Mabadiliko ya Sheria ya wahamiaji Hispania:'Kila mtu ni lengo msingi kwake mwenyewe'
Na Joseph Tulloch - Vatican.
Mnamo mwezi Januari 2026, Baraza la Mawaziri la Hispania liliidhinisha azimio linalowapata wahamiaji bila hati ya makazi, ambao ni mamia na maelfu ya wahamiaji wasio na nyaraka. Wakati ambao mjadala wa kuwarudisha au kuwatia kizuizini umeshika kasi uamuzi huu ulikuwa wa kuvutia. Nchini Hispania, wahamiaji wasio na hati “waliishi kwa miaka mingi gizani,” alisema Amaya Valcarcel mshauri na mtetezi katiku huduma ya wakimbizi inayosimamiwa na Shirika la Wakimbizi la Wajesuit.
Takribani makadirio ya wahanga 500,000 hadi milioni moja walioathiriwa, kurekebishwa kwa hali ya sheria hii ina maana kuwa “ni kutambua uwepo wao kisheria” na kupiga hatua kuelekea “usalama wao kisheria.” Akizungumza na Vatican news, Valcarcel akiwa Hispania alibainisha kuwa wahamiaji wasio na nyaraka “wanafanya kazi muhimu sana” nchini Hispania kwenye sekta kama za kilimo, ukarimu, ujenzi na kazi za ndani. Hata hivyo, bila kuwa na mikataba sahihi ya kazi hizo au mtandao wa usalama, hii ina maana kuwa “wanaishi katika hatari ya kudumu.” Watu wakiwa nje ya Ubalozi wa Pakistan huko Barcelona kufuatia tangazo hili
Swala la Kimaadili na siyo la Kiuchumi
Mara kwa mara majadiliano dhidi ya wahamiaji yanafanywa kwenye mtazmo wa kiuchumi: Nchi za Magharibi zinahitajii waamiaji kwa ajili ya nguvu kazi na kuwalipa pensioni ya idadi ya watu wenye umri mkubwa inayokuwa kwa kasi. Katiaka makala iliyozua mjadala,iliyochapishwa na New York Times, ambayo iliandikwa mapema mwezi huu, Waziri wa Hispania Pedro Sanchez alisisitiza kuwa “kwanza na kwa umuhimu zaidi” sababu za kubadilisha sheria hii zilikuwa za kimaadili zaidi, wala siyo za kiuchumi. Wahamiaji hawa tayari ni sehemu ya jamii na jumuia ya Hispania, hivyo wanastahili kupata haki sawa.
“Kipindi cha mwishoni mwa juma” Sánchez aliandika, “wanatembea na kuingia katika mighahawa na kushiriki michezo ya timu za ndani,” lakini bado mpaka sasa hawakuweza “kupata elimu bora, kulipa kodi au kuchangia katika hali ya usalama kijamii.” Valcárcel alikazia uzito wa mafundisho msingi ya Kanisa yanayosisitiza kuwa wahamiaji hawapaswi “kutazamwa kama nyenzo muhimu ya kiuchumi.” Badala yake, kinyume na mbinu hii ya “utilitarian” Valcárcel alisisitiza kuwa Kanisa linakukumbusha kuwa “kila mtu ni lengo msingi kwake mwenyewe,” anayebeba heshima isiyovunjika na ambaye hapaswi “kutumika kama chombo cha kuhudumia kwa mahitaji ya muda mfupi tu.”
Hatua inayofuata
Wakati huo huo, Valcárcel amesisitiza kuwa, mabadiliko ya sheria bado “siyo suluhisho la kudumu.” Imeandaliwa kutumika kwanza kwa mwaka mmoja, hali inayosababisha kutokujua kitakachofuata baada ya hapo ,alisisitiza Valcárcel, hata hivyo haiondoi mageuzi ya kina ya kimuundo. Kati ya mabadiliko msingi Valcarcel alisisitiza ni kuundwa kwa sera za ujumuishi wa muda mrefu, zenye kuleta ulinzi thabitiwa wafanyakazi, na zaidi sana kufuata njia sahihi za uhamiaji wa kisheria,aliongeza.
Sinodi ya Kiraia ya Ushirikishwaji
Hatimaye, Valcarcel aligusia pia mchakato wa kufanya maamuzi kufuatia hatua hiyo. Mabadiliko ya seria yanaanza na maombi yaliyojumiya uwekaji sahihi zaidi ya wahamiaji 700,000 kwa kushirikiana na mashirikia zaidi ya 900 ya kiraia. Hii ni pamoja na Kanisa Katoliki alibanisha Sanchez katika andiko lake kwa New York Times. Zaidi ya watu 17,000 wa kujitolea walibisha hodi na kutembelea vyuo vikuu, vituo vya kijamii, makanisa, kuchukua sahihi za kuridhia mswada huo kujadiliwa bungeni. Baada ya kuwaleta pamoja watu binafsi na taasisi kwenye jamii zote Hispania, Valcárcel alipendekeza mchakato kutumia lugha ya Kanisa, kama mfano wa “Sinodi ya Kiraia ya Ushirikishwaji,”(Synodal Civil Engagement) hali ambayo imefanya jitihada za kuunganisha jamii iliyokuwa imegawanyika.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here