Picha iliyopigwa Nicosia mnamo Mei 4, 2026, inaonesha mtu mbele ya skrini kubwa akionesha mienendo ya chombo katika Mlango-Bahari wa Hormuz kwenye tovuti ya ufuatiliaji wa meli. Picha iliyopigwa Nicosia mnamo Mei 4, 2026, inaonesha mtu mbele ya skrini kubwa akionesha mienendo ya chombo katika Mlango-Bahari wa Hormuz kwenye tovuti ya ufuatiliaji wa meli.  (AFP or licensors)

Hali ya wasiwasi katika Mlango-Bahari wa Hormuz

Jeshi la Marekani linasema linasindikiza meli za mizigo zilizokwama kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz chini ya mpango mpya wa Rais Donald Trump, "Mpango wa Uhuru "huku makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran yakiendelea kuwa dhaifu.

Na  Nathan Morley

Jeshi la Marekani Jumatatu Mei 4, 2026 lilianza kusindikiza meli za mizigo zilizokwama kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz chini ya mpango mpya wa Rais Donald Trump, "Mpango wa Uhuru,” huku Ripoti za vyombo vya habari zinaonesha kuwa Iran inaendelea kudhibiti mlango-bahari huo na Jumatatu hiyo hiyo, ilirusha makombora na ndege zisizo na rubani kwenye meli za kijeshi na za kibiashara. Wakati huo huo, mashirika ya baharini ya Umoja wa Mataifa yalizitaka meli kuwa na "tahadhari kubwa" huku mkusayiko wa meli  kupitia mlango bahari mwembamba -wenye kupitiwa takriban 20% ya shehena za nishati duniani -ukiendelea kukatizwa sana.

Kukwama kwa mabaharia

Takriban mabaharia 20,000 bado wamekwama ndani ya meli zipatazo 2,000, kulingana na makundi ya kimataifa ya meli. Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini limesema linafanya kazi kuthibitisha mfululizo wa mashambulizi na maonyo ya hivi karibuni yaliyotolewa kwa waendeshaji wa kibiashara. Lango la usalama wa baharini la Jeshi la Wanamaji la Uingereza liliripoti kwamba meli ya mafuta ilipigwa na makombora yasiyotambulika kaskazini mwa Fujairah katika Falme za Kiarabu Jumatatu, Mei 4.

Tahadhari ya kuondoka kwenye nanga

Hilo lilifuatia shambulio la siku moja mapema kwenye meli kubwa ya kubeba mizigo na meli kadhaa ndogo karibu na Iran. Meli zingine zimeamriwa na radio kuondoka kwenye nanga zao, ikionesha kile ambacho mamlaka za baharini zinakielezea kama mazingira ya usalama yanayobadilika haraka. Tangu mwishoni mwa Februari,2026 angalau matukio 41 yanayohusisha meli katika Ghuba ya Arabia, Mlango wa Hormuz na Ghuba ya Oman yameripotiwa, kulingana na vituo vya ufuatiliaji wa kikanda.

Imesasishwa tarehe 6 Mei 2026 saa 10.04 asubuhi na Angella Rwezaula.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

06 Mei 2026, 09:52