2026.08.13 Mashindano ya kimataifa ya kitesurfing ya Kombe la Zanzibar 2026.08.13 Mashindano ya kimataifa ya kitesurfing ya Kombe la Zanzibar  (Photo credit: Stefano Conte)

Kombe la Zanzibar 2026:Mbio za amani,ushirika na udugu

Toleo la sita la mbio za kitesurfing la Kombe la Zanzibar na regatta linatarajiwa kufanyika katika visiwa vya Tanzania mnamo tarehe 23 Agosti 2026.Likiandaliwa na Daktari wa Italia Stefano Conte na Serikali ya Tanzania,mchezo huu unalenga hata kukuza ubora wa michezo huku ukiimarisha udugu na ushirika miongoni mwa watu wa mataifa mbalimbali.

Vatican News

Kwa zaidi ya muongo mmoja, daktari wa Kiitaliano Dkt. Stefano Conte amekuwa akisafiri mara kwa mara hadi Zanzibar,  kisiwa cha Tanzania, ambapo alianza kufanya kazi kama daktari akiwahudumia wakazi wa eneo hilo na wageni. Kile kilichoanza kama "likizo wakati wa kazi" mwaka 2010 kilikuja kuwa ahadi ya muda mrefu. Huku akitoa huduma ya matibabu katika jamii za wenyeji bila malipo, Conte pia aliendeleza shauku yake ya kupiga kitesurfing, ambao ni mchezo katika maji ya joto ya Zanzibar, katika upepo thabiti, na vizuizi vya miamba ya matumbawe vilivyolindwa huunda mazingira bora.

Katika mahojiano na Radio Vatican/Vatican News, alielezea jinsi ambavyo kwa miaka mingi alivyoanza kujiuliza jinsi angeweza kuchangia zaidi ya huduma yake kama daktari. Jibu lake lilikuwa kuanzisha Kombe la Zanzibar, shindano la kimataifa la kitesurfing lililoundwa sio tu kuonesha kisiwa hicho kama mahali pa michezo ya kiwango cha dunia lakini pia kutoa fursa kwa jamii ya wenyeji kupitia utalii na ushirikiano wa Kimataifa.

Zanzibar Cup kitesurfing race and regatta

Shindano la Kombe la Zanzibar la kitesurfing na regatta(Photo credit: Stefano Conte).

Kutoka ndoto hadi uhalisia

Akitumia uzoefu wake kama mwanachama wa muda mrefu wa Shirikisho la Mabaharia la Italia na historia yake ya kitaaluma, Conte alipendekeza kuandaa shindano la kwanza la kimataifa la la kupiga kitesurf Zanzibar. Serikali mahalia  ilikubali wazo hilo, na kuwa mshirika katika mpango huo. Tukio la uzinduzi, lililofanyika kwa mara ya kwanza  mnamo Januari 2024, lilivutia washindani wapatao 20 na mdhamini mmoja. Tangu wakati huo, shindano limekua kwa kasi, sasa likiwakaribisha wanariadha 40-50 na wadhamini 10-15, huku mwonekano ukiongezeka kimataifa.

Ustadi wa michezo na ushirika

Kwa Conte, Kombe la Zanzibar ni zaidi ya mashindano ya maji tu. Anaona michezo kama lugha ya ulimwengu wote inayoweza kuwaleta watu pamoja katika ushirika na kusaidia kuthamini utajiri na utofauti wa tamaduni na asili tofauti. Akiongozwa na ujumbe wa Papa Francisko na Papa Leo XIV, pia amelenga kuunda tukio hilo kuzunguka maadili ya amani, udugu, heshima, na mshikamano.

"Wapendeni kaka na dada kama mnavyotaka kupendwa ninyi"

Zaidi ya kuandaa tukio la michezo, anatumaini  kuunda fursa inayowatia moyo watu kuonana kama kaka na dada badala ya wapinzani. Kanuni yake inayoongoza ni rahisi: "Wapendeni kaka  na dada zenu kama mnavyotaka wawapende ninyi." Dkt. Conte anaamini kwamba ikiwa watu wengi zaidi wangekubali wazo hili la msingi, dunia ingekuwa mahali pa amani zaidi.

Zanzibar Cup kitesurfing race and regatta

Shindano la Kombe la Zanzibar la kitesurfing na regatta(Photo credit: Stefano Conte)

Michezo kama mwalimu

Akitafakari mafunzo ambayo shughuli za michezo zinaweza kutufundisha, Dkt. Conte aliakisi nidhamu, heshima kwa sheria, uvumilivu, na unyenyekevu. Akitumia miaka yake ya kufanya kazi katika upasuaji wa moyo wa watoto, anakumbuka kwamba madaktari bingwa wa upasuaji aliokutana nao pia walikuwa wanyenyekevu zaidi. Katika uzoefu wake, utaalamu wa kweli unajieleza wenyewe, huku kiburi mara nyingi kikificha ukosefu wa usalama. Anasema kwamba ulimwengu wa leo unahitaji uhalisia zaidi na upuuzi kidogo, akiamini kwamba uwezo na uadilifu hatimaye hushinda mwonekano wa kijuu juu.

Zanzibar Cup kitesurfing race and regatta

Shindano la Zanzibar la kitesurfing na regatta(Photo credit: Stefano Conte)

Upekee wa kitesurfing

Kitesurfing huchanganya vipengele vya kuteleza na kusafiri kwa upepp. Wachezaji wake  husimama kwenye ubao huku wakivutwa na kite kubwa inayoweza kudhibitiwa inayoruka takriban mita 20 juu ya ardhi. Ingawa unaweza kuwa hatari ikiwa utafanywa vibaya, Conte anasisitiza kwamba ni salama sana unapofundishwa na wakufunzi waliohitimu katika maeneo yanayofaa. Amewafundisha wanaoanza kibinafsi kuanzia watoto wadogo wa miaka saba au nane hadi watu wazima walio katika miaka yao ya sabini.

Kombe la Sita la Zanzibar

Toleo la sita la Kombe la Zanzibar litafanyika Agosti 23 katika pwani ya mashariki ya Zanzibar, huko Kiwengwa, eneo linalojulikana kwa upepo wake unaoendelea na hali nzuri ya kuteleza kwenye kitesurfing. Dkt. Conte anatumaini kwamba Kombe la Zanzibar litaendelea kukua na kuwa tukio kubwa la michezo ya kimataifa huku likiendelea kuwa kweli kwa dhamira yake ya awali: kutumia michezo kwa kujenga madaraja kati ya watu.

Zanzibar Cup kitesurfing race and regatta

Shindano la Kombe la Zanzibar la kitesurfing na regatta

Kauli mbiu:"Kuwa mmoja kwa wote na wote kwa mmoja"

Kauli mbiu ya tukio hilo inashikilia roho hiyo: "Mmoja kwa wote, wote kwa mmoja." Kwa Conte, hii ni zaidi ya kauli mbiu kwani inaonyesha imani yake kwamba kila mtu ana jukumu la kuwasaidia wengine na kufanya kazi pamoja kuelekea ulimwengu wenye amani na umoja zaidi.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

 

14 Agosti 2026, 11:56