Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 2 Julai 2026 amekutana na kuzungumza na Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 2 Julai 2026 amekutana na kuzungumza na Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia  (ANSA)

Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia Akutana na Papa Leo XIV

Katika mazungumzo ya Baba Mtakatifu Leo XIV na mgeni wake, kwa pamoja wameshukuru na kupongeza uhusiano mzuri uliopo kati ya Vatican na Colombia, kati ya Kanisa na Serikali hususan mchango wa Kanisa katika kuragibisha na kukuza misingi ya umoja wa Kitaifa; haki, amani na maridhiano. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili, baadaye wameangalia hali ya kijamii na kisiasa nchini Colombia pamoja na Ukanda mzima wa Amerika ya Kusini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 2 Julai 2026 amekutana na kuzungumza na Rais Gustavo Francisco Petro Urrego wa Colombia, ambaye, baadaye amepata fursa ya kukutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Daniel Pacho Katibu mkuu msaidizi wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Katika mazungumzo ya Baba Mtakatifu Leo XIV na mgeni wake, kwa pamoja wameshukuru na kupongeza uhusiano mzuri uliopo kati ya Vatican na Colombia, kati ya Kanisa na Serikali hususan mchango wa Kanisa katika kuragibisha na kukuza misingi ya umoja wa Kitaifa; haki, amani na maridhiano.

Wananchi wa Colombia wakishangilia
Wananchi wa Colombia wakishangilia   (AFP or licensors)

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili, baadaye wameangalia hali ya kijamii na kisiasa nchini Colombia pamoja na Ukanda mzima wa Amerika ya Kusini. Wamekazia zaidi athari za vita na uvunjifu wa haki msingi za binadamu; Uhalifu wa kupangwa Kitaifa na Kimataifa ambao kimsingi ni mtandao wa shughuli haramu zinazofanywa na magenge yanayovuka mipaka ya nchi kwa lengo la kujipatia faida kubwa. Huambatana na vitendo kama vile usafirishaji haramu wa binadamu, dawa za kulevya, silaha, na fedha chafu, ambavyo hudhoofisha uchumi na utawala wa sheria. Hatimaye, wakagusia athari za mabadiliko ya tabianchi.

Colombia 2026
03 Julai 2026, 15:32