2026.05.15 Dicastero per la Comunicazione conferenza internazionale “Custodire voci e volti umani”

Uaminifu ni njia halisi ya mchezo wa kielimu na akili unde

“Akili unde,Uandishi wa Habari na Maono ya Magnifica Humanitas" ilikuwa mada ya Mkutano kwa njia ya Mtandao uliofanyika mnamo Juni 25,kuanzia alasiri.Wazungumzaji walikuwa Sr Nina Krapić,Naibu Msemaji wa Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu,Adeline Hulin Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu ya Habari na Ujuzi wa Kidijitali katika UNESCO na Benjamin Rosman,Mkurugenzi wa Taasisi ya MIND,Chuo Kikuu cha Witwatersrand,nchini Afrika Kusini.

Na Davide Imeneo

Vijana wadogo na wengi zaidi wanazungumza na akili unde kana kwamba wanazungumza na rafiki. Semina ya mtandaoni (il webinar formativo)iliyofadhiliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ilisaidia kuelezea jinsi ya kuelimisha na kutambua mapungufu yake.

Vijana na Akili Unde: Kwa Nini Akili unde  inakuwa Siri

Akizungumza na wanafunzi wake, Profesa wa sayansi ya kompyuta aligundua kwamba wengi wao hutumia akili unde kama mwanasaikolojia na alipoonesha mshangao, wanafunzi walimtazama kana kwamba hakuelewa: "Bila shaka, tufanye nini kingine?" Kipindi hicho, kilichosimuliwa na Benjamin Rosman, mkurugenzi wa Taasisi ya Akili katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Afrika Kusini, wakati wa semina ya mafunzo kuhusu akili unde iliyofanyika tarehe 25 Juni 2026 kwa kuratibiwa na  Baraza la Kipapa la Mawasiliano na kuongozwa na Naibu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu, Sr Nina Krapić, kilionesha vyema wakati tunaoishi. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao kwa kujikita na mada: "Akili unde, Uandishi wa Habari na Maono ya Magnifica Humanitas, " kama sehemu ya mwendelezo wa Mkutano wa kwanza uliofanyika tarehe 21 Mei 2026 kabla ya kuchapishwa kwa Waraka wa Kwanza wa Papa Leo XIV wa "Magnifica Humanitas", unaoijikita na masuala ya ubinadamu katika muktadha wa akili unde.


Wazazi na Washirika wa AI:Jukumu la Elimu ya Kidijitali katika Familia

Data inayotoa msingi wa kuelewa muktadha ilitoka kwa Adeline Hulin, Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Vyombo vya Habari na Habari ya UNESCO: Mwaka jana (2025) nchini Marekani, 72% ya vijana waliwasiliana  na "marafiki wa AI," mara nyingi bila wazazi wao kujua, kwa sababu kwa watoto wengi, teknolojia hizi tayari ni sehemu ya maisha ya kila siku, huku ujumuishaji wa watu wazima ukiwa polepole zaidi. Ni 43% tu ya nchi zimejumuisha kipengele cha uelewa wa vyombo vya habari katika mitaala ya shule, na, ni wazi, ikiwa shule hazitashughulikia kipengele hiki cha elimu, mzigo utaangukia kwa familia. UNESCO imejitolea mwongozo maalumu  kwa ajili ya familia, uliochapishwa mnamo Juni 22, siku tatu kabla ya mkutano wa wavuti unaoandaliwa na Baraza la  Kipapa la Mawasiliano(https://www.unesco.org/en/articles/unesco-launches-new-family-guide-digital-age)

Jambo hilo, Hulin alielezea, ni rahisi kuelewa: wazazi wanapaswa kupendezwa na maisha ya kidijitali ya watoto wao kama wanavyopendezwa na maisha yao ya nje ya mtandao, lakini hii haimaanishi kwamba wanahitaji kuwa wataalamu wa teknolojia. Kwa kweli, kama vile nyumbani tunavyojadili marafiki zetu ni akina nani na kilichotokea mchana, mazungumzo hayo yanapaswa kupanuliwa hadi kwenye mada zinazohusiana na ulimwengu wa mtandaoni, kujenga uhusiano wa uaminifu na vijana na kuwapa uhuru polepole. Ni wazi kwamba kuweka mfano pia ni muhimu: watoto wanajitahidi kufuata sheria ambazo wazazi wao hawazifuati kwanza.

Kutoka Akili hadi Hekima: Kujifunza wakati wa kuamini AI

Hulin, katika uwasilishaji wake, alifafanua kwamba kuna tofauti kati ya akili na hekima: "Akili ni kuhusu kutoa majibu, lakini hekima ni kuhusu kuuliza kama majibu hayo yanapaswa kuaminiwa au kutumika kabisa." Kwa hivyo, kutoka  mtazamo huu, lengo la uelewa wa vyombo vya habari ni kukuza kileambacho  Hulin anachokiita "hekima ya AI": kujifunza wakati wa kuamini na wakati wa kutilia shaka, wakati wa kukubali jibu na wakati wa kulithibitisha, wakati wa kutegemea mfumo otomatiki na wakati wa kurudi nyuma. Kanuni hiyo hiyo, zaidi ya hayo, inajitokeza katika kurasa kadhaa za Magnifica Humanitas, wa Papa Leo XIV uliochapishwa Mei, ambapo Papa anakumbuka kwamba kuwaelimisha watu kuhusu matumizi ya AI pia kunamaanisha kuwafundisha wakati wa kutoitumia.

Uelewa uliyoigwa ya AI na Hatari ya kukabidhi uaminifu

Katika suala hili, uchunguzi wa Rosman ni muhimu, unatusaidia kuelewa ni kwa nini suala hilo ni muhimu zaidi kuliko inavyoonekana: akili unde ya kuzalisha huiga huruma, na inafanya vizuri sana; katika baadhi ya vipimo sanifu, hupata alama za juu kuliko watu wa asili na rika tofauti. Hujibu kwa uchangamfu, uvumilivu, na kujiamini, hukumbuka mazungumzo ya awali, haichoki kamwe...kwa kijana anayejitahidi, hii inaonekana hasa kile kinachohitajika. Lakini kitu muhimu kinakosekana: "Tunasoma misemo ya kutia moyo, lakini mfumo hauna ukaribu halisi na wanadamu." Tunapomwamini daktari, mwalimu, au rafiki, "muundo wa uwajibikaji" huundwa kuzunguka uaminifu huo, huku mashine badala yake ikirudisha ishara za uhusiano, bila kuchukua jukumu lolote.

Kuanzia Mitandao ya Kijamii hadi AI ya Kimaadili, kwa nini hukumu ya Kibinadamu bado inahitajika

Rosman alielezea mwelekeo huu kama njia inayobadilika: mitandao ya kijamii imejifunza kuvutia umakini, kufurahisha hasira na mgawanyiko kwa sababu hutoa ushiriki mkubwa; AI ya kuzalisha, kwa upande mwingine, hupata uaminifu kwa sababu inazungumza kama mwanadamu na inaweza kujenga uhusiano na mtumiaji. Kinachoitwa AI ya kimaadili, chenye uwezo wa kutenda na kuamua kwa niaba yetu hata wakati wa kufanya kazi ngumu, kimepata mamlaka yetu ya kuingilia kati katika ulimwengu kwa niaba yetu. Kwa mwenendo huu, ulioanza na mitandao ya kijamii, tunapunguza ulinzi wetu kidogo zaidi kwa kila hatua ya mageuzi... na hili ni tatizo, kwa sababu hakuna teknolojia, hata iwe muhimu kiasi gani, inayopaswa kutuepusha na hukumu. Kuelewa jinsi taarifa zinavyozalishwa, kutambua wakati uhusiano unaigwa, kuamua wakati wa kuzima kifaa ni ujuzi unaowahusu watoto na watu wazima sawa.

Imesasishwa tarehe 4 Juni 2026 saa 6.48 mchana na Angella Rwezaula.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

04 Julai 2026, 12:48