Kard.Sako:Ushirikiano unaimarisha uhusiano na kuunda ukaribu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuunda tume mchanganyiko kwa ajili ya utafiti wa kisayansi kuhusu Biblia, taalimungu, liturujia, katekisimu, kuzichapisha katika lugha ya kisasa inayoeleweka; kupanga mikutano ya maombi ya pamoja na semina juu ya mada ya maslahi ya kawaida; kubadilishana uzoefu wa kiroho, maandalizi ya kizazi kipya cha wakleri wanaoamini katika kazi ya pamoja; kuunganisha mtazamo na hotuba, hasa katika ulimwengu uliochanganyikiwa na usiojali maadili. Hivi ndivyo Patriaki wa Wakaldayo wa Baghdad, Kardinali, Louis Raphael Sako alipendekeza katika tafakari iliyotolewa kwa ajili ya Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo kwa mwaka 2025(kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari) ambapo mwaka huu liaongozwa na kauli mbiu: “Je, unaamini hili?” (Yh 11:26 ).
Makanisa lazima kuongeza jitihada za kutetea haki
Kwa upande wa Mkuu wa Kanisa la Wakaldayo anabainisha kuwa "Katika aina hizi za ushirikiano, Makanisa mbalimbali yanapaswa pia kuongeza jitihada kubwa za kutetea haki na usawa, uraia shirikishi, kupatikana kwa amani na utulivu, kukemea dhuluma, rushwa, umaskini, ujinga na maradhi; utengenezaji wa silaha za kuchochea vita, kusambaratishwa kwa watu wenye msimamo mkali na matamshi ya chuki, kudumisha mazingira safi ili kuepuka majanga yanayoikumba sayari yetu. Ushirikiano huu, ni ujumuishaji wa mshikamano wa kijamii na amani ya raia. Hatimaye, ni mpango wa Agano Jipya ambao Kanisa na Wakristo wanapaswa kutekeleza katika uhalisia wao.
Umoja si kuunganishwa makanisa kuwa moja:kuna historia,tamaduni,sheria na karama
Akizungumzia umoja, Kardinali Sako alikumbusha kwamba “umoja si kuunganishwa kwa makanisa kuwa Kanisa moja na utawala mmoja, kama wengine wanavyofikiri. Kila Kanisa lina historia yake, utambulisho wake, watakatifu wake na wafia dini na tamaduni yake, taratibu zake, sheria zake, lugha yake na karama yake. Kila Kanisa pia lina ‘kichwa’ chake ambacho huhakikisha umoja na uhai wake, na Sinodi ya kufanya maamuzi muhimu zaidi. Ninaamini kwamba ukweli huu wa kihistoria wa kikanisa lazima uheshimiwe na kuhifadhiwa.
Badala ya kuzungumza tofauti lazina kureja utajiri wake
Kardinali kwa njia hiyo alisema kwamba "na badala ya kuzungumzia tofauti, inafaa kurejea utofauti ambazo ni utajiri. Makanisa yetu ya kitume yanaitwa kurejesha imani na ujasiri wa kugundua kila siku matarajio ya utendaji wa pamoja wa kiekumene, hasa katika mazingira magumu yetu. Ushirikiano huu ni kielelezo cha vitendo cha umoja. Unaimarisha uhusiano na kuunda ukaribu."