2022.11.28 RIUNIONE DEI PRESIDENTI DELLE RIUNIONI INTERNAZIONALI DELLE CONFERENZE EPISCOPALI E COORDINATORI DELLE TASK FORCE CONTINENTALI CON LA SEGRETERIA GENERALE DEL SINODO

Sinodi:siku tatu za kazi jijini Roma na viongozi wahusika wa bara

Mkutano huo unaanza Juni 23, na utahitimishwa Alhamisi tarehe 25 Juni 2026 na mazungumzo kati ya Papa Leo XIV na washiriki katika Sekretarieti Kuu ya Sinodi.

Vatican News

Tukiangalia mbele Mikutano ya Kanisa ya 2027-2028, kufuatia kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI mnamo Oktoba 2024, Sekretarieti Kuu ya Sinodi - kama ilivyoelezwa katika taarifa - ​​imeamua kuwaleta pamoja Roma, kuanzia Juni 23, hadi tarehe 25, viongozi wa vyombo vya bara (CELAM, SECAM, FABC, CCEE, FCBCO, n.k.), wanaowakilisha Amerika Kusini, Afrika, Asia, Ulaya, Oceania, Mashariki ya Kati, na Amerika Kaskazini, wakifuatana na waratibu wa timu za sinodi za bara. Mkutano huo utazingatia chapisho la hivi karibuni la“Verso le Assemblee 2027-2028. Tappe, criteri e strumenti per la preparazione”)  -"Kuelekea Mikutano ya 2027-2028. Hatua, vigezo na zana za maandalizi.") Baba Mtakatifu Leo XIV Alhamisi tarehe 25 Juni 2025 atakutana na washiriki na atazungumza na wao katika Ofisi ya Sekretarieti Kuu ya Sinodi.

Kubadilishana uzoefu na mazoea

Katika siku hizi tatu watafanya kazi ya kubadilishana uzoefu unaoendelea na kutambua mienendo ya pamoja na masuala ambayo yanahitaji uchambuzi wa kina wa pamoja kuanzia kusikiliza maendeleo katika utekelezaji wa (Documento finale della XVI Assemblea Generale Ordinaria del Sinodo dei Vescovi) - Hati ya Mwisho ya Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu. Sehemu ya kazi, iliyopangwa katika vikao vya jumla na vikundi vya kazi, itajitolea kusaidia Makanisa  mahalia na makundi ya Makanisa, kwa kuzingatia hasa jukumu la mawasiliano. Siku ya mwisho, washiriki watajadili Makusanyiko ya Bara, ya hatua katika mchakato mpana wa makusanyiko ya Kanisa itakayofikia kilele katika Mkutano Mkuu wa Oktoba 2028, hasa, vigezo vya ushiriki na suala la uwakilishi, matokeo yanayotarajiwa, na jukumu la Sekretarieti Kuu.

Mkutano wa Sinodni 23-25 mjini Vatican

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

23 Juni 2026, 09:24