Kard.Parolin:"Pasaka ya Amani"ni muhimu ili kuondoa Vita,isiyostahili kamwe Mwanadamu
Na Edoardo Giribaldi – Roma.
“Pacem in terris”, "Kamwe vita isitokee tena," "mgogoro wa kimataifa uliogawanyika vipande vipande," ambao akili na utashi lazima vikabiliwe ili kutatua mgawanyiko "kama wanadamu, si kama wanyama, labda wakiwa na silaha za kiteknolojia." Haya ni maneno yaliyotumiwa na Mtakatifu Yohane XXIII, Mtakatifu Paulo VI, Papa Francisko, na Papa Leo XIV, yakiambatana na ishara za kiwango sawa: barua iliyotumwa na Mtakatifu Yohane Paulo I kwa Rais wa Marekani Jimmy Carter kuunga mkono mazungumzo ya amani ya Camp David, kati ya Israeli na Misri mwaka 1978; Mkutano wa kihistoria wa Siku ya Maombi ya Amani huko Assisi mnamo tarehe 27 Oktoba 1986, ambao uliwakutanisha kwa mara ya kwanza viongozi wa dini zote kuu za dunia, hafla iliyoanzishwa na Papa Yohane Paulo II na kufufuliwa na Papa Benedikto XVI miaka 25 baadaye.
"Mbio za kupokezana" halisi zinazokisi jinsi ambavyo mapapa wote wanaofuata Mtaguso wa Pili wa Vatican wamekuwa kama kipande cha Mosaic yaani "vipande vidogo vya picha" ya ushirika wa kimataifa, ambao, leo hii zaidi ya hapo awali, ni muhimu kuvumilia kwa kutangaza "Pasaka ya Amani." Kichwa cha kitabu kipya cha Antonio Preziosi, mwandishi wa habari na mkurugenzi wa Tg2, kilichukuliwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambaye alizungumza alasiri tarehe 22 Julai 2026, katika uwasilishaji wa kazi hiyo katika Jumba la Borromeo, nyumbani kwa Ubalozi wa Italia anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu.
Umoja wa binadamu unatangulia watu binafsi
"Pasaka ya Amani. Kuanzia Yohane XXIII hadi Papa Leo XIV kuelekea Jubilei ya 2033" ndiyo kichwa kamili cha chapisho la Toleo la Mtakatifu Paolo, ambalo Makamu Rais wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Italia, Antonio Tajani, pia alizungumzia. Hotuba ya uzinduzi ya Kardinali Parolin ilikuwa ni mfululizo wa nukuu za kihistoria kutoka kwa Mapapa waliotajwa katika kitabu hicho, kuanzia na na wa sasa, Papa Leo XIV, ambaye aliwahutubia makardinali hasa kwa (Misa di ya kuanza mkutano mkuu wa Makardinali(Concistoro,) kunako tarehe 26 Junuari 2026, kwamba aliwaelekea akisema: "Vita havistahiki kamwe kwa mwanadamu, na havibarikiwi kamwe na Mungu, kwa sababu Muumba ametujalia akili na nia ya kutatua migogoro kama wanadamu na sio kama wanyama, labda wakiwa na silaha za kiteknolojia. Umoja wa familia ya mwanadamu unatangulia watu binafsi na serikali".
Kulia kwa uovu na kunong'ona kwa amani
Kazi, ile ya Preziosi, ambayo wakati huo huo ni "zoezi la unyenyekevu katika kusikiliza", lakini pia ya umuhimu wa karibu na muhimu, katika wakati mgumu wa kihistoria ambao, kama ilivyoelezwa na Papa Leo XIV,(al Corpo Diplomatico accreditato presso la Santa Sede),kwa kikundi cha kidiplomasia kilichoidhinishwa na Vatican, mnamo Januari 9, "udhaifu wa ushirikiano wa pande nyingi ni jambo la kutia wasiwasi hasa katika ngazi ya kimataifa". Hivyo basi kuna haja ya "Pasaka ya amani" ambayo, kama Papa Leo XIV alivyokumbusha katika kitabu chake, Ujumbe wake wa Siku ya Amani Duniani(Messaggio per la Giornata Mondiale della Pace)mwanzoni mwa mwaka huu, una pumzi ya milele, kwani "wakati uovu unapigiwa kelele 'yatosha', amani inanong'onezwa 'milele.'
Nicaea na Jubilei: Hatua za Uekumeni
Kutoka kwa Mtaguso wa Nicaea mnamo 325 BK, ambao pia umepata umuhimu wa haraka kufuatia Ziara ya Papa nchini Uturuki wakati wa maadhimisho yake ya miaka 1700, hadi matarajio ya Jubilei ya Maalum ijayo mnamo 2033, Kardinali Parolin aliakisi kazi ya Preziosi katika kuchunguza "safari ya uvumilivu na ngumu ya uekumeni" kama ufunguo wa "kukabiliana na kile kinachozuia mazungumzo leo na kutuwezesha kufanya kazi ili diplomasia iweze kulenga kutatua migogoro mingi iliyopo ulimwenguni kote."
Kutoka Pacem in terris hadi "vita kamwe visirudiwe"
Tukiendelea na mapapa wa baada ya upatanisho, Kardinali alikumbuka jinsi ambavyo waraka wa Pacem in terris- 'Amani duniani' wa 1963, ulikuwa "hatua muhimu" kwa kila mwanamume na mwanamke mwenye mapenzi mema na "ushuhuda wa kiroho" wa Mtakatifu Yohane XXIII, unaofafanua upya dhana ya maelewano, kwa kuzingatia mantiki na si "nguvu za silaha." Ombi lingine la kukumbukwa lilikuwa lile lililotajwa la Mtakatifu Paulo VI, lililotamkwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York mnamo tarehe 4 Oktoba 1965: "Vita visipiganwe tena!" Wito wake huu uliimarishwa na kukumbatiana na Patriaki wa Kiorthodox Athenagoras huko Yerusalemu mnamo tarehe 5 Januari 1964, na ulikuwa wa haraka sana kiasi kwamba uliendelea hata wakati wa upapa mfupi wa Yohane Paulo I, ambaye alithibitisha kujitolea kwa Kanisa kwa ajili ya umoja wa kiekumeni, mazungumzo kati ya dini, na amani ya dunia.
Maneno na ishara ya Umoja
Katibu Mkuu wa Vatican alithibitisha tena juu ya urithi ulioachwa na Mtakatifu Yohane Paulo II , ambaye pamoja na Siku ya maombi ya amani ambayo yalisasishwa na Waraka wa (Ut unum sint wa mwezi Mei 1995, wito wa dhati kwa jumuiya za Kikristo "kuachana na mgawanyiko ili kutafuta na kugundua upya umoja, unaoendeshwa pia na uzoefu mchungu wa mgawanyiko." Bila kusahau nguvu ya ishara kama vile kuwa Papa wa kwanza kuingia katika Sinagogi la Roma, tarehe 13 Aprili 1986, na Msikiti wa Umayyad huko Damasco, tarehe 6 Mei 2001. Katika ishara dhahiri zaidi ya "kupokezana kijiti" iliyotajwa hapo juu, Kardinali Parolin alisisitiza jinsi ambavyo Papa Benedikto XVI, mnamo tarehe 27 Oktoba 2011, alivyopanua mkutano wa kihistoria wa amani ulioitishwa na mtangulizi wake ili kujumuisha wawakilishi wa ulimwengu wa utamaduni na wasioamini. Hata hivyo, Joseph Ratzinger pia alifanya ishara kuwa muhimu sana: sala katika Msikiti wa Bluu huko Istanbul mnamo tarehe 30 Novemba 2006 (pia ilitembelewa mnamo Novemba 29 iliyopita na Papa Leo XIV) na juhudi za kuhamasisha mazungumzo na Uislamu katika kuunda Jukwaa la Wakatoliki-Waislamu.
Kupokezana kijiti kati ya Papa Francisko na Papa Leo XIV
Kwa kuwa Papa Francisko, basi, tunafika katika nyakati za hivi karibuni, kwenye taswira ya "vita vya dunia vilivyogawanyika vipande vipande" alivyoviibua kwa mara ya kwanza, ambavyo vilimsukuma kujitolea kila siku kwa mazungumzo na dini na ujenzi wa amani, sambamba na Waraka wa Kitume wa Fratelli tutti, wote ni Ndugu ambamo Jorge Mario Bergoglio "anatangaza kulaani vikali kila aina ya vurugu kwa jina la dini".
Kutoka kwa Papa wa Argentina hadi mrithi wake wa Marekani, ambaye amefanya "amani na mazungumzo kuwa maneno muhimu ya Upapa wake" tangu maombi yake ya kwanza, ambayo yalilenga "amani isiyo na silaha na kupokonya silaha." Ahadi ya kawaida kwa Kanisa zima na kuthibitishwa na Papa Leo XIV "katika hotuba zake zote, nyaraka na safari," pia akinyooshea kidole "vita vilivyosahaulika" na vyombo vya habari wakati waZiara yake ya kitume ya hivi karibuni barani Afrika mnamo mwezi Aprili uliopita. Na ilikuwa ni kwa waandishi wa habari, Kardinali Parolin alikumbusha, kama ilivyotokea kwenye hafla ya mkutano uliotolewa kwa washiriki wa timu ya wahariri ya Tg2 tarehe 16 Machi 2026 ambapo Papa Leo XIV alikumbusha "hitaji la kuzungumza juu ya vita kupitia macho ya waathrika na wale wote wanaoteseka kwa sababu yao."
"Ndoto" ya Jubilei ya 2033
Baada ya kukamilisha muhtasari huu, Kardinali Parolin alikakisi kwa kiasi flani fursa ya kutafakari juu ya haja ya kufanya kazi ili kuondokana na matatizo yote ya kihistoria ambayo yametatiza mchakato wa ukaribu wa kiekumeni kati ya dini za Kikristo": Sherehe ya wakati mmoja, mnamo tarehe 20 Aprili 2005, ya Pasaka kwa "madhehebu yote ya Kikristo." Kama Preziosi anavyoandika, hii si "ufundi" rahisi, bali ni msukumo wa kutafuta "kushinda migawanyiko ya kihistoria kwa jina la imani ya pamoja,"ambayo inaona Jubilei ya 2033 kama lengo la kutimiza "ndoto" ya Pasaka ya pamoja katika miaka miwili ya Ufufuko.
Uponyaji pale ambapo kuna majeraha
Upeo ambao Kardinali Parolin alikumbatia kwa matumaini sawa, akisisitiza zaidi kwa maneno ambayo Papa Leo XIV alizungumzia kwa(ai partecipanti alla settimana ecumenica di Stoccolma)Washiriki wa Mkutano wa Juma la Kiekumeni huko Stocolm mnamo tarehe 22 Agosti 2025 kuhusu maadhimisho ya miaka mia moja ya mkutano wa kiekumene wa 1925: “kwa sababu wafuasi wa Kristo wameitwa kuwa wasanifu wa upatanisho: kukabiliana na mgawanyiko kwa ujasiri, kutojali kwa huruma, na kuleta uponyaji pale ambapo pamekuwa na majeraha.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.