Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 29 Julai 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda, nchini DRC kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kabinda. Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 29 Julai 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda, nchini DRC kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kabinda.  (ANSA)

Askofu Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda, DRC

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 29 Julai 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda, nchini DRC kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kabinda na kwamba, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Gambera wa Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Charles Borromée huko Kabinda. Alizaliwa tarehe 14 Februari 1974. Akapewa Daraja ya Upadre 28 Agosti 2005. Papa Leo tarehe 29 Julai 2026 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo la Kabinda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 29 Julai 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda, nchini DRC kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Kabinda na kwamba, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Gambera wa Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Charles Borromée huko Kabinda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Eustache Ntambwe Makoyo, wa Jimbo Katoliki Kabinda alizaliwa tarehe 14 Februari 1974 huko Musoshi, nchini DRC. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 28 Agosti 2005 akapewa Daraja ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Kabinda.

Baraza la Maaskofu nchini DRC
Baraza la Maaskofu nchini DRC

Katika maisha na utume wake kama Padre amewahi kuwa ni Gambera msaidizi wa Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Charles Borromée huko Kabinda kati ya Mwaka 2005 hadi mwaka 2006. Kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa maisha ya kiroho Seminari ndogo ya Mtakatifu Papa Pio X na Mwenyekiti wa Tume ya Kijimbo ya Liturujia. Baadaye alitumwa mjini Roma kwa masomo ya juu zaidi katika muziki mtakatifu na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamili mwaka 2021 kutoka katika Taasisis ya Muziki Mtakatifu, Roma. Baadaye alijiendeleza tena katika sanaa ya muziki na Liturujia kutoka Taasisi ya Kipapa ya Liturujia na huko akajipatia Shahada ya Uzamili.

Baraza la Maaskofu nchini DRC
Baraza la Maaskofu nchini DRC

Baadaye aliamua kwenda kujiendeleza zaidi katika masuala ya Muziki kwenye Chuo Kikuu cha Tor Vergata, kilichoko mjini Roma na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kunako mwaka 2025. Akiwa nchini Italia alifanya utume wake kwenye Jumuiya ya: “Tre Archi angeli huko Livorno.” Na tangu mwaka 2025 hadi kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu XIV tarehe 19 Julai 2026 alikuwa ni Gambera alikuwa wa Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Charles Borromée huko Kabinda nchini DRC.

Uteuzi DRC
30 Julai 2026, 14:39