2026.01.15 Dk.Alvaro Lario,Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD). 2026.01.15 Dk.Alvaro Lario,Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD).  (@VATICAN MEDIA)

Rais wa IFAD:Kilimo kinaweza kuwa chombo cha amani na matumaini

Rais wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD)baada ya kukutana na Papa Leo XIV,Januari 15 alizungumza na Vatican News kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika jamii za vijijini,kama chanzo cha chakula kwa jamii zao na ulimwengu kwa ujumla.

Na Kielce Gussie – Vatican.

Karibu watu bilioni 2.5 hadi 2.6, karibu theluthi moja ya idadi ya watu duniani wanategemea kilimo kwa ajili ya riziki yao, kulingana na takwimu ya hivi karibuni ya Shirika la Chakula Duniani(FAO.) Hata hivyo, kutokana na changamoto kadhaa, kama vile migogoro, mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa rasilimali, wengi wanapambana na ukosefu wa usalama wa chakula. Shirika linazingatia ubinadamu na sio ujumla wa watu, kama vile mtoto nchini Sudan anayejitahidi kupata chakula cha kutosha kwa siku hiyo au kijana mdogo nchini Bangladesh anayetafuta kazi katika mgogoro.

Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) upo katika nchi 92, ukifanya kazi kutekeleza miradi na mipango inayoendeleza ustawi, usalama wa chakula, na ustahimilivu kwa wakazi wa vijijini. Kinachotofautisha IFAD na mashirika mengine ya maendeleo ni kwamba inafanya uwekezaji mkubwa na kwa kawaida, hufadhili miradi pamoja na serikali, jamii, na sekta binafsi. Ufadhili huu wa pamoja husaidia kuhakikisha kwamba washirika wote wanamiliki na kuwajibika.

Kuwekeza katika hatua ya kwanza

Kazi ya Shirika hili la IFAD linaipatia kipaumbele "kuwekeza kwa watu wa vijijini". Lakini ni suala  linalozidi kuzalisha chakula cha kutosha tu. Kama Rais wa Shirika hilo, Dkt. Alvaro Lario, alivyoeleleza kwamba, kitu cha muhimu pia ni kuhakikisha "jamii hizi zinapata pembejeo, teknolojia, vifaa vya kuhifadhia, na masoko ili kuweza kupata mikopo, bima, maji, udongo unaofaa, na mbegu."  Haya yalijiri,  tu mara baada ya kukutana na Papa Leo XIV kwa Mkutano kibinafsi tarehe 15 Januari 2026 mjini Vatican, Dk. Lario alizungumza na Vatican News kwamba, wao hawazingatii uzalishaji wa chakula tu, bali pia kuhusu kuhakikisha kwamba kilimo ni biashara.

Lengo la mwisho ni kujenga mustakabali endelevu na chanya kwa watu katika jamii za vijijini kutafuta kuwalisha kwa maisha yote na si siku moja tu. Kwa shirika hili la IFAD, hiyo ina maana ya kuwekeza katika "hatua ya kwanza": wakulima wadogo na jamii za vijijini. Dk. Lario alielezea kwamba wao ndio wanaozalisha chakula. Haimaanishi kuzingatia "kupokea chakula tu kutoka  nchi zilizoendelea au kutoka katika miji," bali inahusisha "mabadiliko ya mtazamo." Kipaumbele na uwekezaji hupewa watu wanaolima chakula na kutunza ardhi. Bila msaada huu, wanaume na wanawake mara nyingi hujitahidi kujikimu, sembuse kulima chakula cha kutosha kuuza na kuvuna faida za kazi yao.

"Katika maeneo haya ya vijijini, Umaskini mwingi na uliokithiri ni asilimia 80%, Dkt. Lario alisisitiza. "Tunajua kwamba katika nchi zilizoendelea, maeneo ya vijijini kwa kawaida hayawekezwi sana." Badala yake, msisitizo unawekwa kwenye sekta nyingine. Rais wa IFAD alisema kwamba kilimo ni aina ya uzalishaji wa kiuchumi, ni muhimu sana kwa maeneo haya ya vijijini. "Tunajua,kwamba kilimo kiukweli kina ufanisi mara mbili hadi tatu zaidi katika ukuaji wa uchumi kuliko maeneo mengine kwa sababu jamii na nchi nyingi bado zinategemea sana kilimo." Ndiyo maana, ni muhimu sana kuhakikisha kwamba minyororo ya ugavi wa ndani inapaswa kuanzishwa ili iweze kuunganishwa kwa urahisi na masoko mapana ya kikanda na kimataifa.

Zana ya amani

Ili kupambana na ukosefu wa fedha katika ulimwenguni kote, IFAD inatekeleza programu na mipango maalum kwa mahitaji ya watu. Kwa mfano, nchini Sudan, ambapo janga baya zaidi la kibinadamu duniani limetokea,  shirika hilo limezindua mradi uliowekwa kwa wakulima wadogo kuboresha usalama wa chakula, kuongeza mapato, na kujenga ustahimilivu. Zaidi ya hayo, Rais wa IFAD alielezea kwamba amekuwa akikutana na wajumbe na mawaziri wa taifa kujadili jinsi ya kuboresha hali ya sasa. Alibainisha kuwa kufanya kazi katika kuzalisha na kutoa chakula ni muhimu, lakini jambo lingine muhimu ni kuunda mahali pa watu kutumaini mustakabali bora "ambapo wanaweza kuendelea kufanya kazi, kuzalisha, na kuwa na chakula kinachopatikana."

Katika mataifa kama Sudan, ambapo vurugu na migogoro vimeifanya iwe vigumu kuendelea kutoa misaada, Dkt. Lario anaonyesha uhusiano kati ya migogoro na ukosefu wa usalama wa chakula. Migogoro "ni wazi kuwa chanzo cha njaa na cha umaskini," alisema. Hata hivyo, kwa mabadiliko ya mtazamo na unaozingatia zaidi watu kuhusu ulimwengu, kilimo kinaweza kuwa chombo cha amani. "Kwetu sisi, kilimo ni njia moja ya kuunganisha jamii, na inaweza kuwa njia ya upatanishi, katika hali nyingi, amani, lakini pia matumaini," Dk. Lario alisisitiza. Hiyo haimaanishi kwamba njia za kisiasa zipuuzwe. Sauti kama za Papa Leo XIV zinaweza kusaidia kuvutia umakini kwa hali inayoendelea katika nchi mbalimbali.

Muunganisho maalum kwa Papa kutoka Amerika

Baba Mtakatifu Leo XIV katika mkutano wao tarehe 15 Januari 2026, Rais wa IFAD alisema yeye na Papa walizungumzia kuhusu kubadilisha maisha na umuhimu wa kuwaletea watu matumaini. "Sehemu ya matumaini ni muhimu sana kwa sababu inatupa sote kitu cha kutafuta "Walijadili kazi ambayo IFAD inafanya katika jamii kadhaa nchini Peru ambapo Papa Leo XIV alifanya kazi kama Askofu. Baba Mtakatifu alielezea mapambano ambayo jamii nyingi za vijijini zinakabiliwa nayo, alisema “walikuwa wakizalisha chakula kizuri, lakini hawakuwa wakivuna matunda yake." Hili, Dk. Lario alisisitiza, ndilo sehemu muhimu. Hata hivyo, kwa mipango na programu za IFAD zinazoendelea, matumaini ni kwamba jamii hizi zitakuwa na zana, ufikiaji, na rasilimali zinazohitajika ili kutoa sio tu kwa ajili yao wenyewe, bali kwa jamii zinazowategemea.

Rais -IFAD

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

19 Januari 2026, 14:40