Ask.Mkuu Gallagher atoa heshima kwa Waathiriwa wa Vita kuanzia 2014 hadi sasa

Julai 20,ikiwa ni siku ya mwisho ya safari ya Askofu Mkuu Gallagher huko Ukraine alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Rais Zelensky huko Kyiv.Katika ukumbusho wa Maidan kwa wahanga wa mapinduzi ya 2014 na vita vilivyoanza mwaka 2022,kufuatia uvamizi wa Urusi,aliweka shada la waridi kwa kumbukumbu ya wale waliouawa.Julai 19 usiku,mkutano na Baraza la Makanisa na Mashirika ya Kidini la Ukraine ulifanyika.

Na Roberto Paglialonga – Mwakilishi Kyiv

Kwa heshima ya kumbukumbu ya wathiriwa wa mapinduzi ya Maidan ya 2013-2014 na vita vinavyoendelea - vilivyoanzishwa na Urusi mnamo 2014 na kuzidi Februari 2022 katika  siku ya tano na ya mwisho ya utume huko Ukraine kwa Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ilianza asubuhi tarehe 20 Julai 2026, huko Kyiv.

Askofu Mkuu Gallagher amekuwa huko kama  mjumbe maalum wa Papa Leo XIV kwa ajili ya maadhimisho katika Madhabahu ya Mlima Karmeli,  huko Berdychiv (kilomita 180 kutoka mji mkuu) kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 35 tangu kufunguliwa tena kwa miundo ya Kanisa Katoliki la Ibada ya Kilatini nchini humo. Misa ya wazi mbele ya madhabahu kwa Maria Mama wa Mungu ilifanyika Dominika tarehe 19 Julai 2026 mbele ya zaidi ya watu elfu 3.

L'arcivescovo Gallagher con il ministro degli Affari esteri ad interim dell'Ucraina Sibyha

Askofu Mkuu Gallagher akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Sibyha

Mikutano na Rais Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje

Ziara ya kumbukumbu hiyo, iliyoko karibu na Maidan, iliambatana na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje Andriy Sibyha, ambaye Askofu Mkuu Gallagher alikutana naye baadaye kwa ajili ya mkutano wa pande mbili. Wakati wa mkutano huo, ukaribu wa Vatican na watu wa Ukraine ulirudiwa, hasa katika wakati huu wa vita, Vatican ikielezea matumaini kwamba amani ya haki na ya kudumu itapatikana haraka iwezekanavyo. Baadaye asubuhi hiyo,  Askofu Mkuu Gallagher alikutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.


Mkutano na Baraza la Makanisa na Mashirika ya Kidini la Ukraine Yote

Mkutano ulifanyika tarehe 19 Julai  jioni na Baraza la Makanisa na Mashirika ya Kidini kwa Ukraine Yote. Wawakilishi walijadili changamoto zinazoendelea ambazo wao, pamoja na idadi ya watu, wanakabiliana nazo na ushirikiano mzuri ulioanzishwa kati ya madhehebu mbalimbali ya kidini. Walielezea kuwa tatizo kuu linabaki kuwa vita. "Watu wamechoka" walisisitiza, "na bado tunajaribu kuishi kwa heshima na kwa hamu ya kuanza upya kila siku."Hakuna anayetaka amani zaidi yetu, lakini lazima iwe amani ya haki." Kisha wakishukuru Vatican, Balozi wa Vatican nchini Ukraine, Visvaldas Kulbokas, kwa kazi yao, usaidizi wa mara kwa mara, na usaidizi katika nyakati hizi za migogoro, walisisitiza umuhimu wa kuendelea kupokea usaidizi wa kiroho na maombi, huku pia wakisisitiza hitaji la kuweza kuwaomba viongozi wa kisiasa, kupitia diplomasia, kujitolea zaidi na zaidi kukomesha mgogoro huo.

Un momento dell'incontro al ministero degli Affari Esteri

Wakati wa Mkutano na Waziri wa mambo ya Nje wa Ukraine 

Kuondolewa kwa Watu wa Dini kutoka Jeshini

Mafanikio ya Baraza hasa ni katika kuwaondoa wahudumu wa masuala matakatifu kutoka katika huduma ya kijeshi ni muhimu. "Serikali na mamlaka za kisiasa zimeonesha uelewa wao wa umuhimu wa Makanisa, wakitambua jukumu lao kama huduma muhimu kwa watu binafsi na msaada kwa idadi ya watu," walisema. Askofu Mkuu Gallagher alitoa motisha kwa matokeo halisi yaliyopatikana, ambayo si mara zote hutolewa, hasa wakati wa vita.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

21 Julai 2026, 12:24