Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. 

Mapadre wa Lefebvrian na Watu Walei:Utaratibu wa Kurudi kwenye Ushirika Katoliki

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linatuma taarifa kwa maaskofu Ulimwenguni kote kuhusu kile kinachopaswa kufanywa ili kuwakaribisha wale wanaoamua kuondoka kwenye Jumuiya ya Mtakatifu Pio X baada ya kitendo cha mgawanyiko kilichosababisha kutengwa upya na Kanisa.

Vatican News

Kurudi kwenye ushirika wa Kikatoliki baada ya kitendo cha mgawanyiko cha mnamo Julai 1 2026, hakutahitaji kurudia uzoefu wa tume maalum, kama ilivyokuwa kwa hati ya "Ecclesia Dei," kwa sababu Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  tayari limeandaa utaratibu kwa mapadre na waamini walei, wanaowahusika moja kwa moja na  watawa wa kijimbo na viongozi wa Udugu huo wanaofuatilia ibada ya kale na wameungana na Roma. Maagizo hayo yanawasilishwa katika siku zijazo kupitia Balozi za Vatican Ulimwenguni, kama ilivyotangazwa hapo awali katika Maelezo ya hati zilizochapishwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  mnamo tarehe 2 Julai 2026.


Maridhiano kwa Mapadre

Kitendo cha Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, kuanzia tarehe 1 Julai 2026, kinamtaka Padre ambaye ameamua kuondoka katika Jumuiya ya Kipadre ya Mtakatifu Pio X, akiwa tayari kukubali Mtaguso wa Pili wa Vatican na uhalali wa Novus Ordo Missae, yaani Sheria mpya ya Misa, ingawa ameshikamana na ibada ya kale, lazima "amtafute Askofu wa Kawaida (Askofu wa jimbo, Mkuu wa Shirika la Kitawa na Taasisi za kitawa zenye Haki za Kipapa,  Mashirika ya Vyama vya Kitume vyenye Haki za Kipapa, n.k.) akiwa tayari kumkubali kwa majaribio." Kisha Padre lazima "aandike barua kwa mkono wake mwenyewe kwa Baba Mtakatifu ambapo anajitambulisha na kuomba msamaha wa lawama zilizotokana na sababu ya kuwekwa wakfu na Askofu aliyetengwa au asiye wa kawaida, au akiwa amewekwa wakfu kihalali na halali, na baadaye akawa amejiunga na Jumuiya ya Kipadre ya Mtakatifu Pio X."

Kanuni ya  Imani na namna ya kujiunga

Padre lazima pia ambatishe cheti cha kuwekwa wakfu wa kipadre kilichosainiwa na tarehe  ya kufunga nadhiri na kanuni ya kujiunga “Professio fidi na Formula adhaesionis, " kilichosainiwa na kuandikwa tarehe.” Hii ni Kanuni ambayo inafupisha yaliyomo katika imani Katoliki, na Nadhiri na kanuni ya kujiunga, ambayo Padre anaahidi uaminifu kwa Papa, akijitolea kutoshambulia hadharani yeye au mafundisho yake. Anakubali fundisho la namba 25 la Katiba ya kidogma ya Mtaguso II wa Vatican “Lumen Gentium” kuhusu kukubali Majisterio ya Kanisa.


Pia anatamka  kwamba anazingatia  maadhimisho ya Misa kulingana na ibada zilizotangazwa na Papa Paulo VI na Yohane Paulo II kuwa halali na anafuata kanuni za Kanuni ya Sheria ya Kanisa iliyotangazwa na Papa Yohane Paulo II. Padre lazima atume hati (barua yenye cheti, Taaluma, na Kanuni ya kukubali ) zikitumwa na Mkuu wa Shirika "ambaye ataeleza katika barua inayoambatana na nia yake ya kumkubali (ad experimentum) kwa majaribio katika Jimbo  au taasisi yake." Mara tu hati zinapopokelewa kutoka Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume, Baraza hilo litaandika Hati ya msamaha, likimpatia mamlaka Shirika la Watawa kumkubali Padre anayeomba "kwa kipindi cha majaribio cha angalau mwaka mmoja na kisichozidi miaka mitatu, ambapo mwisho wake ataweza kuendelea kwake kupokelewa

Maridhiano kwa Wamini Walei

Hatua hizi, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linaelezea, "yanahusiana na suala la kutokuwa na hatia au kiwango cha uwajibikaji wa kibinafsi wa waamini walei ambao wamejiunga rasmi au kujiunga na Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu Pio X na ambao wanatafuta kuingia katika ushirika kamili na Kanisa Katoliki.” Kutolewa kwa adhabu kwa walei wa Jumuiya ya Mapadre wa  Mtakatifu Pio X hakuwezi, kiukweli, "kudhaniwa  kwa namna ya kiotomatiki, lakini lazima kutathminiwa kwa msingi wa kesi kwa kesi.”

“Kwa kuwa kutokuwa na hatia kunahitaji ufahamu kamili na ridhaa ya makusudi,” hati ya  Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa inasema, mifano ya kutokuwa na hatia iliyothibitishwa inaweza kujumuisha: Walei kushiriki  Daraja la Tatu la Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X; Walei wanaoshiriki mara kwa mara katika sherehe za Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X;  wakishiriki rasmi misimamo yake ya kimafundisho.


Hatua za kufuata

Utaratibu unaopaswa kufuatwa na walei wa Jumuiya ya Kipadre wa Mtakatifu Pio X ambao wamehukumiwa na wanaomba ushirika kamili na Kanisa Katoliki “unahusisha kitendo rasmi cha kufuata kikamilifu mafundisho na utii kwa uongozi wa Kikatoliki, chini ya mamlaka ya Kawaida mahalia, mdhamini wa umoja wa Kanisa Mahalia.” Kwa hivyo, mwamini mlei ambaye ameamua kuacha Jumuiya ya Kipadre  ya Mtakatifu Pio X lazima awasilishe Professio fidei na Formula adhaesionis, yaani cheti cha kufunga nadhini na kanuni ya kujiunga kilicho  na tarehe na kusainiwa, kwa Askofu wao. “Mara tu hati zitakapopatikana, Mkuu wa Eneo hilo  atamkaribisha mwaamini mlei wakati huo na kwa njia anayoona inafaa zaidi.”


Walei wasiohusika

Hati hiyo inasisitiza kwamba “yafuatayo hayapaswi kuzingatiwa: walei wanaohudhuria Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X kwa sababu za kiliturujia au za kiroho tu; walei ambao, ijapokuwa wanafahamu mivutano na Kiti Kitakatifu, hawakatai Majisterio au mamlaka ya Papa wa Roma.” Kuhusu hawa wa mwisho, itatosha kwao kumgeukia “Padre katika ushirika kamili, wakiwa na uamuzi wa kutohudhuria Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X katika siku zijazo.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

02 Julai 2026, 17:06