdoe wa Jimbo Katoliki Mtwara, Askofu Thomas Kiangio wa Jimbo Katoliki Tanga, Askofu Christopher Ndizeye Nkoronko wa Jimbo Katoliki Kahama pamoja na Askofu wa Jimbo mwenyeji la Bagamoyo, Askofu Stephano Lameck Musomba OSA.
Mara bada ya misa hiyo kati ya Masista wanne, Watatu raia wa Tanzania na Kenya walizikwa katika Bustan iliyopo katika Nyumba Mama ya Shirika la Wakarmeli huko Boko, Dar es Salaam - Tanzania, mbele ya uwepo wa wazazi na ndugu zao, isipokuwa Sr Nerina, ambaye ni raia wa Italia na Katibu Mkuu wa Shirika la Wakarmeli atasafirishwa ili kuzikwa katika Nyumba Mama ya Shirika Duniani, huko Santa Marinella, Italia. Mahubiri yalitolewa na Askofu wa Jimbo la Bagamoyo.
Idhaa ya Kuswahili inachapisha mahubiri
Taifa la Mungu, Tumsifu Yesu Kristo. Mungu ni mwema…! Kila wakati…..! Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, siku hizi na wakati huu ni mzito sana, ni wakati wa huzuni, ni wakati wa simanzi kubwa. Tunapo wasindikiza dada zetu hawa kwa wale ambao walionana nao, siku chache zilizo pita watayaona hayo kwa undani zaidi, hawajaumwa, imetokea hivi na tupo hapa tunawaaga. Ni wale ambao walitimiza majukumu yao vizuri, na leo hii tunawaaga, tunawasindikiza, wamekwenda kwa Baba. Huzuni hii, na simanzi hii, inatukumbusha sana maneno ya mwanafalsafa mmoja wa kimarekani. Anaitwa Ralph Waldo Emerson, huyo aliweza kuwa na usemi, unaosema: “maisha ni safari na siyo mwisho wa safari.” Maana yake kuweza kuangalia kwa umakini sana safari hii na kuweza kujiunda katika safari hiyo, tunajua kwamba tunaanza safari ya maisha kwa kuzaliwa kwetu.
Pengine hatujui chochote, lakini baadaye tunakua, tunajifunza na tunapata elimu mbali mbali. Hali hii vile vile inatuongoza kutuonyesha kwamba Mungu yuko kati yetu, Mungu yuko nasi, na katika safari hiyo, tunahitaji kumtambua, tunahitaji kutambua mapenzi yake, na tunahitaji kuyafuata na kuishi inavyo tupasa kama watoto wake. Ni yeye aliye tuumba, na tunatakiwa kutafuta elimu yake. Ili tuweze kutafuta vizuri elimu yake na kumwelewa vizuri na kuyatambua mapenzi yake, hatuna budi kila wakati kutakatifuza chanzo cha elimu yetu, fikra zetu, akili zetu, ili zimtambue vizuri Mungu wetu, lakini vile vile kutakatifuza utashi wetu, kutambua kwamba Mungu ni mkuu, Mungu anastahili sifa zote na anastahili kuchukua nafasi ya kwanza katika maisha yetu, na vile vile kutakatifuza mioyo yetu chanza cha upendo. Mungu ni upendo ili upendo wetu tulio nao uendane na Mungu ambaye ni upendo na kuondoa ubinafsi katika maisha yetu, kwa sababu hiyo, safari hii ya maisha, ni safari ya kujifunza, unaweza usijue, na unaweza usielimike na ukajua chochote, ni safari ya kujifunza, kujishughulisha, kwa namna mbali mbali katika maisha yetu. Ni safari ya kubadilika kutoka katika yale sikuwa najua, kutoka katika kuto kuelewa kwangu, au nikawa katika sehemu ambayo siyo nzuri, ambayo siyo ya kumpendeza Mungu niko katika dhambi, niweze kuwa mcha Mungu, niweze kuishi inavyo ni pasa kama mtoto wake.
Ni safari ya kujitambua sisi wenyewe, mapungufu yetu na vile vile uwezo wetu, na kumuona Mungu ndiye anaweza yote. Na si kujitambua kwamba hatuna maswali, hatuna majibu ya maswali yote ya dunia hii. Tunahitaji msaada wa watu wengine ambao watafanya tukue vizuri kiroho na kimwili. Tuweze kuonekana ni binadamu na katika ubinadamu wetu, tuwaone wenzetu vile vile kama sura na mfano wake mwenyezi Mungu, na kwa sabu hiyo, hili linahitaji sana unyenyekevu. Ununyekevu unaotupasa na kutuongoza kusikiliza, na si kusikiliza tu hata kutii yale tunayo ambiwa na ushauri mbalimbali. Lakini vile vile katika safari, tunakutana na mengi, tunakumbana na mengi, ni sawa na gari ambalo liko barabarani, likifika sehemu, litaona taa nyekundu, inaashiria kwamba inabidi kusimama. Na baadaye utaruhusiwa kuondoka, kwanza simama, kwasababu hayo maisha ni kama safari, yanahitaji vile vile uvumilivu. Na tunapokutana na wengine, yanahitaji vile vile uvumilivu. Na tunapokutana na wengine yanahitaji tuwe na msamaha, tuweze kufanya upatanisho, na tunahitaji muda wa utulivu, katika kelele mbalimbali za Ulimwengu huu, ili tuweze kuwa na nafasi ya kuongea na Mungu wetu, tuweze kuwa na tafakari ya ndani hata juu yetu sisi wenyewe, jinsi tulivyo umbwa kama wanadamu na haya yote yanatuonyesha kabisa kwamba bila kumuweka Mungu katika maisha yetu hatuna maana sisi, na umaana huu unatokana tu na Mungu kwamba anachukua nafasi ya kwanza kwetu
Katika masomo yetu tuliyo sikia, katika somo la kwanza, tumesikia neno “mtu mwenye haki”. Huyo mtu mwenye haki ni nani? Huyo mtu mwenye haki ni mtu wa imani, ni mtu anayetambua neema ya Mungu. Ni mtu anaye tambua msamaha wa Mungu katika maisha yake, na kwasababu kuu hiyo amejaa shukrani kwa Mungu kwasababu kila mara anaona ukuu wake katika yote anayo yatenda na si mtu wa majivuno kwa yale aliyo fanikiwa, ila ni yule ambaye anamshukuru Mungu zaidi kwa kumwinua na anatumia yale aliyo faulu kuyafanya au vipaji alivyonavyo kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu, huyu vile vile ndiye anaye angalia mahitaji ya wengine, na kwasababu hiyo ni mkarimu kwa masikini na wahitaji vile vile, na katika hao anamuona Yesu anayeteseka.
Na kwasabu hiyo, ndiyo maana yuko karibu nao na kuwa mkarimu kwao, na yuko tayari vile vile kuwaongoza wengine wafuate njia ya kumwelekea Mungu. Ni yeye ambaye anajitoa sadaka iliyo hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu. Ni yule ambaye hafuati mkumbo tu, hafuati yale ambayo ulimwengu anaoishi unamwonyesha. Si mtu wakufuata mazoea, yule ambaye kila mara anamuona Mungu katika maisha yake, ata unapo soma Warumi: (12; 1-2) “Sadaka iliyo hai takatifu na ya kumpendeza mungu”. Kifo chake kinakuwa kama sadaka ya kuteketezwa, inayo kubaliwa na kupendezwa na Mungu, kwababu hiyo, sadaka lazima iteketezwe, hasa tunapo elekea katika kitabu cha Mwanzo 4;1…na kuendelea, tunaona sadaka ya Kaini na Abeli. Kaini alitoa sadaka yake na Abeli naye alitoa sadaka yake, na vyote hivi, viliteketezwa lakini sadaka ya Abeli ilipokelewa na Kaini akawa na wivu, ilipokelewa ya Abeli, kwasababu alikuwa ni mtu mwenye haki,ndiyo maana iliweza kupokelewa.
Kaini aliingia katika sadaka akiwa na makando kando yake na akashindwa kumtolea Mungu kile kinachotakiwa machoni pake naona vyote viliteketea, lakini Mungu alipendezwa na sadaka ya Abeli na ndiyo maana wanasema kifo cha mwenye haki ni kama sadaka ya kuteketezwa, yenye kupokelewa na Mungu na ambayo inampendeza Mungu. Ndiyo maana katika somo la kwanza tunasikia hilo, kwamba wenye haki wamo miknoni mwa Mungu na wala taabu yoyote haitawapata na kwaupande mwingine tunaona kundi la wajinga ambao pengine wamejaa kuzomea, kuangalia na kuyaona yote haya kwamba wamepotea hawa, lakini Mungu amewapokea wamo mikononi mwake, na katika hilo, ndiyo maana somo linatuonyesha vile vile mafao ya mbinguni. Tunaona mafao ya duniani hapa, wakati mwingine unaweza kaenda usipate, lakini mafao ya mbinguni, ni mafao ambayo hayabadiliki, hayaishi yanaendelea kuwepo.
Katika Somo la Kwanza tumeyasikia hayo na katika somo la pili tumesikia hivi. Ni kukaa na Mungu katika upendo milele yote, ni kuwa na amani mbinguni, na chini ya ulinzi wa Mungu milele yote, nikutokufa, na katika kutokufa, tunapo lichukulia hili, kama tulivyo sikia katika wasifu,wa dada zetu hawa, wanne hapa, tumeona yote waliyo tenda, tumeona kazi zao njema sana walizo zifanya katika shirika na katika jamii yetu. Na kwasabu hiyo, wapo vichwani mwetu, wapo katika akili yetu, tunawakumbuka. Kwa kutokufa, kuna weza kuwa na sehemu mbili zote, moja kutokufa Mungu amewapokea, watadumu milele naye lakini kutokufa sisi hawatapotea katika kumbu kumbu zetu. Kwa sababu tunayaona matendo yao, tunaona alama zilizowekwa na wao kwetu. Kwa sababu hiyo tunawakumbuka muda wote na tutaendelea kuwakumbuka. Na haya ndio yanayo takiwa katika mtu yanayo takiwa kwa wale wanao tafuta haki ili waweze kuwa watu wenye haki, wakumbukwe kwa yale yale waliyo ya fanya mazuri ya kumpendeza Mungu na kwasababu hiyo kifo chao kama sadaka ya kuteketezwa, inayo mpendeza Mungu, inaonekana hawaonekani. Wamepoteza maisha yao ya duniani hapa, lakini wapo mbinguni na sisi tunawakumbuka kwa akili zetu kwa yale ambayo wametenda na wameyafanya kwa ajili ya shirika, ndiyo maana hatutaweza kusahau. Kutokufa kunaweza kumaanisha vile vile kutokusahau Yale aliyotenda yameweka alama za kudumu, katika familia zetu, katika shirika, na katika yote na ndiyo maana akawa ni mfano kwetu, kwa yale aliyo ya tenda. Na vile vile tunu nyingine au fao lingine la mbinguni ni Utukufu wa milele ambao wataupata pamoja na Mungu.
Na tunaona katika Somo la Pili tunakumbushwa vile vile kwamba Mungu akiwa upande wetu hakuna mbaye anaweza kufanya chochoote, lakini, hili tutambue kwamba Mungu yuko upande wetu, lazima tufanye kazi na tutambue hilo, na tukitambua Mungu yuko upande wetu, tutamshikiria na tutakaa naye. Tunajua kwamba katika maisha yetu, kuweza kuwa na furaha ya kweli ni kuwa na Mungu kwasababu hakuna anayeweza kutunyanganya Mungu, lakini vitu vingine vinanyanganywa, na ndiyo maana tunaposema ni safari, unawezakusema nataka nikajenge nyumba nimejenga ndiyo mwisho, hapana, bado unana kwamba inaendelea mbele na unaangalia mbele zaidi, na mbele yako unamuona Mungu zaidi kuliko yote kwa utukufu wa milele, zota hizi ni mafao ya mbinguni kama tulivyo ambiwa. Katika somo la kwanza na katika somo la pili. Na kama tulivyo ambawa katika masomo hayo, hakuna kitakacho tutenga na upenda wa kristo kwasababu tumsekumbatia huyu, tuponaye huyu, na kwasababu hatuna majivuno, hatuwezi tukajidai katika dunia hii, kwa sababu wakati wowote tunaweza tukaondoka na tukaenda kwake, lakini ni lazima tutafute haki.
Katika Injili ya Mathayo (6, 33), Yesu anasema: “Tafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake, mengine mtapewa kwa ziada.” Katika Injili tuliyoisikia, kutoka Matahayo Yesu anaanza na shukrani “nashukuru Mungu Baba Muumba wa Mbingu na Nchi, mambo hayo umewaficha wenye akili na hekima, wenye majivuno, wale ambao wanaonekana kama wamesoma, wanaonekana kama wanaelewa kila kitu lakini ukawafunulia watoto wachanga, wenye, unyenyekevu,” wale ambao wanaona kwamba Mungu ni muhimu katika maisha yao, na ndiyo maana wanamsikiliza kwanza yeye na badaye kutafuta haki, tunajua kwamba inapatikana katika neema ya Mungu mwenyewe, na vile vile katika msamaha wa Mungu mwenyewe, kama tunivyosikia vile vile katika somo la kwanza limeeleza hivyo lakini katika injili hii mwaliko wa yesu njooni kwangu, njooni nyote mnao elemewa na mizigo nami nitawapunzisha.
Mjifunze kwangu, fuateni yale ambayo ninawaelekeza na kati ya maelekezo aliyotuambia ni amri ya mapendo, “Pendaneni kama nilivyo wapenda ninyi”. katika hili, ninge toa tu mfano mdogo. Kuna mtu mmoja alikua na kiburi, alikuwa tajiri lakini alikuwa na kila kitu na alikuwa na dharau, ilitokea siku mmoja tu akapita mochwari na siku hiyo, mochwari hiyo ilionekana ni ndogo kwa sababu kulikuwa na maiti nyingi,akaona watu walivyo lala katika sakafu, hawawezi wakajisaidia wenyewe wakajishika wakafanya nini….! ila wamelala pale na wakati anaingia, anakutana na maneno kwamba “Sisi, siku zilizo pita tulikuwa kama wewe”, wakati anaingia pale, ameangalia pale, akiwa ameduwaa tu, amepatwa na butwaa, anapo taka kutoka, anakutana na maneno, kwamba “Si mda mfupi utakuwa kama sisi” akaenda nyumbani na alivyokuwa kule nyumbani, akaona akae chini kwanza, afanye kama “reform” katika reform hiyo aende katika njia zake zote za maisha, aangalie mahusiano yake na watu, aangaliye mahusiano yake na Mungu, na katika hilo, alijiulize maswali mengi.
Hivi mimi nina maana gani katika dunia hii, mpaka niweze kuwadharau wengine, mpaka ni weze kuwatukana wengine, mpaka niweze kufanya yale ambayo nilifikili kwamba mimi ni Mungu kumbe siyo, sina maana. Na kutoka hapo, alifanya METANOIYA.Yaani alibadilika alibadirisha fikra zake na mtazamo wake akawa ni mtu ambaye anamcha Mungu. Tunaalikwa, kama tulivyo sikiliza katika wasifu wa dada zetu hawa, tuweze kuishi kama inavyo tupasa kama watoto wa Mungu, na tufanye yote vizuri ni kama leo Mungu anakuja kutuchukua, nilikuwa na dada hawa wote wa nne hapa waboko wakiwa na chata yao, wakati wanaanza, kufungua lakini vile vile wanapofunga na maneno yao nakumbuka mbaye alikuwa anakaribisha wenzake ni Sr Damaris alikuwa anamkaribisha Mama Mkuu aweze kuongea na akaweza kuongea na baadaye wakakaribisha wote waliyo chaguliwa, na badaye wakatambulishwa pamoja tukaagana vizuri. na kwa hiyo unaposikia kwamba hawapo lazima uwe na mshituko, lazima uwe na simanzi na ndiyo maana sasa sisi tunao baki, tunasema buriani dada zetu.
Mmefanya kazi kubwa, mmejitahidi sana, buriani, sisi tunabaki, lakini tunajifunza katika safari yetu ya maisha, tusijisahau. Tusije kujisahau, walau tuweze kufuata mfano wa yule aliyeingia mochwari ili tuweze kubadirika. Maisha yetu hayana maana, ni mavumbi tu kama atujamuweka Mungu mbele. Munga anatupa maana katika maisha yetu, na tunaposema sasa buriani kwa dada zetu hawa, tukisema asante sana kwa kazi mlizo zifanya, tukiangalia shirika, mlivyo ongoza na mlivyoishi na wenzenu.Na wakati mwingine tunasema kwamba tunaomba vile vile muwe waombezi wetu, kama kuna chochote kile hamkuweza kutimiza tuzidi kuwaombea Mungu azidi kuwasafisha. Ili muweze kuingia katika mikono yake, tuseme kwamba ni roho za wenye haki, ambao wamo mikononi mwa Mungu ambao tunawakumbuka leo na tuna wasindikiza. Tunaposema buriani kila mmoja ajitathimini maisha yake, aangalie mahusiano yake na wenzake, atambue kwamba tuna hati miliki ya dunia hii.
Tunahitaji kila mara kufanya uongofu, kufanya vizuri kile mbacho tumekabidhiwa kukifanya ili, wakati wowote Munga atakapo tuchukua tuendele mbele. Tuendelee na twende mikononi mwake, tusije tukajisahau, tukawa na kiburi na matokeo yake tukaondoka katika kiburi na tutambue hilo kwamba Mungu ni Mkuu na Mungu ndiyo muweza wa yote na ndiye anaamuwa yote, lakini wakati huo huo tunapowasindikiza wenzetu hawa tujue kwamba tukiwa katika safari ya hija hiyo, asa tukiwa akatika mwaka huu mtakatifu ambapo kaulimbiu yet inasema kwamba mahujaji katika matumaini sisi ni maujaji katika matumaini na tuweze kuwa wamisionari wa matumaini kwa kuishi na kuwasaidia wengine ambao wamekata tama waweze kuwa na matumaini ili Mungu, itakapofika wakati atupoke mikono ni mwake.
Tuendele kuwaombea na tuseme kwamba mpumzike kwa amani, tunatambua kazi zenu, tunatambua uwepo wenu, tutawakumbuka sana, na pamoja na haya, hata sauti zenu bado tunazo tunazisikia vichwani mwetu, mlivyo kuwa mkiongea na sisi, kwamna ya pekee tunatoa pole sana kwa masista wakalmeri, lakini pole kwetu sote, kwasababu hili ni letu wote, Mungu atutiye nguvu, Mungu atupe imani kubwa na Mungu atupe moyo mkuu na matumaini makubwa, tupokee kwa imani na matumaini, msiba huu mkubwa sana. Ili, tukiwa na matumaini hayo, basi tujue kwamba Mungu amewapokea mikono ni mwake.
Tumsifu Yesu Kristo.