Kambi ya Wakimbizi huko Dafur, Nchini Sudan. Kambi ya Wakimbizi huko Dafur, Nchini Sudan.  (AFP or licensors)

Watu 75 wauawa huko Sudan katika shambulio kwenye kambi ya wakimbizi ya Darfur

Katika nchi hiyo ya Kiafrika,vikosi vya kijeshi viliwashambulia watu waliokimbia makazi yao waliokusanyika katika msikiti karibu na El-Fasher.Hali mbaya ya unyanyasaji huathiri walio hatarini zaidi.Coopi yatoa wito kwa ajili ya watoto wanaolipa ghama ya juu bila hatia.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Zaidi ya watu 75 waliuawa tarehe 20 Septemba 2025  katika shambulio la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye kambi ya wakimbizi ya Abu Chok, karibu na El-Fasher, huko Darfur, kaskazini mwa Sudan. Kitengo cha dharura kinachoendesha kambi ya wakimbizi huku kukiwa na matatizo makubwa kiliripoti hili, kikibainisha kuwa ndege isiyo na rubani ililenga watu waliokimbia makazi yao waliokusanyika msikitini. Makumi walijeruhiwa, wengi wao vibaya.

El-Fasher—ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan huko Darfur, ambapo zaidi ya raia 260,000 wamekwama kwa miezi kadhaa katika hali ya kukata tamaa, bila msaada na wenye mahitaji makubwa—imekuwa ikizingirwa na RSF tangu Mei 2024. Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa umeamua kuwa RSF imefanya uhalifu dhidi ya binadamu. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vilianza Aprili 2023, na tangu wakati huo, mapigano na mashambulizi yamesababisha vifo vya watu 150,000, wengi wao wakiwa raia wasio na silaha, watu milioni 12 waliokimbia makazi yao (kati ya takriban wakazi milioni 50), na mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika karne ya 21.

Mkasa kwa  wadogo

Nchi nzima iko katika magofu, na wale wanaolipa bei ya juu zaidi, kama kawaida, ndio walio hatarini zaidi: watoto. Kwa mujibu wa Chiara Zaccone, mkuu wa ujumbe wa COOPI (Ushirikiano wa Kimataifa) nchini Sudan, anajionea mwenyewe machungu na mapambano ya kuishi kwa wale walioachwa bila chochote. Ushuhuda wake, uliorekodiwa na vyombo vya habari vya Vatican, ni wa mtu ambaye ameona matumaini yanafifia polepole, lakini pia wa mtu ambaye anaendelea kupambana kusaidia watu walio hatarini zaidi. Zaccone alielezea hali mbaya inayowakabili watoto wa Sudan: "Sudan inakabiliwa na moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada

Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, na wengi wao ni watoto. Hakika, wadogo zaidi ni waathirika wa kwanza wa mzozo unaoonekana usio na mwisho. Kila siku, maelfu ya watoto hupoteza maisha, sio tu kutokana na ukatili wa vita, lakini pia kutokana na njaa na utapiamlo. Katika El-Fasher, jiji lililozingirwa kwa karibu miaka miwili, maisha ya kila siku yamekuwa ndoto: "Idadi ya watu inatatizika hata kumudu mlo mmoja kwa siku.

20 Septemba 2025, 14:41