Baba Mtakatifu leo XIV tarehe 15 Agosti 2026 amemteuwa Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Tonga. Baba Mtakatifu leo XIV tarehe 15 Agosti 2026 amemteuwa Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Tonga.  (ANSA)

Askofu Mkuu Gábor Pintér Balozi wa Vatican Ufalme wa Tonga

Askofu mkuu Gábor Pintér ameteuliwa ba Baba Mtakatifu leo XIV kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Tonga na anaendelea kuwa ni Balozi wa Vatican: nchini New Zealand, Visiwa vya Cook, Fiji, Kiribati, Visiwa vya Marshall, Shirikisho la Nchi za Mikronesia, Nauru, Palau, Samoa, na Vanuatu, pamoja na kuwa Mwakilishi wa Kitume katika eneo la Bahari ya Pacifiki. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini New Zealand.

Na Padre Richard A. Mjigwa C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 15 Agosti 2026 amemteuwa Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Tonga na anaendelea kuwa ni Balozi wa Vatican: nchini New Zealand, Visiwa vya Cook, Fiji, Kiribati, Visiwa vya Marshall, Shirikisho la Nchi za Mikronesia, Nauru, Palau, Samoa, na Vanuatu, pamoja na kuwa Mwakilishi wa Kitume katika eneo la Bahari ya Pacifiki. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Julai 2024 alimteuwa Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi wa Vatican nchini New Zealand na kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Gábor Pintér alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Honduras. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Gábor Pintér alizaliwa tarehe 9 Machi 1964 huko Kunszentmárton, nchini Hungaria. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Juni 1988 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe Mosi, Juni 1996 akajiunga na diplomasia ya Kanisa na hivyo kutumwa nchini Haiti, Bolivia, Sweden, Ufaransa, Ufilippini na Austria.

Askofu mkuu Gàbor Pintèr, Balozi wa Vatican Ufalme wa Tonga
Askofu mkuu Gàbor Pintèr, Balozi wa Vatican Ufalme wa Tonga   (ANSA)

Tarehe 13 Mei 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Belarus na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, akawekwa wakfu tarehe 15 Julai 2016 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Tarehe 12 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Honduras. Na ilipogota tarehe 27 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini New Zealand. Katika maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho, tarehe 15 Agosti 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV akamteuwa Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Tonga.

Ufalme wa Tonga
18 Agosti 2026, 11:32