Kard.Parolin:Kumweka wakfu wa kiaskofu wa Askofu Mkuu Pegoraro
Vatican News
Neno la Yesu la leo, linalotangazwa katika makanisa yote duniani, pia linasikika katika mahali patakatifu pa Mtakatifu Maria wa Mungu Mpaji, huko Sarmeola ya Rubano, likitualika tusiogope, bali tutangaze ujumbe wake hadharani bila kuionea haya Injili yake mbele ya watu. Alisema hayo Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, wakati wa kumweka wakfu wa Kiaskofu, Askofu Mkuu Renzo Pegoraro, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha(PAV). Tukio hilo lilifanyika Domiika tarehe 21 Juni 2026 ambapo Kardinali Parolin aliongoza ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu katika Kanisa moja la Padova, sehemu moja ya Kituo cha Kiafya kiitwacho Kazi ya Mungu Mpaji cha Mtakatifu Antoni (OPSA). Katika kituo hicho, ambacho kinahifadhi takriban watu 600 wenye udhaifu na ulemavu, Askofu huyo alijitolea kama daktari wakati wa miaka yake ya seminarini, huku akiwasaidia wakazi na bado anaongoza kamati ya maadili.
Udhaifu wa Kukaribisha
Hii ndiyo sababu uchaguzi wa kufanya misa katika kituo hicho (OPSA) kwamba haukuwa kwa bahati mbaya, Katibu wa Vatican alisisitiza katika mahubiri yake, kutokana na kwamba "nyumba hii nzuri inakaribisha aina mbalimbali za udhaifu wa binadamu na inawajali kwa kiwango cha juu cha taaluma na umakini maalum kwa upekee wa kila mgeni," ikiwakilisha ishara" ya kile ambacho Chuo cha Kipapa kinahifadhi katika utafiti." Kardinali Parolin alirudia, kuwa "Tunaweza karibu kusema," "kwamba uendelezaji wa maisha, ambao Chuo cha Kipapa kinahakikisha kupitia utafiti na uzalishaji wa kisayansi, hapa umejumuishwa katika usaidizi na usaidizi ambao OPSA inawapa wageni wake: karibu pande mbili za sarafu moja, vivuli viwili vya kujitolea kwa kipekee ambayo Mungu Baba anahakikisha kwa kila mwanaume na mwanamke. Na hakika ni jambo la kupongezwa sana kwamba huduma yako ya kiaskofu inachukua hatua zake za kwanza kiishara kuanzia hapa."
Msiogope kutenda mema
Akichukua msukumo kutoka katika usomaji wa Injili, Katibu Mkuu wa Vatican alihimiza kuwa: "Tusiogope kuwatendea wengine mema, tusiwaogope wale "wanaopanga njama kwa siri" au wale "wanaoua mwili." Ujasiri, hautoki ghafla kutoka katika roho yetu isiyo na woga, lakini umejikita katika uhakika usiotetereka kwamba maisha ya wanafunzi wa Yesu yanalindwa na uaminifu usioisha wa Baba. Yesu ana uhakika kwamba Mungu ndiye mlinzi mwenye wivu wa maisha ya mwanadamu na anajua kwamba hakuna nguvu ya mwanadamu inayoweza kuyatoa kutoka kwa utunzaji Wake. Hakika, kama vile mama anavyo na ujuzi wa 'kiwango cha milimita' kuhusu mtoto wake, vivyo hivyo Mungu anajali hata maelezo yanayoonekana kuwa madogo sana." Na hasa wanafunzi wa seminari vijana kutoka "Seminari ya Pamoja" iliyoko karibu na Kituo hicho(OPSA), ambao walihudumu katika madhabahuni Juni 21. Kardinali Parolin aliwakumbusha hao kwamba "Mungu Baba amewachagua ninyi na anaahidi utunzaji mpole zaidi kwa kila mmoja wenu,"huku akinukuu maneno ya Mtakatifu Paulo, ambaye "alielewa upyaisho wa wito wake mwenyewe kama huduma ya upatanisho na amani."
Akipiga Magoti mbele ya Mungu na jirani
Hatimaye, Kardinali Parolin alikumbuka Ziara ya kitume ya Papa Leo XIV kwenda Hispania, ambapo "aliwahimiza Wakristo wote wasiogope kufanya maamuzi ya kiinjili ya ujasiri." Miongoni mwa mapendekezo mengi yaliyopokelewa, Kardinali alikumbuka picha halisi kuwa "iliyonigusa mimi binafsi na kwa namna fulani inaweza kuunda aina ya mchanganyiko na ujumbe. Katika Uwanja wa Cibeles huko Madrid, mbele ya umati usio na mipaka, wakati wa mahubiri yake ya sherehe ya Mwili na Damu ya Kristo(Corpus Christi,) Papa Leo XIV alizungumzia udini wa nchi hiyo kama 'shule ya imani ambayo tunaweza kuitoa hata leo.' Shule inayotufundisha kupiga magoti mbele ya Mungu na mbele ya jirani yetu, kwa sababu hakuna mtu anayeweza kupiga magoti mbele ya Bwana na kumdharau ndugu yake; shule inayotufundisha upendo usio na kifani unaokuwa zawadi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.